Jumatano, 12 Septemba 2018

Vijue vinywaji vya ajabu vinavyotamba duniani


1. The Sourtoe Cocktail
Hicho ni kinywaji kinachopatikana katika Jiji la Dawson, Canada, maeneo ya Yukon.  Kinywaji hicho huwa kina kidole cha mguu wa binadamu ndani yake ambacho kimekolezwa chumvi.  Kiuhalisia, hutakiwi kukila kidole hicho, japokuwa wengine huvila kwa bahati mbaya.  Lakini wakati unamalizia kinywaji hicho kwenye bilauri, ni dhahiri kidole hicho kitagusa midomo yako!

2. Snake Wine
Hiyo ni divai (wine) inayopatikana nchini Vietnam, ambayo ndani yake huwekwa nyoka wazima, wakabakia humo wakiwa wazima au wamekufa.  Wanywaji wasioogopa, hunywa divai hiyo na kuwala nyoka hao.

3. Seagull Wine
Hii ni divai inayotumiwa na Waeskimo ambapo ndani yake hutumbukizwa ndege wa baharini aliyekufa kwa ajili ya kuikoleza.  Kwa hiyo, wanywaji huamua wenyewe matumizi ya ndege huyo.

4. Lizard Wine
Hii ni divai inayotokana na mchele ambayo inatumiwa nchini China.  Ndani yake hujazwa mijusi ambapo mchanganyiko huo hudaiwa kumlinda mnywaji dhidi ya mapepo mabaya.

5. Chicha de Muko
Hii ni pombe ya mahindi ambayo kutayarishwa kwake ni pamoja na kuyatafuna mahindi na kisha kuyatemea kwenye chombo maalum ambamo huwekwa na kuchanganywa na vitu vingine hadi inakuwa pombe.

6. Kumis (Fermented Mare’s Milk)
Hii ni pombe itokanayo na maziwa ya farasi yaliyowekwa hadi yakachachuka, inatumiwa na watu wa Mongolia.

7. Yak Butter Tea
Hii ni chai inayotumiwa huko Tibet ikiwa ni mchanganyiko wa siagi, majani ya chai na chumvi ambavyo huongezewa ngano iliyokaangwa na maziwa ya mtindi.

8. Bilk (Milk Beer)
Hii ni bia inayotumiwa nchini Japan ikiwa ni mchanganyiko wa maziwa, shayiri na mimea ya mihopi (hop).

9. The Aunt Roberta cocktail
Hiki ni kinywaji cha mchanganyiko wa gin,  vodka, brandy, matunda aina ya absinthe  na blackberry.  Kinatumika pia kusafishia vyombo ikiwa ni pamoja na kudeki sakafu.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni