Jumanne, 11 Septemba 2018

Magari mawili yagongana njia panda Dodoma

 Taarifa zilizotufikia hivi punde zinaeleza kuwa, kuna ajali imetokea asubuhi hii ya Jumanne, Septemba 11, 2018 ikihusisha gari la serikali (STK) aina ya V8 na gari binafsi kugongana eneo la Nanenane jijini Dodoma.

Inasemekana V8 ilikuwa ikilipita gari jingine njiapanda ya kwenda Chuo Kikuu cha Dodoma (UDOM) na gari ndogo iliyokuwa mbele ikaingia ghafla kuelekea UDOM ndipo ajali ilipotokea.

Inaelezwa kuwa gari hilo ni la kiongozi wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) lakini baada ya kuzungumza na RPC wa Dodoma, Girres Muroto amesema hajapata taarifa za tukio hilo bado.

Endelea kufuatilia taarifa zaidi kupitia mtandao wetu.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni