Jumapili, 9 Septemba 2018

Malengo ya SDGs sasa pia ni kwa watoto wa shule za Chekechea. :UN


 




Umoja wa Mataifa kwa ushirikiano na kampuni ya Mattel, Inc.,umezindua aina mpya ya  mawasiliano  ya kufikisha ujumbe wa  malengo ya maendeleo endelevu , SDGs kwa watoto wa shule za Chekechea.
Aina hiyo mpya ni  kupitia vipindi vya mlululizo vya vikaragosi maarufu vya  Thomas na rafiki zake (Thomas and Friends.)
Kupitia taarifa iliyotolewa katika uzinduzi wa ushirika huo uliofanyika leo kwenye Makao Makuu ya Umoja wa Mataifa mjini New York  Marekani, imesema malengo saba kati ya 17 ya maendeleo endeleo  yatajumuishwa vipindi 8 kati ya mlululizo wa vipindi 26  vipya vya vikaragosi hivyo vya Thomas & Friends, ambavyo vinaanza kurushwa  leo rasmi nchini Marekani kupitia kipindi chaneli ya Nick Jr, wakati kwingineko duniani vitaanza kurushwa hewani  miezi kadhaa ijayo.
Malengo yatakayohusishwa katika vipindi hivyo ni namba 4 lihusulo elimu bora; namba 5 la usawa wa kijinsia; namba 11miji na jamii endelevu , namba 12 la uzalishaji na matumizi endelevu na  namba 15 kuhusu maisha ya nchi kavu katika sayari hii.
Katika uzinduzi huo mkurugenzi wa kitengo cha uhusiano wa nje kwenye idara ya habari kwa umma ya Umoja wa Mataifa (DPI), Maher Nasser, amesema, “katika juhudi za kutaka malengo ya SDGs  kujulikana na kuhamasisha watu wa rika zote, Thomas & Friends ndio chaguo kwa watoto pamoja na wazazi wao na vilvile  walezi wao.”
Ameongeza kuwa, “Thomas & Friends SDGs imekuwa chombo muafaka kwa kuwafundishia watoto umuhimu wa kushiriki katika juhudi za kimataifa za kukomesha  umaskini, kutoa fursasawa kwa mtoto wa kike na wa kiume na bila shaka tukifanya hivyo huku  tunailinda sayari yetu.”
Ubia huu mpya baina ya Umoja wa Mataifa na Thomas & Friends utatayarisha video funzi  za kuelimisha kuhusu maisha ya utotoni pamoja na vidokezo kwa wazazi na mawasiliano mengine  kupitia wavuti wao mpya,  AllAboutForGlobalGoals.com ambao pia umezinduliwa leo, katika lugha ya kiingereza  na lugha zingine zitafuata hapo baadaye.
Rais wa kampuni ya Mattel, Richard Nixon, amesema kuwa Thomas anafaa sana wakati huu ambapo watoto wanaletewa kwa mara ya kwanza mambo muhimu katika maisha yao kama yalivyo katika malengo ya maendeleo endelevu. Akiongeza kuwa ndio maana Umoja wa Mataifa upo na ndio limekuwa somo muhimu kwa Thomas kwa kipindi cha miaka 70.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni