Hatua
ya mahakama moja nchini Misri ya kuthibitisha hukumu ya kifo kwa watu
75, haikufuata utaratibu unaostahili katika kusikiliza kesi na endapo
hukumu hiyo itatekelezwa itakuwa ni ukiukwaji mkubwa wa haki.
Ameongeza kuwa suala linguine linalokiuka haki ni hatua ya hatua ya Misri ya kuwahukumu watu wengi kwa mkupuo na sheria mpya iliyopitishwa ambayo inawapa kinga maafisa wa vyombo vya dola dhidi ya kushtakiwa kutokana na makosa ambayo huenda wameyatenda.
Hukumu hiyo ya kifo ilitangazwa vifo wakati wa hukumu ya pamoja iliyotolewa Julai mwaka huu ambapo watu 739 walihukumiwa kwa makossa mbalimbali kutokana na maandamano ya Agosti mwaka wa 2013 yaliyoongozwa na wafuasi wa kundi la Muslim Brotherhood ambayo yalizimwa na jmabavu ya jeshi la polisi..
Bi. Bachelet amesema, “ jinsi kesi ilivyoendeshwa katika mahakama ya jinai mjini Cairo, imekosolewa vikali…na ni sahihi kufnya hivyo, watu 739 wameshtakiwa kwa mkupuo na hawakukubaliwa hata mmoja kuwakilishwa na mawakili mahakamani na wala hawakupewa fursa ya kujitetea.”
Ameongeza kuwa, “washukiwa hawakupewa haki ya kutoa ushahidi wao na pia upande wa mashtaka haukutoa ushahidi wa kutosha kuweza kuthibitisha kweli wana hatia .Hivyo hukumu ya kifo kwa watu 75 iliyohakikishwa jana, endapo itatekelezwa itakuwa ni ukiukwaji mkubwa wa haki na sharia ambao haitowezekana kuugeuza.”
Bi Bachelet amesema ni matumaini yake kuwa mahakama ya rufaa ya Misri itatengua hukumu hiyo na kuhakikisha kuwa viwango vya kimataifa vya sheria vinafuatwa na pia vinaheshimiwa.
Kamatakamata ya jeshi dhidi ya maandamano ya kundi la Muslim Brotherhood katika maeneo ya Rabaa al-Adawiya, uwanja wa Rabaa al-Adawiya na katka jukwa la Nahda mjini Cairo tarehe 14 Agosti 2013, yanadaiwa kusababisha vifo vya watu 900 na wengi ni raia ambao hawakuwa na silaha. Mauaji yanadaiwa kufanywa na vikosi vya serikali ya Misri. Baadae serikali ilidai kuwa waandamanji wengi walikuwa wamebeba silaha na kuwa polisi kadhaa waliuawa.
Wakati huohuo Julai mwaka huu, bunge la Misri lilipitisha sheria inayowapa kinga askari dhidi ya makossa yaliyotokea kati ya Julai 3 2013, hadi siku ambayo jeshi lilipindua serikali ya rais Morsi na pia Januari 10 mwaka wa 2016.
Sheria hiyo inampa uwezo rais kuwateuwa askari kadhaa kuwa askari wa kikosi cha akiba na kuwapa kinga na vile vile kumpa kinga ya kidiplomasia waziri yeyote akiwa ofisini au akiwa ziarani nje ya nchi.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni