arijani Rajabu kwa
vyovyote ni mmoja wa wanamuziki ambao wametoa mchango mkubwa katika
ulimwengu huu wa muziki. Japo ni miaka mingi toka mauti yake
yalipomfika, bado nyimbo zake zinapigwa na wanamuziki mbalimbali
majukwaani na hata kurudiwa kurekodiwa tena. Marijani alizaliwa maeneo
ya Kariakoo mwaka 1954. Mama yake alikuwa mama wa nyumbani wakati baba
yake alikuwa na shughuli za uchapishaji. Maisha yake ya utoto yalikuwa
ya kawaida ila alikuwa kipenda sana uimbaji wa Tabu Ley na mwimbaji
mmoja wa Guinea Sorry Kandia. Alilelewa vizuri kwa misingi ya dini ya
Kiislam kwa hivyo alihudhuria mafunzo ya dini utotoni kama inavyotakiwa.
Akiwa na umri wa miaka 18 hivi, alijiunga na STC Jazz, ikiwa chini ya
mpiga gitaa maarufu wakati huo Raphael Sabuni, kabla ya hapo bendi hii
ilikuwa unajulikana kama The Jets. Katika bendi hii Marijani aliweza
kutoka nje ya Tanzania kwa mara ya kwanza ambapo alikwenda Nairobi na
kurekodi nyimbo zilizotoka katika label ya Phillips. Mwaka 1972 Marijani
alihamia bendi ya Safari Trippers. Hapa ndipo ubora wake ulifunguka
haswa na kuweza kuinyanyua Safari Trippers kuwa moja ya bendi maarufu za
wakati huo. Waliweza kutoa vibao vilivyopendwa mfululizo na kuweza
kuzunguka nchi nzima. Vibao kama Rosa nenda shule, Georgina,Mkuki
moyoni, viliweza kuuza zaidi ya nakala 10000 za santuri na hivyo
kuwezesha bendi kuwa na vyombo vyake vizuri. Bendi wakati huo ikiwa na
wanahisa wanne, ambao kwa bahati mbaya wakati bendi ndio iko juu,
wakakosa kuelewana na ukawa ndio mwisho wa bendi hiyo. Miezi michache
baadae Marijani na wenzie waliibukia Dar International. Pia huku
kulikuwa na wanamuziki wazuri na haraka bendi ilipata umaarufu wa hali
ya juu kwa vibao vyake kama Zuena na Mwanameka. kutokana na hali wakati
huo bendi ilirekodi vibao hivi RTD na kuambulia sh 2500/- tu.
Kilichosikitisha zaidi ni kuwa nyimbo zao tisa ziliuzwa kwa kampuni ya
Polygram bila ridhaa yao. Kati ya mwaka 1979 na 1986 bendi ilipiga
karibu kila wilaya nchi hii na kufurahisha sana watu na mtindo wao wa
Super Bomboka. Uchakavu wa vyombo hatimae mwaka huo 1986, ukamaliza mbio
za bendi hii. Kwa miezi michache Marijani akashiriki katika lile kundi
kubwa la wanamuziki 57 waliotengeneza Tanzania All Stars, kundi hili
lilirekodi vibao vinne ambavyo si rahisi kwa bendi zilizopo sasa kufikia
ubora wake kimuziki. Marijani alipitia Mwenge Jazz kw muda mfupi, na
kukaa kama mwaka mmoja Kurugenzi Jazz ya Arusha, kisha akajaribu
kuanzisha kundi lake la Africulture na mtindo wa Mahepe lakini kwa
ukosefu wa vyombo mambo hayakuwa mazuri. Kufiki1992 hali ya Marijani
ilikuwa ngumu akiishi kwa kuuza kanda zake ili aweze kuishi.Pamoja na
nyimbo nyingi, za kuimbia Chama tawala na serikali, na hata tungo yake
Mwanameka kutumiwa katika mtihani wa kidato cha Nne. Rajabu Marijani
hajawahi kukumbukwa rasmi kama mmoja wa wasanii bora Afrika ya Mashariki
CHANZO KITIME BLOG
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni