Jumatatu, 10 Septemba 2018

Spika wa Bunge Job Ndugai Awapiga Marufuku Wabunge Kuingia Bungeni na Kucha Bandia au Kope Bandia

Spika wa Bunge, Job Ndugai, leo septemba 10, 2018  amepiga marufuku wabunge waliobandika kucha na kope bandia kuingia katika Ukumbi wa Bunge.

Spika Ndugai amesema hayo wakati wa kipindi cha maswali na majibu, baada ya Mbunge wa Viti Maalumu, Fatma Tawfiq kuhoji idadi ya wanawake walioathirika macho kutokana na matumizi ya kope bandia kwani baadhi ya wanawake wameathirika na vipodozi vikiwamo kucha za na kope za kubandika.
Swali hilo lilijibiwa na Naibu Waziri wa Afya Mhe. Faustine Ndugulile  ambapo amesema Takribani wagonjwa 700 kwa mwaka hupokelewa katika hospitali ya Taifa Muhimbili (MHN), wakiwa na matatizo ya ngozi yanayaotokana na kumeza vidonge vinavyobadili rangi ya mwili mzima, pamoja na vipodozi vyenye kemikali. 
 
Dk. Ndungulile amesema kwa sasa wizara kupitia Mamlaka Chakula, Dawa na Vipodozi (TFDA) haina utaratibu wa kudhibiti kope wala kucha za kubandika kwa sababu hakuna sheria inayoipa ya kudhibiti bidhaa hizo.


Pamoja na mambo mengine, Dk. Ndungulile alisema anaomba kuwapa somo wabunge akisema; “tunapozichubua ngozi zetu tunaondoa kinga, mtu anayejichubua ngozi anaingia katika hatari ya kupata saratani, magonjwa ya ngozi, rangi ya asili ni nzuri ilitengenezwa kwa ajili ya kujikinga na magonjwa mbalimbali hivyo nawaomba msiharibu ngozi zenu kwa vipodozi.”

Baada ya Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dk. Faustine Ndungulile kujibu swali hilo, Spika Ndugai alisema; “Kutokana na elimu hiyo, na mimi leo napiga marufuku kwa wabunge wote kuingia bungeni wakiwa na kucha na kope bandia, lakini kwa wale wanaojichubua naendelea kuchukua maoni,” amesema Spika Ndugai huku baadhi ya wabunge wanaume wakipaza sauti kwa kusema “na nywele bandia huku Dk. Ndunglile akimshukuru kwa kuungana na serikali kupiga marufuku matumizi ya kope na kucha bandia.”

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni