Jumatatu, 10 Septemba 2018

Kifo cha Mohammed Kirumira kimezusha masuali kuhusu ongezeko la vifo vya maafisa wa usalama Uganda


 

Rais wa Uganda Yoweri Museveni Jana usiku alihutubia taifa ambapo alizungumzia masuala kadhaa ambayo yameshuhudiwa nchini humo siku za hivi karibuni.
Hotuba ya rais iliangazia sana changamoto za usalama zinazoikumba nchi kwa sasa. Lakini pia alizungumzia masuala ya kawi, elimu, kilimo na miundo msingi.


Museveni alitoa hotuba yake kwa taifa saa kadhaa baada ya afisa maarufu wa cheo cha juu Muhammad Kirumira, kuuawa kwa kupigwa risasi karibu na nyuambani kwake kwenye vitongoji vya mji mkuu Kampala Jumamosi usiku.
Kirumira ambaye ni afisa aliyekuwa anakumbwa na utata aliuawa hatua chache kutoka nyumbani kwake huko Bulenga.








Machi mwaka 2017, Felix Kaweesi, msemaji wa jeshi la polisi nchini Uganda aliuawa kwa kupigwa risasi


Mwandishi wa BBC aliye mjini Kampala anasema Museveni alizungumzia mauaji ya hivi punde ya Bw Kirumira, aliyekuwa mbunge Ibrahim Abiriga na aliyekuwa msemaji wa polisi Felix kaweesi.
Alisema njia bora za kupambana na uhalifu zinahitaji kuanza kutumiwa kwa mfano kuwekwa alama za vidole kwenye bunduki zote.
"Kama bunduki zote zingekuwa na alama, mara unapopigwa risasi ikiondolewa na kupelekwa kwenye mashine, inaweza kutambuliwa risasi imetoka kwa bunduki namba fulani. Kama magari na pikipiki zingekuwa na namba za elektroniki sasa hivi tungekuwa tungemjua muuaji," alisema Museveni
 Mwezi Juni mbunge Ibrahim Abiriga aliuwa pamoja na mlizi wake karibu na nyumbani kwake

Mfululizo wa mauaji Uganda yatia wasiwasi

Kirumira ni kati ya watu kadhaa wakiwemo meja Mohammed Kigundu na Felix Kaawesi waliouawa katika hali kama hiyo katika kipindi cha miaka 2 iliyopita,
Machi mwaka 2017, Felix Kaweesi, msemaji wa jeshi la polisi nchini Uganda aliuawa kwa kupigwa risasi alipokuwa akiendesha gari kwenda kwa nyumbani kwake. Wauaji wake bado hawajapatikana.
Mwezi Juni mbunge Ibrahim Abiriga aliuwa pamoja na mlizi wake karibu na nyumbani kwake nje ya mji wa kampala, hakuna mtu aliyekamatwa kufuatia mauaji hayo.


Kirumira alisema alikuwa akiishi kwa hofu kwa sababu ya vitisho vya kuuliwa alivyokuwa akipata, lakini kwamba hilo halikumzuia kusema ukweli.
'Tunawafichua waovu ili tuliokoea taifa. Ukizungumza unakufa, ukinyamaza unakufa basi ni bora uzungumze na ufe wakati ujumbe umewafikia watu.
"Basi ujumbe wangu kwa wauaji wanaoshika bunduki ni kwamba, mukiniua ni bure tu. Kwa sababu kama mjumbe nimetekeleza lengo langu la kuwasiliana na jamii' Kirumira aliwaambia waandishi habari Uganda kwa wakati mmoja


Watu nchini uganda walitoa maoni kuhusu mauaji hayo. Wakitumia mitandao ya kijamii wakihoji ni kwa nini kuna uhalifu mwingi unaohusu bunduki nchini humo.
Wiki tatu zilizopita, Uganda ilikumbwa na maandamano kufuatia kukamatwa na kuteswa wabunge Robert Kyagulanyi na Francis Zaake.
Vikosi vya Uganda vilijibu kwa kuwapiga risasi watu sita na kuwajeruhi wengine kadhaa.
Habari za kuuawa kwa Kirumira ziliwashutusha wengi ndani na hata nje ya Uganda.
Muda mfupi kabla ya kuhotubia taifa, Rais Museveni pia alitoa rambi rambi zake katika ujumbe huuu kwenye twitter kufuatia mauaji hayo ya Kirumira


Kadhalika kuna wanaojadili kuusu kuendelea kushuhudiwa kwa mauaji ya maafisa wa polsi na wa jeshi katika kesi ambazo bado mpaka sasa hazijatatuliwa.

 

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni