Wandamba ni kabila la Tanzania wanaoishi kiasili katika mkoa wa Morogoro, Wilaya ya Kilombero, hasa katika mji wa Ifakara pamoja na vijiji vya Mofu, Ruipa, Mbingu, Mngeta, Merera, Chita, mlimba ,Ngombo na Biro.
kulingana na historia na tafiti za kihistoria koo za kwanza za kindamba zliishi katika eneo la biro ambapo kulikuwa na kanisa na shule ,ikumbukwe kipindi hicho wilaya ya kilombero ilitambulika kuwa na wilaya ya ulanga,
kabila la wandamba kwa kawaida ni wakulima wazuri wa zao la mpunga ,pia ni wavuvi wazuri, sana ,siri mmojawapo ya mndamba kama amekutembelea nyumbani kwako ,mpikie wali ,kabila hili ni maarufu sana kwakupenda wali , na ndio maana hulima sana mpunga kuliko zao jengine ,
kama nilivyokwambia hapo awali hupenda sana samaki huweza kumla samaki bila kutoa miba ,miba hutoka yenyewe pembezoni mwa midomo,watani wa kabila hilo wakiwemo wangoni,wambunga na wengine hupenda kuwa watania kuwa kamwe huwezi kushindana na mndamba kumla samaki mwenye miba mingi kama perege na wengine atakushinda tu
,wandamba hupenda kuishi pembezoni mwa mito mikubwa katika bonde la kilombero , kama vile mto kilombero, mto mpanga,mto fulua na mingine mingi,ya morogoro .hiyo yoe kutokana na vyakula vyake anavyopenda kama mpunga hulimwa bondeni ,pia samaki hupatikana katika mabonde na mito,
kwa kawaida bonde la kilombero hufurika sana maji hasa katika miezi janauryimachi hadi aprili katika mvua za masika hivyo kukwamisha usafiri ,ila kwa wandamba wana usafiri wao maarufu ujulikanao kama mtumbwi, ni msaada mkubwa hasa kama mafuriko yameingia usiku mndamba huamisha familia yake kwa usafiri huo.
licha ya mtumbwi pia hata nyumba zao ni za kujikinga na mafuriko ,kwakua wanajua wanaishi katika maeneo bondeni ,kwakufuata ardhi yenye rutuba kwa ajili ya kilimo cha mpunga ,pia uvuvi wa samaki ,kutokana na hilo wandamba wananyumba za maeneo hayo maarufu kama lingo, lingo ni nyumba ndefu iliyojengwa kwa miti mirefu, kama nyumba ya ghorofa moja ,hivyo husaidia kuepuka mafuriko ambayo hukaa kwa wiki au kuendelea ,lingo hujengwa kwa miti imara hivyo ni viguma kuanguka.
kijana wa kindamba sharti ajue kuogelea kwasababu asilimia kubwa shughuli nyingi huzifanya katika mto ,kama vile kuvua samaki, kusafiri ,kuoga na kadhalika,
kwa upande wa ngoma wandamba wana ngoma nyingi ila ngoma kubwa zipo aina mbili na hupigwa katika matukio tofauti nazo ni lindenda na sangula
lindenda ni ngoma ya kindamba ngoma hii hupigwa katika misiba hasa wakati wa pombe ya marehemu arobaini na nakadhalika.
pia endapo marehemu ataacha wosia kuwa endapo atakufa ataomba apigiwe ngoma hiyo wakati wa mazishi yake ndugu hufanya hivyo .kwa kifupi lindenda ni ngoma ya kuomboleza msibani katika kabila la kindamba.
sangula ni ngoma ya kindamba ambayo hupigwa katika sherehe, sikukuuu mbalimbali haswa katika kipindi cha mavuno mwezi wa sita kuendelea hadi dicemba kwakua asilimia kubwa ya wandamba ni waumini wa makanisa ya kikristo hasa kanisa katoliki kama krismas, mwaka mpya kipaimara,ubatizo,ndoa ,sikukuu ya wakulima nk.
kama utahitaji ngoma hii pendwa basi nakusihi unapaswa kujiandaa kuaandaa pesa ya kuwalipa wachezaji wa ngoma hiyo pamoja wapigaji ngoma filimbi,manyanga ,kikosi cha ngoma ya sangula huwa 10 au zaidi . pia utapswa kuandaa chakula cha kutosha pia pombe za kienyeji kama vile pombe ya mpunga, pombe ya mahindi maarufu kama komoni ,ulanzi,
kwa upande wa mwingine wandamba hupendelea kuzungumza ni mahodari kuzungumza ukimpa nafasi ya kujieleza anajieleza,pia aslimia 90 sio washari wandamba hawapendi ugomvi ,ni wakarimu ,ila pindi anapoona ameonewa hufuata sheria, na endapo watakosa haki hushirikiana katika kutafuta haki,wapo tayari kuanzisha vurugu kubwa za kikabila ,matukio mengi katika wilaya hizo yanajieleza juu ya kabila hilo , na makabila ya wafugaji hata serikali.
kwa upande wa mwanamke wa kindamba hujifunza kazi mbalimbali, mapishi ,kulea watoto, na kilimo,
wanawake wa kindamba ni mahodari kwakutwanga pepeta, ,ambapo ni kitafunwa maarufu katika jamii hiyo ,pia ni wachapakazi hata katika kilimo cha mpunga .
pombe ya asili ya kindamba ni pombe ya mpunga ,pombe hiyo hutengenezwa kwa zao la mpunga ,pia pombe ya mahindi maarufu kama komoni,ulanzi mnazi nk
Lugha yao ni Kindamba (wenyewe wanatamka Chindamba), ambacho kinafanana sana na Kimbunga (69%) na Kipogoro (56%), lugha ya Wapogoro wanaoishi katika wilaya ya Ulanga. Hiyo inathibitisha kwamba asili yao ni moja.
Upande wa dini wengi wao ni wafuasi wa Yesu Kristo katika Kanisa Katoliki.
Mwaka 1987 walikadiriwa kuwa 79,000, mbali ya Wambunga waliokuwa 29,000.
Ni maarufu kwa kupenda kula wali na samaki hata mwaka mzima.
makala hii mwanahabari imeandikwa deus liganga mwenyeji wa kilombero ,pia ni mndamba
deusliganga@yahoo.com, 0659944423
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni