Jumatatu, 10 Septemba 2018

Watoto laki tano kufa kwa njaa mwaka huu: Save the Children

Watoto wanatarajiwa kufa kwa njaa maeneo ya mapigano


Shirika la kimataifa linalohusika na watoto la Save the Children, linakadiria kwamba zaidi ya watoto laki tano wa kike na wa kiume wanatarajiwa kufa kwa njaa mwaka huu katika nchi zilizokumbwa na mizozo na hivyo huduma za kibinadamu kushindwa kufikishwa katika maeneo hayo.
Shirika la Save the Chlidren limesema kuwa kwa mjibu wa takwimu za umoja wa mataifa ni kwamba mwakaja pekee kuna matukio zaidi ya 1000 yaliyosababisha kuzuiwa kwa misaada ya kibidamu kuwafikia raia waliokuwa katika maeneo yenye machafuko idadi ambayo imekuwa na ongezeko mara mbili tangu mwaka 2012
Hata hivyo ongezeko ni kubwa kutokana na mapigano katika nchi za Sudan Kusini,Yemen,Mali na Syria.


Mkurugenzi mkuu wa shirika la Save the Children Kevin Watkins,anasema kuwa kwa sasa imekuwa ni jambo la kawaida njaa kutumika kama silaha ya kivita.
Hata hivyo jambo jingine lililotajwa na shirika hilo,ni pande zinazopigana,kuzuia misaada ya kibinadamu kwa makusudi hali inayosababisha hali ngumu kwa raia waliokwama maeneo ya mapigano.
Kwa mjibu wa takwimu za umoja wa mataifa, mwaka jana pekee kulikuwa na matukio 1,460 ya mashirika ya misaada kukataliwa kuwafikia watu wenye mahitaji ya kibiandamu katika maeneo ya mapigano.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni