Jumanne, 11 Septemba 2018

Ajali ya Gari la Kubeba Mbao Yaua Watu Wanne Rombo

Na Dixon Busagaga,Rombo.
Watu  wanne wakiwemo wawili wa familia moja wamefariki dunia papo hapo baada ya gari walilokuwa wakisafiria aina ya Isuzu kuacha njia na kwenda kugonga gema katika eneo la Kikelelwa wilayani Hai.

Waliofariki dunia wametambulika kwa majina ya Emanual Josephat Silayo (28) ,Viviano silayo (35) wakazi wa Mbomai Juu,Juma Idd (20) maarufu kama mwarabu na mwingine aliyefahamika kwa jina moja la Deolla .

Kamanda wa polisi mkoa wa Kilimanjaro Hamis Issah aliyefika eneo la tukio amethibitisha kutokea kwa ajalo hiyo na kwamba dereva wa Loli hilo lililokuwa limebeba mbao alikimbia kusiko julikana baada ya ajali..

"Jitihada za kumtafuta dereva zinafanyika na chanzo cha ajali ni kupoteza muelekeo kwa Lori hilo na baadae kugonga Gema ndipo watu waliokuwa wanmekaa mbele walichomoka na kwenda kupigiza vichwa katika Gema na kupasuka"alisema Kamanda Issah.

Kamanda Issah amesema gari hilo likiwa na shehena ya mbao lilikuwa likitokea eneo la West Kilimanjaro ,eneo maarufu kwa uchanaji wa mbao na kwamba lilikiwa likielekea Rombo kupitia njia ya Rongai.

"Ni gari la kubeba mbao lilikua linatoka West Kilimanjaro kupitia njia ya Kikelelwa wilayani Rombo ,Gari aina ya Isuzu likiwa na namba za usajili T 889 ACN lilimshinda dereva na kuacha njia na baadae kugonga ngema iliyosababisha watu wanne waliokuwemo katika gari hilo kufa papo hapo." alisema Kamanda Issah.

Miili ya marehemu wote imehifadhiwa katika hosptali ya wilaya ya Rombo kwa ajili ya maandalizi ya mazishi.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni