Beki wa kushoto wa klabu ya Manchester United na timu ya taifa ya
England Luke Shaw aliyepata mshtuko baada ya mgongano wa bahati mbaya na
beki wa Uhispania Dani Carvajal katika nusu ya pili ya mchezo
uliowakutanisha miamba hao wawili ambapo England akiwa nyumbani
alifungwa goli 2-1 na Hispania
Baada ya majeraha hayo ya kichwa Shaw alirudi United kwa ajili ya
ufuatiliaji zaidi na matibabu siku ya Jumatatu licha ya beki huyo kuumia
wakati anaitumikia timu yake ya taifa.
akiongea na wanahabari kocha wa timu ya taifa ya England Gareth
Southgate alisema ” Hakuna mtu aliyetamani kuona tukio kama hilo”na
kuongeza kuwa Shaw alitolewa uwanjani akiwa amefungwa vifaa vya
kumuingizia hewa ya oksijeni lakini alisema kuwa amepata tena ufahamu
haraka katika chumba cha matibabu, na hivi karibuni alikuwa akiwasiliana
na marafiki na familia.
Baada ya beki huyo kisiki mwenye ustadi wa aina yake kuumia katika
mchezo huo wa jumamosi dhidi ya Uhispani huku kocha wake Jose Mourinho
akishuhudia jukwaani, msaada wa beki huyo utakosekana katika timu yake
ya Manchester United katika mchezo wao wa siku ya jumamosi dhidi ya
Watford,hivyo Luke Shaw hatakuwepo kwenye mchezo huo utakaofanyika
katika dimba linalomilikiwa na The Golden Boys au jeshi la njano Watford
linalojulikana kama Vicarage Road Stadium.
Siku chache kabla, Shaw alikuwa amefungua hadithi ya hofu ya mguu wake
uliovunjika, ambalo alikiri alikuwa karibu na kumchukuliwa na
kumlazimisha kufikiria kustaafu kutoka mchezo huo kwa umri wa miaka 23
tu.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni