mwana wa liganga blog ni blog ya kutoa taarifa, matukio, yaliyotokea katika ulimwengu hususani katika nchi yaTanzania blog hii inasimamiwa na mwandishi wa habari kitaaluma bwana Deus Thomas liganga.lengo ni kutoa taarifa kwa umma,kwa maendeleo ya taifa na Dunia kwa ujumla kwa mawasiliano kuhusu mtangazo, habari, wasiliana nasi 0659944423,deusliganga@yahoo.com,mzeeliganga@gmail.com
Jumatano, 12 Septemba 2018
Vijue vinywaji vya ajabu vinavyotamba duniani
1. The Sourtoe Cocktail
Hicho ni kinywaji kinachopatikana katika Jiji la Dawson, Canada, maeneo ya Yukon. Kinywaji hicho huwa kina kidole cha mguu wa binadamu ndani yake ambacho kimekolezwa chumvi. Kiuhalisia, hutakiwi kukila kidole hicho, japokuwa wengine huvila kwa bahati mbaya. Lakini wakati unamalizia kinywaji hicho kwenye bilauri, ni dhahiri kidole hicho kitagusa midomo yako!
2. Snake Wine
Hiyo ni divai (wine) inayopatikana nchini Vietnam, ambayo ndani yake huwekwa nyoka wazima, wakabakia humo wakiwa wazima au wamekufa. Wanywaji wasioogopa, hunywa divai hiyo na kuwala nyoka hao.
3. Seagull Wine
Hii ni divai inayotumiwa na Waeskimo ambapo ndani yake hutumbukizwa ndege wa baharini aliyekufa kwa ajili ya kuikoleza. Kwa hiyo, wanywaji huamua wenyewe matumizi ya ndege huyo.
4. Lizard Wine
Hii ni divai inayotokana na mchele ambayo inatumiwa nchini China. Ndani yake hujazwa mijusi ambapo mchanganyiko huo hudaiwa kumlinda mnywaji dhidi ya mapepo mabaya.
5. Chicha de Muko
Hii ni pombe ya mahindi ambayo kutayarishwa kwake ni pamoja na kuyatafuna mahindi na kisha kuyatemea kwenye chombo maalum ambamo huwekwa na kuchanganywa na vitu vingine hadi inakuwa pombe.
6. Kumis (Fermented Mare’s Milk)
Hii ni pombe itokanayo na maziwa ya farasi yaliyowekwa hadi yakachachuka, inatumiwa na watu wa Mongolia.
7. Yak Butter Tea
Hii ni chai inayotumiwa huko Tibet ikiwa ni mchanganyiko wa siagi, majani ya chai na chumvi ambavyo huongezewa ngano iliyokaangwa na maziwa ya mtindi.
8. Bilk (Milk Beer)
Hii ni bia inayotumiwa nchini Japan ikiwa ni mchanganyiko wa maziwa, shayiri na mimea ya mihopi (hop).
9. The Aunt Roberta cocktail
Hiki ni kinywaji cha mchanganyiko wa gin, vodka, brandy, matunda aina ya absinthe na blackberry. Kinatumika pia kusafishia vyombo ikiwa ni pamoja na kudeki sakafu.
Jumanne, 11 Septemba 2018
MASHINDANO MAPYA ULAYA;
Chama cha Soka Barani Ulaya (UEFA) kimesema kipo kwenye hatua za
mwisho kuja na michuano mipya kwa ngazi ya vilabu barani humo, ambayo
itakuwa ni michuano ya tatu kwa ukubwa baada ya #UEFAChampionsLeague na #EuropaLeague.
Mkuu wa Chama cha Vilabu barani Ulaya (ECA) Andrea Agnelli ndiye
aliyetoa taarifa hiyo kwenye mkutano mkuu wa mwaka wa chama hicho
unaofanyika nchini Croatia, lakini hajaweka wazi mfumo wa mashindano
hayo utakavyokuwa.Pichani ni Benjamani Mkapa akila kiapo Cha Kuwa Balozi wa Tanzania Nchini Nigeria Mbele ya Rais Julius Kambarage Nyerere IKULU Jijini Dar Tarehe 18-10-1976,Katikati ni Katibu mkuu kiongozi wa Rais Wakati huo Ndugu Timothy Opiyo.
Pichani ni Benjamani Mkapa akila kiapo Cha Kuwa Balozi wa Tanzania Nchini Nigeria Mbele ya Rais Julius Kambarage Nyerere IKULU Jijini Dar Tarehe 18-10-1976,Katikati ni Katibu wa Rais Wakati huo Ndugu Timothy Opiyo.
GABON: MTANGAZAJI AJIUA BAADA YA KUTOLIPWA MSHAHARA KWA MIEZI 15 (MWAKA 1 NA MIEZI 3)
Mtangazaji wa Kituo cha Redio nchini Gabon (Redio Gabon) amejiua baada ya kutolipwa mshahara kwa miezi 15
Marius Pierre Foungues alikuwa Mtangazaji wa kipindi cha “Succès du temps passé” kilichokuwa kikirushwa kila siku za Jumapili asubuhi
Mwanahabari huyo alikuwa akikabiliwa na hali ngumu ya maisha ikiwa ni pamoja na matatizo ya kiafya
SHAMBULIO LA SEPTEMBA 11: MIAKA 17 BAADAYE, BADO MAJERAHA HAYAJAPONA
Miaka 17 imepita tangu dunia ilipotingishika kufuatia mashambulizi makubwa ya kigaidi yaliyolenga jengo refu zaidi duniani, World Trade Centre jijini New York na Jengo la Wizara ya Ulinzi (Pentagon) jijini Washington.
Leo Wamarekani wakiongozwa na Rais Donald Trump, wataadhimisha kumbukumbu ya tukio hilo lililotokea Septemba 11, 2001 ambapo zaidi ya watu 3000 walipoteza maisha, shughuli itakayofanyika Shanksville, Pennsylvania nchini humo.
Japokuwa siku nyingi zimepita, bado jinamizi la tukio hilo linaendelea kuwasumbua Wamarekani wengi, hasa wale waliopoteza ndugu zao kwenye tukio hilo baya zaidi katika historia ya ugaidi duniani huku wengine wakiachwa na ulemavu wa kudumu.
Katika maadhimisho hayo, watu wote watasimama kimya kwa dakika moja kuwaenzi wote waliopoteza maisha katika tukio hilo, huku majina ya watu wote waliopoteza maisha yakitajwa.
Wamarekani wengi wameendelea kuisisitiza serikali yao kuhakikisha tukio kama hilo halijirudii ndani ya ardhi ya nchi hiyo na kufanya kila kinachowezekana kukomesha ugaidi duniani kote.
Mshukiwa mkuu wa matukio hayo, Osama bin Laden aliyekuwa kiongozi wa Kundi la Al Qaeda, aliuawa Mei 2, 2011 Abbottabad, Pakistan na majeshi ya Marekani chini ya Rais Barrack Obama, katika oparesheni iliyopewa jina la Neptune Spear.
Maalimu Seif Kuchukua fomu kupitia Chadema | CUF na CHADEMA ni kitu kimoja
Mwenyekiti waBaraz la wazee Chadema Bw. Hashimu Juma amedai kuwa chadema na CUF ni kitu kimoja hivyo basi kama CCM wakifanikiwa kumtoa maalim seif zanzibar basi kutokana na wao kuwa kitu kimoja maalimu atachukua fomu kupitia chama hiko cha chadema pamoja na viongozi wengine wote wa maalim seif.
Beki wa Manchester United kukosa mechi hizi baada ya kupata majeraha
Beki wa kushoto wa klabu ya Manchester United na timu ya taifa ya
England Luke Shaw aliyepata mshtuko baada ya mgongano wa bahati mbaya na
beki wa Uhispania Dani Carvajal katika nusu ya pili ya mchezo
uliowakutanisha miamba hao wawili ambapo England akiwa nyumbani
alifungwa goli 2-1 na Hispania
Baada ya majeraha hayo ya kichwa Shaw alirudi United kwa ajili ya ufuatiliaji zaidi na matibabu siku ya Jumatatu licha ya beki huyo kuumia wakati anaitumikia timu yake ya taifa.
akiongea na wanahabari kocha wa timu ya taifa ya England Gareth Southgate alisema ” Hakuna mtu aliyetamani kuona tukio kama hilo”na kuongeza kuwa Shaw alitolewa uwanjani akiwa amefungwa vifaa vya kumuingizia hewa ya oksijeni lakini alisema kuwa amepata tena ufahamu haraka katika chumba cha matibabu, na hivi karibuni alikuwa akiwasiliana na marafiki na familia.
Baada ya beki huyo kisiki mwenye ustadi wa aina yake kuumia katika mchezo huo wa jumamosi dhidi ya Uhispani huku kocha wake Jose Mourinho akishuhudia jukwaani, msaada wa beki huyo utakosekana katika timu yake ya Manchester United katika mchezo wao wa siku ya jumamosi dhidi ya Watford,hivyo Luke Shaw hatakuwepo kwenye mchezo huo utakaofanyika katika dimba linalomilikiwa na The Golden Boys au jeshi la njano Watford linalojulikana kama Vicarage Road Stadium.
Siku chache kabla, Shaw alikuwa amefungua hadithi ya hofu ya mguu wake uliovunjika, ambalo alikiri alikuwa karibu na kumchukuliwa na kumlazimisha kufikiria kustaafu kutoka mchezo huo kwa umri wa miaka 23 tu.
Baada ya majeraha hayo ya kichwa Shaw alirudi United kwa ajili ya ufuatiliaji zaidi na matibabu siku ya Jumatatu licha ya beki huyo kuumia wakati anaitumikia timu yake ya taifa.
akiongea na wanahabari kocha wa timu ya taifa ya England Gareth Southgate alisema ” Hakuna mtu aliyetamani kuona tukio kama hilo”na kuongeza kuwa Shaw alitolewa uwanjani akiwa amefungwa vifaa vya kumuingizia hewa ya oksijeni lakini alisema kuwa amepata tena ufahamu haraka katika chumba cha matibabu, na hivi karibuni alikuwa akiwasiliana na marafiki na familia.
Baada ya beki huyo kisiki mwenye ustadi wa aina yake kuumia katika mchezo huo wa jumamosi dhidi ya Uhispani huku kocha wake Jose Mourinho akishuhudia jukwaani, msaada wa beki huyo utakosekana katika timu yake ya Manchester United katika mchezo wao wa siku ya jumamosi dhidi ya Watford,hivyo Luke Shaw hatakuwepo kwenye mchezo huo utakaofanyika katika dimba linalomilikiwa na The Golden Boys au jeshi la njano Watford linalojulikana kama Vicarage Road Stadium.
Siku chache kabla, Shaw alikuwa amefungua hadithi ya hofu ya mguu wake uliovunjika, ambalo alikiri alikuwa karibu na kumchukuliwa na kumlazimisha kufikiria kustaafu kutoka mchezo huo kwa umri wa miaka 23 tu.
Ajali ya Gari la Kubeba Mbao Yaua Watu Wanne Rombo
Na Dixon Busagaga,Rombo.
Watu
wanne wakiwemo wawili wa familia moja wamefariki dunia papo hapo baada
ya gari walilokuwa wakisafiria aina ya Isuzu kuacha njia na kwenda
kugonga gema katika eneo la Kikelelwa wilayani Hai.
Waliofariki dunia wametambulika kwa majina ya Emanual Josephat Silayo (28) ,Viviano silayo (35) wakazi wa Mbomai Juu,Juma Idd (20) maarufu kama mwarabu na mwingine aliyefahamika kwa jina moja la Deolla .
Kamanda
wa polisi mkoa wa Kilimanjaro Hamis Issah aliyefika eneo la tukio
amethibitisha kutokea kwa ajalo hiyo na kwamba dereva wa Loli hilo
lililokuwa limebeba mbao alikimbia kusiko julikana baada ya ajali..
"Jitihada
za kumtafuta dereva zinafanyika na chanzo cha ajali ni kupoteza
muelekeo kwa Lori hilo na baadae kugonga Gema ndipo watu waliokuwa
wanmekaa mbele walichomoka na kwenda kupigiza vichwa katika Gema na
kupasuka"alisema Kamanda Issah.
Kamanda
Issah amesema gari hilo likiwa na shehena ya mbao lilikuwa likitokea
eneo la West Kilimanjaro ,eneo maarufu kwa uchanaji wa mbao na kwamba
lilikiwa likielekea Rombo kupitia njia ya Rongai.
"Ni
gari la kubeba mbao lilikua linatoka West Kilimanjaro kupitia njia ya
Kikelelwa wilayani Rombo ,Gari aina ya Isuzu likiwa na namba za usajili T
889 ACN lilimshinda dereva na kuacha njia na baadae kugonga ngema
iliyosababisha watu wanne waliokuwemo katika gari hilo kufa papo hapo."
alisema Kamanda Issah.
Miili ya marehemu wote imehifadhiwa katika hosptali ya wilaya ya Rombo kwa ajili ya maandalizi ya mazishi.
Kuna uwezekano mkubwa wa kutokea El Nino mwishoni mwa mwaka huu:WMO
Mwishoni
mwa waka huu wa 2018 kuna uwezekano mkubwa wa kuzuka matukio ya El Nino
kwa mujibu wa takwimu mpya zilizotolewa leo na shirika la hali ya hewa
duniani WMO.
Shirika
hilo linasema uwezekano wa kuzuka kwa hali hiyo ni asilimia 70 na
taarifa za mapema zitazisaidia jamii kujiandaa na matukio yanayoambatana
na hali hiyo kama mvua kubwa, mafuriko na ukame.
Kwa mujibu wa katibu mkuu wa WMO Petteri Taalas, mabadiliko ya tabia nchi yanachangia kwa kiasi kikubwa kubadilisha mzunguko wa matukio ya El Nino na La Nina pamoja na athari zake katika jamii.
Kwa mfano amesema mwaka 2018 ulianza na hali dhaifu ya La Nina lakini hali hiyo haikutosheleza kupunguza mwenendo wa joto Kali lililotawala na hii ikimaanisha kwamba mwaka 2018 uko mbioni kuwa moja ya miaka yenye joto la kupindukiaduniani.
Mabadiliko hayo pia yamesababisha kuendelea kwa matukio mengine kama mafuriko makubwa Japan, India na Kusini mwa Asia, pia moto wa nyikani uliosababisha harasa kubwa Marekani ikiwemo kukatili maisha ya watu.
Hata hivyo WMO inasema haitarajii hali ya El Nino kuwa mbaya zaidi kama ilivyokuwa 2015-216 lakini bado italeta athari kubwa, ingawa shirika hilo linaamini utabiri huu wa mapema utasaidia kuokoa maisha na kupunguza athari za kiuchumi.
Hii ni mara ya kwanza WMO inajumuisha utabiri wa El Nino katika mtazamo wake wa kimataifa wa hali ya hewa kwa msimu wa Septemba hadi Novemba.
Kwa mujibu wa katibu mkuu wa WMO Petteri Taalas, mabadiliko ya tabia nchi yanachangia kwa kiasi kikubwa kubadilisha mzunguko wa matukio ya El Nino na La Nina pamoja na athari zake katika jamii.
Kwa mfano amesema mwaka 2018 ulianza na hali dhaifu ya La Nina lakini hali hiyo haikutosheleza kupunguza mwenendo wa joto Kali lililotawala na hii ikimaanisha kwamba mwaka 2018 uko mbioni kuwa moja ya miaka yenye joto la kupindukiaduniani.
Mabadiliko hayo pia yamesababisha kuendelea kwa matukio mengine kama mafuriko makubwa Japan, India na Kusini mwa Asia, pia moto wa nyikani uliosababisha harasa kubwa Marekani ikiwemo kukatili maisha ya watu.
Hata hivyo WMO inasema haitarajii hali ya El Nino kuwa mbaya zaidi kama ilivyokuwa 2015-216 lakini bado italeta athari kubwa, ingawa shirika hilo linaamini utabiri huu wa mapema utasaidia kuokoa maisha na kupunguza athari za kiuchumi.
Hii ni mara ya kwanza WMO inajumuisha utabiri wa El Nino katika mtazamo wake wa kimataifa wa hali ya hewa kwa msimu wa Septemba hadi Novemba.
Kofi Annan kuzikwa Ghana, Alhamisi
Mwili wa aliyewahi kuwa Katibu Mkuu
wa Umoja wa Mataifa Kofi Annan, ambaye alifariki mwezi uliopita,
umewasili katika nchi aliyozaliwa, Ghana.
Mwili wake uliwasili
katika Uwanja wa Ndege wa Kotoka International Airport mjini Accra,
ukisindikizwa na familia yake na maafisa wengine wa Umoja wa Mataifa.Anatarajiwa kuzikwa kitaifa siku ya Alhamisi.
Kulikuwa na hali ya maombolezowakati mwili wake ukiwasili uwanjani hapo na kupokelewa na Rais wa Ghana Akufo Addo na viongozi wa kimila na kwa heshima ya kijeshi.
Mwili wake umehifadhiwa katika Ukumbi wa Kimataifa wa mikutano wa Ghana, wakati ukisubiri kuzikwa.
kofi Annan alikuwa ni Katibu mkuu wa kwanza wa Umoja wa Mataifa, kutoka katika eneo la kusini mwa jangwa la Sahara na kuleta mafanikio sio tu katika bara la Afrika, lakini pia dunia nzima.
Aliwahamasisha vijana wengi nchini mwake na waliheshimu kile alichosimamia.
Atandikwa viboko kwa kumpa kichanga pombe kali
Picha ya Mtandao
MKAZI wa Kijiji cha Buzirayombo wilayani Chato, mkoani Geita, Makubi Wanjala (25) amecharazwa viboko vitano kwenye makalio baada ya kubainika kumpa pombe kali mtoto wa miezi minane.
Kijana huyo ambaye ni mvuvi wa samaki kwenye mwalo wa Chato Beach, alikutana na kichapo hicho jana, majira ya saa tatu asubuhi eneo la mwalo huo baada ya kuomba kumbeba mtoto huyo kabla ya kumnywesha pombe kali aina ya "Shimha".
Akizungumza na gazeti hili, Mwenyekiti wa kitongoji cha Kalema, Fares Kabunazi, alisema akiwa kwenye majukumu yake ya kawaida alipokea simu kutoka kwa mmoja wa wavuvi kuwa anahitajika haraka eneo la mwalo wa Chato Beach na kuelezwa kuna dharura imejitokeza eneo hilo.
Baada ya kufika eneo la tukio alimshuhudia mtoto wa miezi minane (jina tunalihifadhi) akiwa amelegea kutokana na kupewa pombe hiyo.
Kiongozi huyo alifanikiwa kunusuru maisha ya kijana huyo baada ya kuuzuia umati wa wananchi waliokuwa wamekusanyika eneo hilo wakiwa na lengo la kumdhuru kijana huyo kutokana na kitendo chake cha kumnywesha pombe mtoto mdogo.
"Kutokana na jazba walizokuwa nazo wananchi na baada ya kumsikiliza mtuhumiwa pamoja na mama mzazi wa mtoto huyo, niliamua kutoa amri ya kucharazwa viboko vitano kwenye makalio yake na kumfukuza kufanya shughuli za uvuvi kwenye mwalo huo," alisema Kabunazi.
Akisimulia mkasa huo, mama mzazi wa mtoto hiyo, Husna Ally (28), alisema kijana huyo alifika dukani kwake na kukaa kwenye moja ya viti vilivyoko eneo hilo, huku akitumia pombe kali iliyoko kwenye kifungashio cha chupa ya plastiki na kuomba kumbeba mtoto huyo.
"Alipofika hapa dukani kwangu pamoja na pombe yake aliniomba kumbeba mtoto wangu...bila kuelewa kinachoendelea, nilimpa mtoto kwa nia njema kabisa, lakini baadaye ndiyo nilishangaa kumwona akimnywesha mwanangu pombe, huku mtoto akiendelea kulegea...ndipo baadhi ya wananchi walivyoona hali hiyo wakampigia simu mwenyekiti wetu wa kitongoji," alisema Husna.
Kwa upande wake kijana huyo, Makubi Wanjala, alikiri kumnywesha mtoto huyo pombe kwa madai hakujua kama ni kosa na kudai alimpa kiasi kidogo tu cha pombe hiyo.
Hata hivyo, alisema anajutia kosa hilo kutokana na kucharazwa bakora tano kwenye makalio kwa kuwa aliamini alikuwa akiburudika baada ya kumaliza kazi ya uvuvi.
Kwa mujibu wa Sheria ya Mtoto ya mwaka 2009 Ibara ya 13 kifungu kidogo cha (1), mtu yeyote haruhusiwi kumtesa mtoto au kumfanyia vitendo vingine vya ukatili, kumpa adhabu za kinyama au kumdhalilisha ikiwa ni pamoja na kumfanyia mambo ya kimila yanayoondoa utu wake au yenye madhara katika ustawi wake kimwili au kiakili.
Mama Samia awataka Wananchi kuchukua tahadhari juu ya ugonjwa wa Ebola
Makamu wa Raisi wa Tanzania Samia Suluhu Hassan amewataka wananchi mkoani Kigoma kuchukua tahadhari ya ugonjwa wa ebola kwa kutopokea wageni kiholela wanaoingia nchini bila kufuata utaratibu wa kisheria.
Samia ametoa wito huo wakati akizungumza na wananchi wa Kijiji cha Mwakizega wilayani Uvinza na kuwataka kufuata ushauri wa wataalamu wa afya juu ya njia za kujikinga na ugonjwa huo.
Aidha amesema ugonjwa huo ni hatari ikilinganishwa na magonjwa mengine na kwamba kwa sasa ugonjwa huo umeripotiwa kushamiri katika nchi ya Kongo Mashariki inayopakana kwa karibu sana na mkoa wa Kigoma.
Magari mawili yagongana njia panda Dodoma
Taarifa zilizotufikia hivi punde zinaeleza kuwa, kuna ajali imetokea
asubuhi hii ya Jumanne, Septemba 11, 2018 ikihusisha gari la serikali
(STK) aina ya V8 na gari binafsi kugongana eneo la Nanenane jijini
Dodoma.
Inasemekana V8 ilikuwa ikilipita gari jingine njiapanda ya kwenda Chuo Kikuu cha Dodoma (UDOM) na gari ndogo iliyokuwa mbele ikaingia ghafla kuelekea UDOM ndipo ajali ilipotokea.
Inaelezwa kuwa gari hilo ni la kiongozi wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) lakini baada ya kuzungumza na RPC wa Dodoma, Girres Muroto amesema hajapata taarifa za tukio hilo bado.
Endelea kufuatilia taarifa zaidi kupitia mtandao wetu.
Inasemekana V8 ilikuwa ikilipita gari jingine njiapanda ya kwenda Chuo Kikuu cha Dodoma (UDOM) na gari ndogo iliyokuwa mbele ikaingia ghafla kuelekea UDOM ndipo ajali ilipotokea.
Inaelezwa kuwa gari hilo ni la kiongozi wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) lakini baada ya kuzungumza na RPC wa Dodoma, Girres Muroto amesema hajapata taarifa za tukio hilo bado.
Endelea kufuatilia taarifa zaidi kupitia mtandao wetu.
BSS yarudi upya, Madam Rita asema maneno mazito
Shindalo la kusaka vipaji la BSS limekuwa likifuatiliwa kwa ukaribu sana huku likiwa tayari limefanikiwa kuwatoa mastaa kibao ambao hawakuwa wakifahamika kama Kala Jeremiah, Baby Madaha, Peter Msechu na wengine. Shindano hilo linatarajiwa kuanza kutimua vumbi upya kuanzia Septemba 22, 2018 katika mkoa wa Mwanza, Madam Rita aahidi makubwa katika msimu huu wa tisa na kufunguka mazito.
Mwili wa aliyekuwa Katibu Mkuu Umoja wa Mataifa Kofi Annan umewasili Ghana kwa ajili ya maziko
Mwili wa aliyewahi kuwa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Kofi Annan,
ambaye alifariki mwezi uliopita, umewasili katika nchi aliyozaliwa,
Ghana.
Mwili wake uliwasili katika Uwanja wa Ndege wa Kotoka International Airport mjini Accra, ukisindikizwa na familia yake na maafisa wengine wa Umoja wa Mataifa
Kulikuwa na hali ya maombolezowakati mwili wake ukiwasili uwanjani hapo na kupokelewa na Rais wa Ghana Akufo Addo na viongozi wa kimila na kwa heshima ya kijeshi.
Mwili wake umehifadhiwa katika Ukumbi wa Kimataifa wa mikutano wa Ghana, wakati ukisubiri kuzikwa.
Kofi Annan alikuwa ni Katibu mkuu wa kwanza wa Umoja wa Mataifa, kutoka katika eneo la kusini mwa jangwa la Sahara na kuleta mafanikio sio tu katika bara la Afrika, lakini pia dunia nzima.
Chanzo BBC
Mwili wake uliwasili katika Uwanja wa Ndege wa Kotoka International Airport mjini Accra, ukisindikizwa na familia yake na maafisa wengine wa Umoja wa Mataifa
Kulikuwa na hali ya maombolezowakati mwili wake ukiwasili uwanjani hapo na kupokelewa na Rais wa Ghana Akufo Addo na viongozi wa kimila na kwa heshima ya kijeshi.
Mwili wake umehifadhiwa katika Ukumbi wa Kimataifa wa mikutano wa Ghana, wakati ukisubiri kuzikwa.
Kofi Annan alikuwa ni Katibu mkuu wa kwanza wa Umoja wa Mataifa, kutoka katika eneo la kusini mwa jangwa la Sahara na kuleta mafanikio sio tu katika bara la Afrika, lakini pia dunia nzima.
Chanzo BBC
Jumatatu, 10 Septemba 2018
Hukumu ya kifo dhidi ya watu 75 Misri haikuzingatia haki:Bachelet
Hatua
ya mahakama moja nchini Misri ya kuthibitisha hukumu ya kifo kwa watu
75, haikufuata utaratibu unaostahili katika kusikiliza kesi na endapo
hukumu hiyo itatekelezwa itakuwa ni ukiukwaji mkubwa wa haki.
Ameongeza kuwa suala linguine linalokiuka haki ni hatua ya hatua ya Misri ya kuwahukumu watu wengi kwa mkupuo na sheria mpya iliyopitishwa ambayo inawapa kinga maafisa wa vyombo vya dola dhidi ya kushtakiwa kutokana na makosa ambayo huenda wameyatenda.
Hukumu hiyo ya kifo ilitangazwa vifo wakati wa hukumu ya pamoja iliyotolewa Julai mwaka huu ambapo watu 739 walihukumiwa kwa makossa mbalimbali kutokana na maandamano ya Agosti mwaka wa 2013 yaliyoongozwa na wafuasi wa kundi la Muslim Brotherhood ambayo yalizimwa na jmabavu ya jeshi la polisi..
Bi. Bachelet amesema, “ jinsi kesi ilivyoendeshwa katika mahakama ya jinai mjini Cairo, imekosolewa vikali…na ni sahihi kufnya hivyo, watu 739 wameshtakiwa kwa mkupuo na hawakukubaliwa hata mmoja kuwakilishwa na mawakili mahakamani na wala hawakupewa fursa ya kujitetea.”
Ameongeza kuwa, “washukiwa hawakupewa haki ya kutoa ushahidi wao na pia upande wa mashtaka haukutoa ushahidi wa kutosha kuweza kuthibitisha kweli wana hatia .Hivyo hukumu ya kifo kwa watu 75 iliyohakikishwa jana, endapo itatekelezwa itakuwa ni ukiukwaji mkubwa wa haki na sharia ambao haitowezekana kuugeuza.”
Bi Bachelet amesema ni matumaini yake kuwa mahakama ya rufaa ya Misri itatengua hukumu hiyo na kuhakikisha kuwa viwango vya kimataifa vya sheria vinafuatwa na pia vinaheshimiwa.
Dominic Chavez/World Bank
Kamatakamata ya jeshi dhidi ya maandamano ya kundi la Muslim Brotherhood katika maeneo ya Rabaa al-Adawiya, uwanja wa Rabaa al-Adawiya na katka jukwa la Nahda mjini Cairo tarehe 14 Agosti 2013, yanadaiwa kusababisha vifo vya watu 900 na wengi ni raia ambao hawakuwa na silaha. Mauaji yanadaiwa kufanywa na vikosi vya serikali ya Misri. Baadae serikali ilidai kuwa waandamanji wengi walikuwa wamebeba silaha na kuwa polisi kadhaa waliuawa.
Wakati huohuo Julai mwaka huu, bunge la Misri lilipitisha sheria inayowapa kinga askari dhidi ya makossa yaliyotokea kati ya Julai 3 2013, hadi siku ambayo jeshi lilipindua serikali ya rais Morsi na pia Januari 10 mwaka wa 2016.
Sheria hiyo inampa uwezo rais kuwateuwa askari kadhaa kuwa askari wa kikosi cha akiba na kuwapa kinga na vile vile kumpa kinga ya kidiplomasia waziri yeyote akiwa ofisini au akiwa ziarani nje ya nchi.
Watoto laki tano kufa kwa njaa mwaka huu: Save the Children
Shirika la kimataifa linalohusika na
watoto la Save the Children, linakadiria kwamba zaidi ya watoto laki
tano wa kike na wa kiume wanatarajiwa kufa kwa njaa mwaka huu katika
nchi zilizokumbwa na mizozo na hivyo huduma za kibinadamu kushindwa
kufikishwa katika maeneo hayo.
Shirika la Save the Chlidren
limesema kuwa kwa mjibu wa takwimu za umoja wa mataifa ni kwamba mwakaja
pekee kuna matukio zaidi ya 1000 yaliyosababisha kuzuiwa kwa misaada ya
kibidamu kuwafikia raia waliokuwa katika maeneo yenye machafuko idadi
ambayo imekuwa na ongezeko mara mbili tangu mwaka 2012Hata hivyo ongezeko ni kubwa kutokana na mapigano katika nchi za Sudan Kusini,Yemen,Mali na Syria.
Mkurugenzi mkuu wa shirika la Save the Children Kevin Watkins,anasema kuwa kwa sasa imekuwa ni jambo la kawaida njaa kutumika kama silaha ya kivita.
Hata hivyo jambo jingine lililotajwa na shirika hilo,ni pande zinazopigana,kuzuia misaada ya kibinadamu kwa makusudi hali inayosababisha hali ngumu kwa raia waliokwama maeneo ya mapigano.
Kwa mjibu wa takwimu za umoja wa mataifa, mwaka jana pekee kulikuwa na matukio 1,460 ya mashirika ya misaada kukataliwa kuwafikia watu wenye mahitaji ya kibiandamu katika maeneo ya mapigano.
Kifo cha Mohammed Kirumira kimezusha masuali kuhusu ongezeko la vifo vya maafisa wa usalama Uganda
Rais wa Uganda Yoweri Museveni Jana
usiku alihutubia taifa ambapo alizungumzia masuala kadhaa ambayo
yameshuhudiwa nchini humo siku za hivi karibuni.
Hotuba ya rais
iliangazia sana changamoto za usalama zinazoikumba nchi kwa sasa. Lakini
pia alizungumzia masuala ya kawi, elimu, kilimo na miundo msingi.Museveni alitoa hotuba yake kwa taifa saa kadhaa baada ya afisa maarufu wa cheo cha juu Muhammad Kirumira, kuuawa kwa kupigwa risasi karibu na nyuambani kwake kwenye vitongoji vya mji mkuu Kampala Jumamosi usiku.
Kirumira ambaye ni afisa aliyekuwa anakumbwa na utata aliuawa hatua chache kutoka nyumbani kwake huko Bulenga.
Mwandishi wa BBC aliye mjini Kampala anasema Museveni alizungumzia mauaji ya hivi punde ya Bw Kirumira, aliyekuwa mbunge Ibrahim Abiriga na aliyekuwa msemaji wa polisi Felix kaweesi.
Alisema njia bora za kupambana na uhalifu zinahitaji kuanza kutumiwa kwa mfano kuwekwa alama za vidole kwenye bunduki zote.
"Kama bunduki zote zingekuwa na alama, mara unapopigwa risasi ikiondolewa na kupelekwa kwenye mashine, inaweza kutambuliwa risasi imetoka kwa bunduki namba fulani. Kama magari na pikipiki zingekuwa na namba za elektroniki sasa hivi tungekuwa tungemjua muuaji," alisema Museveni
Mfululizo wa mauaji Uganda yatia wasiwasi
Kirumira ni kati ya watu kadhaa wakiwemo meja Mohammed Kigundu na Felix Kaawesi waliouawa katika hali kama hiyo katika kipindi cha miaka 2 iliyopita,Machi mwaka 2017, Felix Kaweesi, msemaji wa jeshi la polisi nchini Uganda aliuawa kwa kupigwa risasi alipokuwa akiendesha gari kwenda kwa nyumbani kwake. Wauaji wake bado hawajapatikana.
Mwezi Juni mbunge Ibrahim Abiriga aliuwa pamoja na mlizi wake karibu na nyumbani kwake nje ya mji wa kampala, hakuna mtu aliyekamatwa kufuatia mauaji hayo.
Kirumira alisema alikuwa akiishi kwa hofu kwa sababu ya vitisho vya kuuliwa alivyokuwa akipata, lakini kwamba hilo halikumzuia kusema ukweli.
'Tunawafichua waovu ili tuliokoea taifa. Ukizungumza unakufa, ukinyamaza unakufa basi ni bora uzungumze na ufe wakati ujumbe umewafikia watu.
"Basi ujumbe wangu kwa wauaji wanaoshika bunduki ni kwamba, mukiniua ni bure tu. Kwa sababu kama mjumbe nimetekeleza lengo langu la kuwasiliana na jamii' Kirumira aliwaambia waandishi habari Uganda kwa wakati mmoja
Watu nchini uganda walitoa maoni kuhusu mauaji hayo. Wakitumia mitandao ya kijamii wakihoji ni kwa nini kuna uhalifu mwingi unaohusu bunduki nchini humo.
Wiki tatu zilizopita, Uganda ilikumbwa na maandamano kufuatia kukamatwa na kuteswa wabunge Robert Kyagulanyi na Francis Zaake.
Vikosi vya Uganda vilijibu kwa kuwapiga risasi watu sita na kuwajeruhi wengine kadhaa.
Habari za kuuawa kwa Kirumira ziliwashutusha wengi ndani na hata nje ya Uganda.
Muda mfupi kabla ya kuhotubia taifa, Rais Museveni pia alitoa rambi rambi zake katika ujumbe huuu kwenye twitter kufuatia mauaji hayo ya Kirumira
Kadhalika kuna wanaojadili kuusu kuendelea kushuhudiwa kwa mauaji ya maafisa wa polsi na wa jeshi katika kesi ambazo bado mpaka sasa hazijatatuliwa.
Rais wa Sudan avunja baraza la Mawaziri
Rais Omar al Bashir
Amemteua Motazz Moussa kuwa Waziri mkuuu mpya wa nchi hiyo, ambaye anashika nafasi ya Bakri Hassan Saleh aliyechaguliwa kuongoza nafasi hiyo mwaka 2017.
Kabla ya kuteuliwa katika nafasi yake hiyo, Motazz Moussa alikuwa ni Waziri anayeshughulikia masuala ya umeme na umwagiliaji.
Uamuzi huo umekuja mara tu baada ya Rais Omar al Bashir kuitisha kikao cha dharura cha maafisa wa chama tawala katika makaazi yake katika kipindi ambacho wasiwasi wa hali ya kuuchumi imekuwa ikiongezeka kutokana na kupanda bei za vitu na vingine kutopatikana.
Hakuna nafasi nyingine za mawaziri zilizotangazwa , lakini idadi ya mawaziri katika serikali mpya itapungua mpaka 21 kutoka 31, hatua ambayo inalenga kupunguza matumizi.
Awali Naibu Mwenyekiti wa chama tawala nchini humo cha National Congress Faisal Hassan amewaambia waandishi wa habari kwamba Mawaziri wa Mambo ya Nje, ulinzi na masuala ya Rais watabaki katika nafasi zao, litakapoundwa baraza jipya la mawaziri.
Kumekuwa na upinzani tangu Januari mwaka huu, baada ya bei ya mkate kupanda maradufu, baada ya serikali kuondosha ruzuku ya chakula.
Kushuka kwa Sarafu ya Sudan kumesababisha ugumu katika kununua ngano nje ya nchi na bidhaa nyingine.
Wachambuzi wanasema kuwa uchumi wa Sudan umekuwa na matatiuzo toka Sudan ya kusini ilipojitenga na nchi hiyo mwaka 2011.
LIVE: Rais Magufuli kuhitimisha ziara yake Kanda ya Ziwa
LIVE: Rais Magufuli leo anahitimisha ziara yake Kanda ya Ziwa kwa
kufungua miradi mbalimbali. Leo yuko katika daraja la Mto Sibitu,
mpakani mwa Mkoa wa Simiyu na Singida. Matangazo haya pia yako MBASHARA #AZAMTWO
Spika wa Bunge Job Ndugai Awapiga Marufuku Wabunge Kuingia Bungeni na Kucha Bandia au Kope Bandia
Spika wa Bunge, Job Ndugai, leo septemba 10, 2018 amepiga marufuku wabunge waliobandika kucha na kope bandia kuingia katika Ukumbi wa Bunge.
Spika Ndugai amesema hayo wakati wa kipindi cha maswali na majibu, baada ya Mbunge wa Viti Maalumu, Fatma Tawfiq kuhoji
idadi ya wanawake walioathirika macho kutokana na matumizi ya kope
bandia kwani baadhi ya wanawake wameathirika na vipodozi vikiwamo kucha
za na kope za kubandika.
Swali hilo lilijibiwa na Naibu Waziri wa Afya Mhe. Faustine Ndugulile ambapo amesema Takribani
wagonjwa 700 kwa mwaka hupokelewa katika hospitali ya Taifa Muhimbili
(MHN), wakiwa na matatizo ya ngozi yanayaotokana na kumeza vidonge
vinavyobadili rangi ya mwili mzima, pamoja na vipodozi vyenye kemikali.
Dk.
Ndungulile amesema kwa sasa wizara kupitia Mamlaka Chakula, Dawa na
Vipodozi (TFDA) haina utaratibu wa kudhibiti kope wala kucha za
kubandika kwa sababu hakuna sheria inayoipa ya kudhibiti bidhaa hizo.
Pamoja na mambo mengine, Dk. Ndungulile alisema anaomba kuwapa somo wabunge akisema; “tunapozichubua ngozi zetu tunaondoa kinga, mtu anayejichubua ngozi anaingia katika hatari ya kupata saratani, magonjwa ya ngozi, rangi ya asili ni nzuri ilitengenezwa kwa ajili ya kujikinga na magonjwa mbalimbali hivyo nawaomba msiharibu ngozi zenu kwa vipodozi.”
Pamoja na mambo mengine, Dk. Ndungulile alisema anaomba kuwapa somo wabunge akisema; “tunapozichubua ngozi zetu tunaondoa kinga, mtu anayejichubua ngozi anaingia katika hatari ya kupata saratani, magonjwa ya ngozi, rangi ya asili ni nzuri ilitengenezwa kwa ajili ya kujikinga na magonjwa mbalimbali hivyo nawaomba msiharibu ngozi zenu kwa vipodozi.”
Baada
ya Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto,
Dk. Faustine Ndungulile kujibu swali hilo, Spika Ndugai alisema;
“Kutokana na elimu hiyo, na mimi leo napiga marufuku kwa wabunge wote
kuingia bungeni wakiwa na kucha na kope bandia, lakini kwa wale
wanaojichubua naendelea kuchukua maoni,” amesema Spika Ndugai huku
baadhi ya wabunge wanaume wakipaza sauti kwa kusema “na nywele bandia
huku Dk. Ndunglile akimshukuru kwa kuungana na serikali kupiga marufuku
matumizi ya kope na kucha bandia.”
LEO NDIYO SIKU YA MWISHO KUCHUKUA FOMU, SIMBA WATOA TAMKO
Uongozi wa Simba umesema leo ndiyo siku ya mwisho kwa wanachama wa timu hiyo kuchukua fomu kwa ajili uya kugombea nafasi mbalimbali za uongozi.
Kwa mujibu wa Ofisa Habari wa klabu, Haji Manara, amewasihi wanachama wa klbu kujitokeza leo Jumatatu ili kuhakikisha wanapata haki yao kikatiba.
Aidha Manara amewataka wanachama kuitumia Jumatatu ya leo vizuri kwa ajili ya kuchua fomu hizo maana hakuna uwezekano wa siku kuongezwa.
Simba inatoa msisitizo huo ili kuja kupata rasmi viongozi watakaoiwezesha kuja kuanza kazi ikiwa katika muundo mpya wa kimabadiliko.
Klabu hiyo itafanya uchaguzi wake mkuu Novemba 3 2018 kwa ajili ya kuwapata viongozi wake wapya baada ya utawala uliopo madarakanani kumaliza muda wake.
Serikali Yagoma Kuwalipa Watumishi Waliofukuzwa Kazini Kwa Kuwa na Vyeti FEKI
Serikali imesema haitawalipa watumishi waliofukuzwa kazi kwa kuwa na vyeti feki kutokana na udanganyifu huo.
Akijibu
swali la nyongeza la Mbunge wa Viti Maalumu, Aida Khenani bungeni
jijini Dodoma leo, Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Utumishi na Utawala
Bora, George Mkuchika amesema serikali haijapanga kumlipa mtumishi
yeyote ambaye mkataba wake ni feki.
Akiuliza
swali hilo, Aida amesema kabla ya kupunguzwa kwa watumishi hao
waliodaiwa kuwa na vyeti feki, serikali ilikuwa na vyeti feki na hadi
sasa kuna upungufu wa watumishi wa kiasi gani.
“Serikali
ya Tanzania inathamini zaid vyeti kuliko taaluma, kuna wengine walikuwa
wamebakisha mwaka mmoja tu ili wastaafu, je, serikali ina mpango gani
wa kuwalipa watumishi hao,” amesema.
Mkuchika
akijibu hilo amesema; “Mwajiri alikuajiri akijua vyeti ulivyompelekea
ni sahihi, kitendo cha kumdanganya kinafuta mkataba wenu na serikali
haijapanga kuwalipa watumishi wa aina hiyo,”
Bondia wa kitanzania kampiga KO muingereza nyumbani kwao
Ushindi wa Hassan Mwakinyo unakuja dhidi ya Sam Eggington wiki mbili tu baada ya kupata taarifa na kuanza maandalizi, Hassan ameshinda kwa Knock Out dhidi ya Sam kwa kumpiga round ya 2 katika pambano la round 10.
Pambano hilo la round 10 za uzito wa kati lilifanyika katika mji wa Birmigham nchini England, licha ya kuwa na sapoti kubwa kwa Sam Eggington kutokana na kuwa nyumbani hakuweza kupata ushindi dhidi ya Hassan.
Jumapili, 9 Septemba 2018
STARS YAWASILI JIJINI DAR
Timu ya Taifa ya Tanzania “Taifa Stars” imerudi leo kutoka Uganda ambapo ilicheza mchezo wa kutafuta tiketi ya kucheza fainali za Africa dhidi ya Uganda.
Katika mchezo uliochezwa jana Jumamosi Septemba 8,2018 nchini Uganda, Stars ilikwenda ya mabao 0-0.
Katika kundi L mpaka sasa Uganda inaongoza ikiwa na alama 4 wakati Stars ikiwa na mbili huko Lesotho ina 1 na Cape Verde wakiwa na 0.
Wakati huo Lesotho wanashuka kibaruani leo kucheza na Cape Verde ambayo haina alama yoyote.
YANGA YAIBUKA NA USHINDI KIDUCHU TAIFA DHIDI YA AFRICAN LYON
Kikosi cha Yanga kimeibuka na ushindi wa bao 1-0 dhidi ya African Lyon katika mchezo wa kirafiki uliopigwa Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.
Bao pekee la Yanga limewekwa kimiani na Yusuph Mhilu mnamo dakika za mwisho za mchezo.
Yanga wametumia mechi hiyo kama maandalizi ya kujiandaa na mechi zijazo za Ligi Kuu Bara.
Katika kipute hicho, Yanga imewakosa nyota wake baadhi ikiwemo Kelvin Yondani, Thaban Kamusoko, Juma Mahadhi walio majeruhi na wengine waliokuwa Uganda kwa majukumu ya timu ya taifa.
BREAKING: Msafara wa Rais Magufuli wapata ajali Meatu
GARI lililokuwa limebeba waandishi wa habari wa Mkoa wa Simiyu limepata ajali kwenye msafara wa Rais John Magufuli mjini Mhanuzi wilayani Meatu ambapo liligongwa na magari mengine kwa nyuma.
Waandishi wa habari watatu, Adan Mhando wa Channel Ten, Faustine Fabian wa Mwananchi, Rehema Evansi wa Azam TV, na Mpiga picha wa ITV, wamepata majeraha madogomadogo na wamekimbizwa hospitali ya wilaya Meatu.
Lulu amaliza kimya chake cha siku 323 leo
Muigizaji wa Bongo Movie Elizabeth Michael maarufu kwa jina la LuLu baada ya kimya kirefu katika mitandao ya kijamii, leo Jumapili ya September 9 2018 amevunja kimya hicho kwa kupost post ya kwanza katika ukurasa wake wa instagram baada ya kukaa kimya kwa siku 323.
Lulu leo amemaliza kimya chake cha siku 323 bila kupost kwa kupost picha ya mpenzi wake DJ Majjizo ambaye amekuwa nae kwenye mahusiano kwa muda mrefu sasa, Lulu amepost picha ya Majjizo katika ukurasa wake wa instagram na kuandika maneno ya kumtakia heri ya kumbukumbu ya siku ya kuzaliwa.
Mara ya mwisho Lulu kupost picha kupitia ukurasa wake wa instagram ilikuwa October 22 2017 ikiwa ni siku 23 kabla ya kuhukumiwa kifungo cha miaka 2 jela kwa kukutwa na hatia ya kumuua bila kukusudia muigizaji mwenzake Steven Kanumba April 7 2012 ila May 14 2018 Lulu alibadilishiwa kifungo na kuanza kutumikia kifungo cha nje.
Fahamu dalili na tiba ugonjwa wa presha ya macho
MTU anaweza kujiuliza presha ya macho au kitaalamu Glaucoma ni nini? Hili ni ongezeko la presha ya macho, kimsingi macho huwa yana presha ya 10mmhg mpaka 21mmhg lakini inapozidi hapo mtu hutambuliwa kuwa ni mgonjwa wa presha ya macho.
Mara nyingi ugonjwa huu hurithiwa na hauonyeshi dalili zozote mpaka baadaye sana mtu anapokua mtu mzima.
Ugonjwa huu huathiri mishipa ya fahamu inayohusika na kuona kitaalamu huitwa optic nerve na mgonjwa asipokua makini na matibabu yake basi huweza kupata upofu wa moja kwa moja na asione tena maishani mwake.
CHANZO CHA UGONJWA
Kitaalamu upande wa mbele ya jicho kuna majimaji ambayo kitaalamu tunaita aquous homour ambayo kazi yake ni kuleta virutubisho kwenye sehemu za jicho iitwayo iris, lenzi na cornea.
Pia majimaji hayo huondoa mabaki ya matumizi ya virutubisho hivyo vilevile hutunza shepu ya jicho. Sasa majimaji haya yanapozidi ndio presha ya macho inapanda.
Kwa kawaida hali hii hurithiwa kutoka kwenye kizazi kimoja mpaka kingine na sababu zingine zinazoweza kuongeza presha hii ni magonjwa ya macho.
Kuumia jicho kwa kupigwa na kitu au kumwagikiwa kemikali au baada ya upasuaji wa macho wa kutibu tatizo lingine la macho ni moja ya chanzo kingine cha tatizo la jicho.
WENYE HATARI YA KUUGUA PRESHA YA MACHO
Unaweza kujiuliza ni watu gani wako kwenye hatari ya kuugua ugonjwa huu? Jibu ni kwamba ni wale wote ambao ukoo wao una kawaida ya kuwa na wagonjwa wa maradhi haya ya presha ya macho.
Wengine ni watu wanaougua ugonjwa wa kisukari, watu wenye umri zaidi ya miaka 40, watu walioumia macho, watu wanaotumia dawa fulanifulani kama predinisolone ambazo huweza kuathiri macho, watu waliopata ajali na kuumia macho na watu wasioona vizuri wanaweza kupatwa na presha ya macho.
DALILI ZA UGONJWA HUU
Zipo dalili nyingi za mtu mwenye presha ya macho na mara nyingi ugonjwa huu dalili zake haziji moja kwa moja kwani huja kwa kujificha sana bila muhusika kujua.
Mgonjwa anakuja kugunduliwa kwenye hatua mbaya kabisa ambayo ni ya hatari kwake. Moja ya dalili ya maradhi haya ni mtu kushindwa kuona mbali na pembeni, mgonjwa kuwa na macho mekundu na kusikia maumivu makali ya macho.
Dalili nyingine ni mgonjwa kuhisi kichefuchefu na kutapika, kuona kama mawingumawingu au ukungu.
VIPIMO VYA PRESHA YA MACHO
Ili kugundua kwamba una tatizo la presha ya macho unatakiwa uonapo dalili huzo kwenda haraka hospitali kumuona daktari ambaye atatumia vipimo maalumu kupima presha yako ya macho.
Baada ya hapo atapima kuangalia kama mishipa ya fahamu inayohusika na kuona imeathirika kiasi gani. Mara nyingi kipimo cha tenometry ndicho hutumika kupima presha ya macho.
TIBA YA MARADHI HAYA
Hakuna dawa ya kutibu ugonjwa huu kabisa lakini kuna dawa za kutumia kwa muda wote wa maisha yako ambazo zitakua zinapunguza presha ya macho yako.
Dawa hizo ni zile za matoni kama vile timolol lakini pia wakati mwingine kuna aina za upasuaji hufanyika kuweka matundu kwenye iris ili kuachia majimaji yanayoleta tatizo kupita na kupunguza presha ya macho.
Mtu anaweza kujiuliza je, unaweza kuzuia ugonjwa huu, jibu ni kwamba huwezi kuzuia maradhi haya lakini unaweza kuzuia upofu kwa kuanza matibabu mapema na kuyafuatilia matibabu kwa umakini kama utakavyoelekezwa na daktari wa macho.
Malengo ya SDGs sasa pia ni kwa watoto wa shule za Chekechea. :UN
Umoja wa Mataifa kwa ushirikiano na kampuni ya Mattel, Inc.,umezindua aina mpya ya mawasiliano ya kufikisha ujumbe wa malengo ya maendeleo endelevu , SDGs kwa watoto wa shule za Chekechea.
Aina hiyo mpya ni kupitia vipindi vya mlululizo vya vikaragosi maarufu vya Thomas na rafiki zake (Thomas and Friends.)
Kupitia taarifa iliyotolewa katika uzinduzi wa ushirika huo uliofanyika leo kwenye Makao Makuu ya Umoja wa Mataifa mjini New York Marekani, imesema malengo saba kati ya 17 ya maendeleo endeleo yatajumuishwa vipindi 8 kati ya mlululizo wa vipindi 26 vipya vya vikaragosi hivyo vya Thomas & Friends, ambavyo vinaanza kurushwa leo rasmi nchini Marekani kupitia kipindi chaneli ya Nick Jr, wakati kwingineko duniani vitaanza kurushwa hewani miezi kadhaa ijayo.
Malengo yatakayohusishwa katika vipindi hivyo ni namba 4 lihusulo elimu bora; namba 5 la usawa wa kijinsia; namba 11miji na jamii endelevu , namba 12 la uzalishaji na matumizi endelevu na namba 15 kuhusu maisha ya nchi kavu katika sayari hii.
Katika uzinduzi huo mkurugenzi wa kitengo cha uhusiano wa nje kwenye idara ya habari kwa umma ya Umoja wa Mataifa (DPI), Maher Nasser, amesema, “katika juhudi za kutaka malengo ya SDGs kujulikana na kuhamasisha watu wa rika zote, Thomas & Friends ndio chaguo kwa watoto pamoja na wazazi wao na vilvile walezi wao.”
Ameongeza kuwa, “Thomas & Friends SDGs imekuwa chombo muafaka kwa kuwafundishia watoto umuhimu wa kushiriki katika juhudi za kimataifa za kukomesha umaskini, kutoa fursasawa kwa mtoto wa kike na wa kiume na bila shaka tukifanya hivyo huku tunailinda sayari yetu.”
Ubia huu mpya baina ya Umoja wa Mataifa na Thomas & Friends utatayarisha video funzi za kuelimisha kuhusu maisha ya utotoni pamoja na vidokezo kwa wazazi na mawasiliano mengine kupitia wavuti wao mpya, AllAboutForGlobalGoals.com ambao pia umezinduliwa leo, katika lugha ya kiingereza na lugha zingine zitafuata hapo baadaye.
Rais wa kampuni ya Mattel, Richard Nixon, amesema kuwa Thomas anafaa sana wakati huu ambapo watoto wanaletewa kwa mara ya kwanza mambo muhimu katika maisha yao kama yalivyo katika malengo ya maendeleo endelevu. Akiongeza kuwa ndio maana Umoja wa Mataifa upo na ndio limekuwa somo muhimu kwa Thomas kwa kipindi cha miaka 70.
Kupitia taarifa iliyotolewa katika uzinduzi wa ushirika huo uliofanyika leo kwenye Makao Makuu ya Umoja wa Mataifa mjini New York Marekani, imesema malengo saba kati ya 17 ya maendeleo endeleo yatajumuishwa vipindi 8 kati ya mlululizo wa vipindi 26 vipya vya vikaragosi hivyo vya Thomas & Friends, ambavyo vinaanza kurushwa leo rasmi nchini Marekani kupitia kipindi chaneli ya Nick Jr, wakati kwingineko duniani vitaanza kurushwa hewani miezi kadhaa ijayo.
Malengo yatakayohusishwa katika vipindi hivyo ni namba 4 lihusulo elimu bora; namba 5 la usawa wa kijinsia; namba 11miji na jamii endelevu , namba 12 la uzalishaji na matumizi endelevu na namba 15 kuhusu maisha ya nchi kavu katika sayari hii.
Katika uzinduzi huo mkurugenzi wa kitengo cha uhusiano wa nje kwenye idara ya habari kwa umma ya Umoja wa Mataifa (DPI), Maher Nasser, amesema, “katika juhudi za kutaka malengo ya SDGs kujulikana na kuhamasisha watu wa rika zote, Thomas & Friends ndio chaguo kwa watoto pamoja na wazazi wao na vilvile walezi wao.”
Ameongeza kuwa, “Thomas & Friends SDGs imekuwa chombo muafaka kwa kuwafundishia watoto umuhimu wa kushiriki katika juhudi za kimataifa za kukomesha umaskini, kutoa fursasawa kwa mtoto wa kike na wa kiume na bila shaka tukifanya hivyo huku tunailinda sayari yetu.”
Ubia huu mpya baina ya Umoja wa Mataifa na Thomas & Friends utatayarisha video funzi za kuelimisha kuhusu maisha ya utotoni pamoja na vidokezo kwa wazazi na mawasiliano mengine kupitia wavuti wao mpya, AllAboutForGlobalGoals.com ambao pia umezinduliwa leo, katika lugha ya kiingereza na lugha zingine zitafuata hapo baadaye.
Rais wa kampuni ya Mattel, Richard Nixon, amesema kuwa Thomas anafaa sana wakati huu ambapo watoto wanaletewa kwa mara ya kwanza mambo muhimu katika maisha yao kama yalivyo katika malengo ya maendeleo endelevu. Akiongeza kuwa ndio maana Umoja wa Mataifa upo na ndio limekuwa somo muhimu kwa Thomas kwa kipindi cha miaka 70.
8 Septemba 2018 ni siku ya kimataifa yakutojua kusoma na kuandika
jumuiya ya kimataifa imeombwa kuchukua hatua za pamoja kuendeleza elimu na ujuzi katika vita dhidi ya kutojua kusoma na kuandika.
Wito
huo umetolewa na shirika la Umoja wa Mataifa la elimu, sayansi na
utamaduni UNESCO, wakati wa kuadhimisha siku ya kimataifa ya kutojua
kuandika wala kusoma ambayo inasherehekewa kila mwaka tarehe 8
Septemba duaniani kote.
Wito huu unakuja kukiwa na taarifa za watu milioni 750 duniani kote wasiojua kusoma wala kuandika na kati ya hao wote theluthi mbili ni wanawake ambao bado ni vijana.
Kauli mbiu ya mwaka huu ni kuendeleza kujua kusoma na kuandika pamoja na ujuzi. Umoja wa Mataifa unasema siku hii ni fursa nzuri kwa wadau kumulika mabadiliko katika viwango vya kusoma na kuandika duniani na pia kutafakari changamoto zilizosalia kuhusu suala hili.
Umoja wa Mataifa unasema kusoma na kuandika ni kipengee muhimu cha malengo ya Umoja wa Mataifa ya maendeleo endelevu na pia ajenda ya Umoja wa Mataifa ya 2030.
UNESCO inasema kuna watu milioni 192 duniani hawana ajira na huhitaji elimu na ujuzi kuweza kujiendeleza kimaisha.
Nalo lengo namba 4 lina shabaha ya kuhakikisha kuwa vijana wengi wanapata elimu na watu wazima ambao hawana elimu kuwawezesha kuipata.
Wito huu unakuja kukiwa na taarifa za watu milioni 750 duniani kote wasiojua kusoma wala kuandika na kati ya hao wote theluthi mbili ni wanawake ambao bado ni vijana.
Kauli mbiu ya mwaka huu ni kuendeleza kujua kusoma na kuandika pamoja na ujuzi. Umoja wa Mataifa unasema siku hii ni fursa nzuri kwa wadau kumulika mabadiliko katika viwango vya kusoma na kuandika duniani na pia kutafakari changamoto zilizosalia kuhusu suala hili.
Umoja wa Mataifa unasema kusoma na kuandika ni kipengee muhimu cha malengo ya Umoja wa Mataifa ya maendeleo endelevu na pia ajenda ya Umoja wa Mataifa ya 2030.
UNESCO inasema kuna watu milioni 192 duniani hawana ajira na huhitaji elimu na ujuzi kuweza kujiendeleza kimaisha.
Nalo lengo namba 4 lina shabaha ya kuhakikisha kuwa vijana wengi wanapata elimu na watu wazima ambao hawana elimu kuwawezesha kuipata.
Jisajili kwenye:
Machapisho (Atom)