Jumatatu, 10 Septemba 2018

Bondia wa kitanzania kampiga KO muingereza nyumbani kwao

Good News kwa Tanzania imepokelewa leo kutoka kwa Bondia wa kitanzania Hassan Mwakinyo ambaye ameingia kwenye headlines baada ya kumtembezea kichapo bondia wa kiingereza Sam Eggington.
Ushindi wa Hassan Mwakinyo unakuja dhidi ya Sam Eggington wiki mbili tu baada ya kupata taarifa na kuanza maandalizi, Hassan ameshinda kwa Knock Out dhidi ya Sam kwa kumpiga round ya 2 katika pambano la round 10.

Pambano  hilo la round 10 za uzito wa kati lilifanyika katika mji wa Birmigham nchini England, licha ya kuwa na sapoti kubwa kwa Sam Eggington kutokana na kuwa nyumbani hakuweza kupata ushindi dhidi ya Hassan.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni