Kwa
sasa kuna baadhi ya watanzania ni washabiki wakubwa sana wa mziki wa
Taarabu. Na tunapozungumzia orodha ya miziki ya Tanzania na Afrika
mashariki kwa ujumla, hatuwezi kuacha kutaja mziki wa taarabu.
Licha ya kwamba kwa sasa mziki huu unaonekana kama unafifia hivi, kwa ujumla ni mziki wenye mashabiki wengi sana. Leo mtapata kujua historia ya chimbuko la muziki huu hapa Afrika mashariki. Wapo wanaodai kuwa mziki huu asili yake uarabuni na wapo wanaodai kuwa mziki huu umechipukia hapa hapa Afrika.
Kwa nini wnasem umechipukia kwa Waafrika?.Historia ipo hivi, kabla ya mwaka 1850 wakazi waliokuwa wakiishi katika pwani ya Afrika mashariki kuanzia Mto Juba nchini Somalia mpaka Msumbiji, walikuwa wakiimba mashairi yao yenye kusifu viongozi wao na familia zao. Tukimaanisha kuwa thamani ya mziki au kazi za mziki wenye radha ya Pwani ulikuwepo hata kabla ya miaka 1850.
Na kuna ushahidi wa kutosha juu ya uwepo wa mashairi ya Kiswahili hata kabla ya ujio wa waarabu. licha ya kwamba mashairi hayo ya waswahili yaliathiriwa sana na tamaduni za kiarabu lakini bado Lugha ya Kiswahili ilikuwepo na ilitumika katika mashairi. Mfao mzuri ni Fumo Lyongo na Utenzi wa Mwana Kupona.
Na kwa nini wanasema cumechipukia Uarabuni?.Historia ya chimbuko la muziki wa taarabu ipo kama ifuatavyo, wakati Zanzibar ikiwa chini ya sultan Said Sayyid kuanzia miaka ya 1840 kulikuwa na mabadiliko makubwa katika utamaduni wa waswahili. Na ifahamike kuwa masultani baada ya kazi walipenda sana kuimbiwa mashairi, na kulikuwa na taratibu za kuharika watu mbalimbali kuja kuburudisha masultani wa Zanzibar ndani na nje ya Zanzibar.
Ndipo miaka ya 1870 aliharikwa mwimbaji wa taarabu kutoka Misri ambaye alipata nafasi ya kuwaburudisha masultuni wa Zanzibar. Kijana huyo kutoka Misri ambaye jina lake halikufahamika, aliweza kukonga nyoyo za masultani wa zanzibar kwani aina ya mziki huo ulikuwa ni mzuri sana. Masultani walitokea kuupenda sana mziki huo uliokuwa ukiimbwa na kijana huyo kutoka Misri kwa namna ulivyokuwa ukiimbwa na namna ya watu wanavyocheza kwa polepole.
Huku kukisikia ala za mziki zilizokuwa zikitoa sauti nzuri na zenye kukonga nyoyo za wasikilizaji. Na maraa ya muhaliko kuisha kijana huyo alirudi kwao Misri hukuakiwa amepewa zawadi nyingi na Sulatan wa Zanzibar wa wakati huo.
Mambo yakaja kubadilika Zanzibar chini ya sultani Barghash kwenye miaka ya 1870, ambapo alimwagiza kijana aliyefahamika kwa jina la muhammed Ibrahim kwenda Misri kwa ajili ya kujifunza mziki huo wenye kukonga nyoyo za masultani. Na aliporudi aliwafundisha vijana wengine na wakaunda kundi la taarabu hapo hapo Zanzibar miaka ya 1890.Na wakati huo kundi la kijana huyo likizidi kuendelea kisiwani hapo, kukaibuka vijana wengine waliotokea kuupenda mziki huo na kuanza kujifunza zaidi.
Mpaka kufikia miaka ya 1905, kuliundwa kundi lingine la taarabu lililojulikana kama Akhwan-Safa. Kundi hili lilihusisha wanamuziki wa kiarabu na walitumia Lugha ya kiarabu,na walikuwa wakitoa burudani katika maeneo ya Darajani Krabu katika Mji wa Mawe (stone Town), watu wengi walilipenda sana kundi hili la muziki wa taarabu na kusikika kila kona ya mji hapo Zanzibar.
Mambo hayakuishi hapo, kwani miaka ya Baadae hasa kwenye miaka ya 1908, kukaundwa kundi jingine lililofahamika kwa jina la Naadi Shuba ambalo pia lilikuwa na wanamuziki wa kiarabu waliotokea visiwa vya Komoro na wao pia walitumia Lugha ya kiarabu. Kama ilivyo kwa makundi yaliotangulia, kundi nalo lilipendwa sana kwa kuwa lilitumia lugha ya kiarabu ambao ndio waliokuwa watalawa maeneo hayo.
Mabadiliko makubwa yalikuja kutokea kwenye miaka ya 1920 baada ya kuundwa kwa kundi la taarabu lililohusisha wanamuziki wa Kiswahili, kundi hili lilikuja kupendwa sana na watu wengi pale Zanzibar na Afrika mashariki kwa ujumla. Na sababu ya kupendwa ni kutokanana matumizi ya lugha ya Kiswahili ambayo inaeleweka na wakazi wengi waliokuwa wakiiishi kisiwani hapo.
Kundi hili lilianzishwa na mwanamuziki mkongwe wa taarabu aliyefahamika kwa jina la Siti Bint Saad( alizaliwa katika kijiji cha Kisaumi na baadae kuja mjini baada ya kugundulika kuwa na sauti nzuri kwa ajili ya taarabu), mwanamuziki huyu alipendwa kutokana na uwezo wake wa kuimba kwa Lugha tatu yaani Kiswahili, kiarbu na kihindi.
Yeye akiwa na kundi lake waliweza kurekodi album yao ya kwanza mwaka 1930 huko nchini India. Na jambo la kufahamu ni kwamba kulikuwa na mabadiliko ya mambo yalikuwa yakiimbwa kwenye mziki wa taarabu. Kwa mfano wakati huo(1930) mziki wa taarabu ulikuwa ukiimba mambo ya mapenzi lakini kipindi cha kudai uhuru (1950-1960) ulitumika kisiasa zaidi.
Na mara baada ya uhuru mziki huu uliweza kufika maeneo ya Tanzania bara hasa yale maeneo ya pwani kama Dar es Salaam na Tanga. Ambapo kwaTanga kuna mwanamuziki kama BI.Shakira. na kusambaa kwa mziki huu Tanzania bara kulitokana na uwepo wa wanamuziki mahiri wa taarabu kama wakina Bibi Kidude.
Kwa ujumla Mpaka sasa mziki wa taarabu hasa wa Kiswahili unapendwa sana na baadhi ya watu nchini Tanzania na Afrika mashariki kwa ujumla. Na wanamuziki wa taarabu kwa sasa na hata hapo awali wanaheshimika na kujipatia mafanikio makubwa katika maisha yao.
Mafanikio hayo yanakuja kutokana na kuwana mashabki wengi ambao ugharamia kununu kanda za mziki wa taarabu au wakati mwingine kuhudhuria matamasha ya mziki wa taarabu. Wapo wanamuziki wengi sana ambao wamefaidikana bado wanafaidika sana, baadhi yao ni khadija Kopa, Mzee Yusuph na Aisha mashauzi.
Hiyo ndiyo historia ya chimbuko la Muziki wa Taarabu kutoa katika lugha ya kiarabu mpaka lugha ya kiswahili Afrika mashariki. Maandiko haya ni sehemu ndogo sana ya historia ya mziki wa Taarabu, hivyo mawazo yako yanahitajika sana.

Hakuna maoni:
Chapisha Maoni