Jumanne, 11 Septemba 2018

Mama Samia awataka Wananchi kuchukua tahadhari juu ya ugonjwa wa Ebola


Makamu wa Raisi wa Tanzania Samia Suluhu Hassan amewataka wananchi mkoani Kigoma kuchukua tahadhari ya ugonjwa wa ebola kwa kutopokea wageni kiholela wanaoingia nchini bila kufuata utaratibu wa kisheria.

Samia ametoa wito huo wakati akizungumza na wananchi wa Kijiji cha Mwakizega wilayani Uvinza na kuwataka kufuata ushauri wa wataalamu wa afya juu ya njia za kujikinga na ugonjwa huo.

Aidha amesema ugonjwa huo ni hatari ikilinganishwa na magonjwa mengine na kwamba kwa sasa ugonjwa huo umeripotiwa kushamiri katika nchi ya Kongo Mashariki inayopakana kwa karibu sana na mkoa wa Kigoma.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni