Mwili wa aliyewahi kuwa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Kofi Annan,
ambaye alifariki mwezi uliopita, umewasili katika nchi aliyozaliwa,
Ghana.
Mwili
wake uliwasili katika Uwanja wa Ndege wa Kotoka International Airport
mjini Accra, ukisindikizwa na familia yake na maafisa wengine wa Umoja
wa Mataifa
Kulikuwa na hali ya maombolezowakati mwili wake
ukiwasili uwanjani hapo na kupokelewa na Rais wa Ghana Akufo Addo na
viongozi wa kimila na kwa heshima ya kijeshi.
Mwili wake umehifadhiwa katika Ukumbi wa Kimataifa wa mikutano wa Ghana, wakati ukisubiri kuzikwa.
Kofi
Annan alikuwa ni Katibu mkuu wa kwanza wa Umoja wa Mataifa, kutoka
katika eneo la kusini mwa jangwa la Sahara na kuleta mafanikio sio tu
katika bara la Afrika, lakini pia dunia nzima.
Chanzo BBC
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni