Jumamosi, 29 Julai 2017

Tamko zito la Jukwaa na Wahariri baada ya Chadema kuwafukuza waandishi TBC

Jukwaa la Wahariri Tanzania (TEF) limesema limepokea kwa masikitiko taarifa ya kufukuzwa kwa waandishi wa habari wa TBC wakati wakitimiza wajibu wao
katika ofisi za Makao makuun ya Chama cha Demokrasia na Maendelea (CHADEMA) zilizopo ofisi za Kinondoni jijini Dar es salaam.






 Soma taarifa kamili:
 

Neno la Okwi kwa Mashabiki wa Simba



 Mshambuliaji wa kimataifa wa Simba kutoka Uganda, Emmanuel Okwi, ametua kambini Afrika Kusini jana na kuwaambia mashabiki wa timu hiyo wajiandae kuona "vitu vyake" katika mechi ya kirafiki dhidi ya Rayon FC itakayofanyika Agosti 8 (Simba Day).


Okwi amewaambia mashabiki na wanachama wa Simba wawe watulivu, amejiandaa kuwapa kile wanachokitarajia kutoka kwake na anafahamu vizuri ndoto za klabu hiyo yenye makao makuu yake Mtaa wa Msimbazi, Kariakoo jijini.

"Nitakuwa Dar es Salaam siku ya Simba Day, najua watu wanahamu ya kuniona, mashabiki wawe watulivu," alisema mshambuliaji huyo

Ijumaa, 28 Julai 2017

Asilimia 53 ya Watanzania Wasema Usalama Umeimarika Nchini- TWAWEZA



Zaidi ya nusu ya Watanzania wamesema kuwa hali ya usalama nchini imeimarika  ikilinganishwa na miaka takriban miwili iliyopita na kuwafanya wananchi waishi kwa utulivu na amani.
Hayo yamesemwa na Mkurugenzi Mtendaji wa shirika lisilo la Kiserikali lijulikanalo kama Twaweza, Bw. Aidan Eyakuze wakati akiwasilisha matokeo utafiti wa “Hapa Usalama Tu: Usalama, Polisi na Haki nchini Tanzania” kupitia sauti za wananchi kwa waandishi wa habari leo jijini Dar es salaam.
Bw. Eyakuze alisema kuwa takwimu zilizo kusanywa na sauti za wananchi kwa mwaka huu zimeonesha kuimarika kwa usalama kwa wananchi wa Tanzania Bara ikilinganishwa na miaka iliyopita.
“Tumeongea na watu 1805 kuwauliza hali ya usalama katika maeneo wanayoishi na asilimia 53 ambayo ni sawa na nusu ya Watanzania Bara wamesema hali ya usalama imeimarika na inaridhisha” alisema Bw.Eyakuze.
Bw.Eyakuze amesisitiza kuwa wamekusanya taarifa kutoka kwa wananchi wenyewe,  kupitia simu zao za mikononi ambapo wameona kuwa watanzania wengi wapo kwenye hali ya usalama na hii inamewapa taswira tofauti na taarifa zinazotolewa na vyombo  vya habari.
Aidha, Bw.Eyakuze amesema kuwa asilimia 47 ya wananchi wanaridhishwa na utendaji kazi wa jeshi la Polisi nchini kutokana na kuzuia na kutatua uhalifu na kuwajali wananchi.
Ripoti hiyo imeonyesha kuwa wananchi wanapata pia ulinzi kutoka kwa polisi jamii, maarufu kama sungusungu na asilimia 41 ya wananchi wamesema wana vikundi vya sungusungu katika maeneo yao na wanaridhika na huduma zinazotolewa.
Utafiti huu ulifanyika mnamo Aprili 2017 ukihusisha mikoa yote ya Tanzania Bara na wa kwanza barani Afrika wenye uwakilishi wa kitaifa unaotumuia simu za mkononi.

Bei ya tiketi kushuhudia pambano kati ya Mayweather na McGregor ni kufuru



 Tiketi za kushuhudia mpambano wa masumbwi kati ya bondia, Floyd Mayweather dhidi ya Conor McGregor zinauzwa kwa dola 150,000.

 Mpambano huo unatajwa kuwa wa gharama zaidi kuwahi kutokea na tiketi kwa sasa zinauzwa kama njugu.
Mayweather mwenye miaka 40 awali alistaafu lakini amerejea kupambana na McGregor.



Unatarajiwa kupigwa Agosti 26 katika uwanja wa T-Mobile mjini Las Vegas utakaoingiza watu elfu 20.
Unaweza ukanunua na wewe Tiketi yako   HAPA   ili ukashuhudie pambano hilo la kukata na shoka.

Mwanariadha, Francis Damian aitoa kimasomaso Tanzania Jumuia ya Madola



 Timu ya taifa ya Tanzania ya mchezo wa riadha ya vijana walio na umri chini ya miaka 17 imerejea kwa kishindo leo baada ya  kutwaa medali ya shaba ya michuano ya sita ya dunia ya vijana ya Jumuia ya Madola (Bahamas 2017 Commonwealth Youth Games) yaliyomalizika hivi  karibuni huko nchini India.


Mwanariadha wa Tanzania, Francis Damian amefanikiwa kushika nafasi ya tatu  katika mashindano hayo na kupata medali ya shaba kwenye mbio hizo kwa upande wa wavulana baada ya kukimbia umbali wa mita 3000 akitumia muda wa 8.37.51 wakipishana kwa sekunde 13.55 na mshindi wa kwanza Mkenya na sekunde 2.36  kwa mshindi wa nafasi ya pili ambaye ni raia wa Canada.
Kwa kutwaa medali hiyo, Damasi Francis ameiwezesha Tanzania kushika nafasi 19 kwenye ushindi wa jumla wa riadha nakufungana na Botswana, Cyprus, pamoja na Afrika Kusini.
Na kufanikiwa kushika nafasi ya 31 kwa ushindi wa jumla wa michezo yote na kufungana na  Nchi za Grenada,Namibia na Rwanda.
Katibu mkuu wa wizara ya Habari , Utamaduni ,Sanaa na Michezo, Elisante Ole Gabriel ameongoza mapokezi ya viongozi na wachezaji hao waliowasili katika uwanja wa ndege wa kimataifa wa Mwl Julius k . Nyerere hii leo.



Ushindi mwingine alioupata Ester Bullaya Mahakamani leo




Leo July 28, 201 7 Mahakama ya Rufaa imeitupa rufani iliyofunguliwa na wapigakura wa Jimbo la Bunda kwenye kesi ya kupinga matokeo ya uchaguzi yaliyompa ushindi Mbunge wa Jimbo hilo, Ester Bulaya. 
Wapigakura hao ambao wanampigania aliyekuwa Waziri wa Chakula, Kilimo na Ushirika na mgombea Ubunge wa CCM Jimbo la Bunda Mjini, Stephen Wasira, ni Magambo Masato, Matwiga Matwiga, Janes Ezekiel na Ascetic Malagila.
Uamuzi huo umetolewa na Naibu Msajili wa Mahakama hiyo, Elizabeth Mkwizu ambaye amesema, upande wa walalamikaji uliwasilisha hoja 10 za kupinga ushindi wa Bulaya, lakini hoja hizo hazikuwa na mashiko, hivyo zinatupiliwa mbali.

Neymar avua jezi ya Barcelona na kuamua kuondoka




Mshambuliaji wa klabu ya Barcelona Neymar Dos Santos leo ametawala upya vichwa vya habari  baada ya kuvua jezi ya mazoezi ya Barcelona na kuondoka uwanjani.
Neymar alikuwa mazoezini na katika hali ya kawaida kulitokea kutokuelewana kati yake na mchezaji mpya wa klabu hiyo Nelson Semedo ndipo Neymar alipokasirika.
Neymar alionekana kutaka kumkabili Semedo lakini wakati anamfuata huku akionekana mwenye hasira ndipo Sergio Bosquet na Javier Mascherano walimzuia.
Baada ya Neymar kuzuiwa kuendeleza ugomvi alivua jezi maalumu ya mazoezi (bibs) akaitupa pembeni kisha akaupiga mpira kwa hasira na kuondoka zake.
Neymar amefanya tukio hilo katika kipindi hiki ambacho anahusishwa na uhamisho wa kwenda katika klabu ya PSG na huku ikitajwa kwamba hana furaha na Barcelona.
Tukio hili limezidi kuongeza tetesi kwamba Neymar anaweza kuondoka Barca lakini Barca kwa upande wao pia wamechoshwa  na tabia za Neymar haswa starehe zake.

Harbinder Seth na Rugemarila wamefikishwa Mahakamani tena leo




Leo July 28, 2017 Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu imeamuru mmiliki wa Kampuni ya kufua umeme ya IPTL, Harbinder  Singh Sethi apewe matibabu kutokana na matatizo ya kiafya yanayomkabili.
Hayo yameelezwa na Hakimu Mkazi Mkuu, Huruma Shaidi baada ya Seth kudai anahitaji kuwa na nguvu ambayo haitopatikana kama Afya yake itakuwa dhaifu, hivyo ameomba apatiwe matibabu.
Kutokana na kuwa afya ni muhimu kwa binaadam, Mahakama imetoa kibali ili mshtakiwa huyo apate matibabu na keshi imeahirishwa hadi August 3, 2017 k
wa ajili ya kutajwa.
 

Alhamisi, 27 Julai 2017

Dunia lazima ijitahidi kulinda na kuhifadhi mikoko:UNESCO




 unia inahitaji kufanya juhudi zaidi kulinda na kuhifadhi mikoko ya pwani ambayo ni miongoni mwa maliasili iliyohatarini duniani. Wito huo uliotolewa leo ni kwa mujibu wa Shirika la Umoja wa mataifa la elimu, sayansi na utamaduni, UNESCO .
UNESCO imetoa wito huo katika siku ya kimataifa ya uhifadhi wa mfumo wa mikoko inayoadhimishwa kila mwaka Julai 26.
Mikoko, na aina zingine za miti zinazoota ufukweni mwa bahari na kwenye mito inasaidia kuimarisha uhakika wa chakula, kuendeleza uvuvi na bidhaa zingine za msituni.
Pia inajukumu muhimu na la kipekee la kukusanya na kuhifadhi kiasi kikubwa cha gesi ya ukaa kutoka hewani na baharini, ambacho ni muhimu kwa kukabiliana na mabadiliko ya tabianchi.
Takribani asilimia 67 ya mikoko imetoweka hivi leo na karibu mikoko yote ambayo hailindwi inaweza kutoweka katika miaka 100 ijayo. UNESCO inaitaka jumuiya ya kimataifa kubadili mwenendo huo wa uharibifu, kwa sababu ya jukumu muhimu la mikoko katika kuhakikisha dunia inakuwa na afya muafaka.

ACACIA yalipa Milioni 460 za ushuru



Mgodi wa dhahabu wa Acacia Bulyanhulu (BGML) uliopo katika Halmashauri ya Msalala, mkoa wa Shinyanga jana Jumatano Julai 26,2017 umekabidhi hundi yenye thamani ya Shilingi 460,732,841.08/= kwa ajili ya ushuru wa Huduma kwa halmashauri ya Msalala.

Akizungumza wakati wa kukabidhi hundi hiyo,Meneja Mkuu wa Mgodi wa Bulyanhulu Graham Crew alisema kiasi hicho ni asilimia 67 ya malipo ya ushuru wa huduma kwa ajili ya kipindi cha miezi sita kuanzia Januari hadi mwezi Juni mwaka huu ambacho ni asilimia 0.3 ya ukokotoaji wa ushuru wa huduma wa mgodi huo katika kipindi hicho.
 
 “Jumla ya malipo ya ushuru wa huduma kwa kipindi cha miezi sita iliyopita ni shilingi za Kitanzania 687,660,956.84/=,ambapo malipo hayo yamegawanywa katika halmashauri mbili ambazo ni Msalala inayopata asilimia 67 na Nyang’wale iliyopo mkoani Geita inapata asilimia 33”,alifafanua Crew.
 
Alisema kutokana na mgawanyo huo,halmashauri ya Msalala imelipwa shilingi milioni 460 (460,732,841.08/= ) na Nyang’wale shilingi Milioni 226 (226,928,115.76/=.
 
“Ushuru umepungua kwa kuwa mgodi haujafanya mauzo ya makinikia ambayo yamezuiwa tangu mwanzoni mwa mwezi machi mwaka huu, hivyo tunafahamu kuwa tutalipa zaidi tutakapouza makinikia ambayo yapo yanaendelea kukusanywa mgodini”,aliongeza Crew.
 
Katika hatua nyingine Crew alisema tangu mwaka 2000 mpaka sasa mgodi huo umelipa zaidi ya shilingi 10,247,742,957/= za kodi ya ushuru wa huduma na kampuni ya Acacia ilianza kutoa malipo ya ushuru wa huduma wa asilimia 0.3 ya mapato ghafi kwa halmashauri husika mwaka 2014.
 
 “Mgodi wetu unaendelea kuwa na matarajio ya kuchangia kuimarisha sekta ya viwanda kwenye uchimbaji madini katika halmashauri ya Msalala huku tukiendelea kutekeleza mkakati wa Jamii Endelevu wa Acacia ulioanzishwa mwaka 2016 kwa kushauriana na wadau lengo likiwa ni kuchangia maendeleo ya Jamii Endelevu inayonufaika na kukua kwa uchumi ndani ya jamii ili kujenga mahusiano ya kuaminika”,alisema Crew.
 
Akipokea hundi hiyo kisha kuikabidhi kwa Mkurugenzi wa Halmashauri ya Msalala, Mkuu wa wilaya ya Kahama Fadhili Nkurlu aliushukuru mgodi wa Acacia Bulyanhulu kwa kuendelea kuunga mkono jitihada za serikali katika kutoa huduma kwa jami.
 
“Hiki kiwango cha shilingi milioni 460 tulichopokea ni kiwango kizuri ingawa kimepungua ulikinganisha na kipindi cha miezi sita cha Mwezi Juni hadi Desemba 2016,furaha inatujaza kwamba ile shilingi milioni 300 na zaidi ipo ndani ya Makinikia, yatakapouzwa tutaipata na tutaendelea kuboresha huduma za kijamii”,alieleza Nkurlu.
 
Nkurulu alimuomba mkurugenzi wa halmashauri ya Msalala kuhakikisha fedha zilizotolewa na mgodi huo zitumike kwa huduma za kijamii kama zilivyokusudiwa ikiwemo kuboresha huduma za afya na miundombinu.
 
Naye Mkurugenzi wa Halmashauri ya Msalala Simon Berege alisema mapato waliyopokea kutoka mgodi huo yako chini kwa shilingi milioni 300 ukilinganisha na kipindi kilichopita cha kuanzia Mwezi Julai hadi Desemba 2016 ambapo mgodi huo ulipokea shilingi milioni 760.
 
“Sisi tumepokea mapato haya kama tunavyopkea mapato mengine tunayopata katika halmashauri zetu,mapato haya ni yako chini ukilinganisha na kipindi kilichopita,tunaambiwa mapato yamepungua kutokana na Makinikia ambapo sasa yamesimama,hii inaleta changamoto katika ukusanyaji wa mapato katika halmashauri yetu, tunaamini mazungumzo baina Acacia na serikali yakiisha halmashauri yetu itapata mapato mengi Zaidi,” aliongeza Berege.
 
 

Tundu Lissu Kaachiwa Kwa Dhamana



 Mbunge wa Singida Mashariki (CHADEMA) na Rais wa Chama cha Mawakili Tanzania, Mhe. Tundu Lissu ameachiwa kwa dhamana ya Milioni 10 leo katika kesi yake iliyokuwa inamkabili ya uchochezi.

Mahakama ya Kisutu imempa dhamana Mh Tundu Lissu kwa sharti la kuwa na wadhamini wawili watakaosaini dhamana ya thamani ya milioni kumi.

Aidha, Mahakama hiyo pia imemtaka Tundu Lissu kutokuondoka nje ya jiji la Dar es Salaam bila kuwa na kibali maalum cha mahakama. Uamuzi huo umetolewa mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu wa Mahakama ya Kisutu Jijini Dar es Salaam, Wilbard Mashauri.

Upande wake Tundu Lissu alikuwa anatetewa na jopo la mawakali 18 likiongozwa na Fatma Karume na Peter Kibatala ambapo katika shauri la kwanza waliomba Mahakama impe dhamana mteja wao.

Tundu Lissu alitiwa katika mikono ya dola mnamo Julai 20 siku ya Alhamsi katika uwanja wa ndege akiwa anaelekea nchini Rwanda. na siku iliyofuata  jeshi hilo lilikwenda kufanya upekuzi nyumbani kwa Mbunge huyo.
Aidha kesi yake imepangwa kusikilizwa Agosti 24 mwaka huu baada ya wadhamini wake kukamilisha taratibu zote za kumdhamini.

“Walioshindwa kuviendesha Viwanda akiwemo Mbunge wa CCM wavirudishe” – Rais JPM




Rais wa Magufuli amewaagiza viongozi wa Manispaa ya Morogoro na viongozi wa Mkoa huo kuwaacha wafanyabiashara wadogo wadogo waendelee kufanya biashara zao katika eneo la Kituo Kikuu cha mabasi, Msamvu.
Rais Magufuli ametoa agizo hilo leo July 27, 2017 baada ya msafara wake uliokuwa unatokea Dodoma kuelekea Dar es Salaam kusimamishwa na wananchi eneo la Msamvu na kumueleza kero ya kunyanyaswa na Manispaa wakifukuzwa katika maeneo wanayofanyia biashara hasa baada kituo cha mabasi cha Msamvu kujengwa upya.
Mbali na hilo, Rais Magufuli amemuagiza RPC Morogoro SACP – Ulrich Onesphory Matei kuhakikisha Askari Mgambo hawawasumbui wafanyabiashara wadogo wadogo na kuwataka wafanyabiashara hao kutofanya vurugu wakati utaratibu mzuri unaandaliwa kwa ajili yao.
Aidha, Rais Magufuli amewataka watu waliobinafsishiwa viwanda mbalimbali mkoani Morogoro kuvirejesha Serikalini kama wameshindwa kuviendeleza ili wapewe wawekezaji wengine wenye uwezo wa kuviendeleza na kuzalisha ajira.
>>>”Ninarudia wito wangu nilioutoa nyuma, kwamba wenye viwanda hapa Morogoro ambao wameshindwa kuviendesha, akiwemo Mbunge wa hapa wa CCM ambaye alibinafsishiwa viwanda vingi,  kama ameshindwa kuviendesha avirudishe ili tuwape watu wengine kwa sababu vijana hawa wanakosa ajira, nazungumza kwa uwazi kwa sababu msema kweli ni mpenzi wa Mungu.” – Rais Magufuli.


 

Jumatano, 26 Julai 2017

Twaweza waibuka na Utafiti kuhusu Jeshi la Polisi



 Taasisi huria ya Tafiti Nchini Twaweza wanataraji kutoa majibu utafiti Mpya unaohusu usalama wa Nchi pamoja na Jeshi la Polisi.

Utafiti huo unatarajiwa kutolewa majibu kesho Tarehe 27, Julia , kwenye Ukumbi wa Makumbusho ya Taifa Posta Jijini Dar es Salaam.

Msemaji Mwendeshaji ni Aidan Eyakuze wa Twaweza, wasemaji waalikwa ni Msemaji wa Jeshi la Polisi Nchini Barnabas Mwakalukwa na Mwandishi wa habari  Mkongwe Richardz Mgamba.




Haya ndiyo Maajabu 6 ya Dunia

 https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEiNx4BGWuM0NWSNse1jdPIACzXnLPCgagqwZhTafXqRFNsYNFidTNYweihsrzTEEZwc-G2Afi43sAmFaxfvJI28UVHBaR_nz5Ja7n_YeYhhwHVTV7V6I7BggZF9mXbKzkRt-GItc5jfHLu2/s1600/The_Great_Wall_of_China_at_Jinshanling-edit.jpg
​1. Ukuta mkubwa wa china (the great wall of china)
Taj Mahal, IndiaUkuta Mkuu wa China ni mfululizo wa ngome iliyojengwa na   mawe, matofali, mbao, kuni, na vifaa vingine, kwa ujumla kujengwa kwenye mstari wa mashariki hadi magharibi kulinda mpaka wa kihistoria wa kaskazini ya China ili kulinda nchi Kichina na himaya dhidi upekuzi na uvamizi wa mbalimbali makundi kuhamahama ya Eurasian Nyika. Kuta kadhaa walikuwa inajengwa mapema kama karne ya 7 KK; hayo, baadaye alijiunga pamoja na kufanywa na nguvu kubwa, sasa pamoja inajulikana kama Ukuta Mkuu Hasa maarufu ni ukuta kujengwa 220-206 KK. na Qin Shi Huang, Mfalme wa kwanza wa China. Kidogo ya kwamba ukuta bado. Tangu wakati huo, Ukuta Mkuu ina na mbali wamekuwa upya, iimarishwe, na kuimarishwa; Wengi wa ukuta uliopo ni kutoka nasaba ya Ming.

Madhumuni mengine ya Ukuta Mkuu kuwa ni pamoja na udhibiti wa mpaka, kuruhusu kuanzishwa kwa ushuru wa bidhaa kusafirishwa pamoja Silk Road, kanuni au faraja ya biashara na udhibiti wa uhamiaji na uhamiaji. Aidha, sifa kujihami ya Ukuta Mkuu walikuwa kuimarishwa kwa ujenzi wa zamu minara, askari kambi, vituo ngome, dalili uwezo kwa njia ya moshi au moto, na ukweli kwamba njia ya Ukuta Mkuu pia aliwahi kuwa ukanda usafiri .

Ukuta Mkuu huo wa stretches kutoka Dandong  mashariki, hadi katika Ziwa Lop katika magharibi, pamoja arc kwamba takribani delineates makali ya kusini ya Mongolia ya. Kina Archaeological utafiti, kwa kutumia teknolojia ya hali, ina alihitimisha kuwa kuta Ming kupima 8850 km (5500 mi)  Hii ni alifanya juu ya 6259 km (3889 mi) sehemu ya ukuta halisi, 359 km (223 mi) mitaro. na 2232 km (1387 mi) ya vikwazo vya asili kujihami kama vile milima na mito.Utafiti mwingine Archaeological iligundua kuwa ukuta mzima na wote wa matawi yake kupima nje kuwa 21,196 km (13,171
 https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEjeF4S0KYLLXrfzkwVwkyun772tu14FXd7xXD7qwbf5J_AeCG9RPmw2CXxhwVd1zHU_azHdDaQgHaX8TR9v-vJmFOl783MT4fZKtlxL2TT3vYLx6sKOYtqUwCRTcVoMUW308QAYkfnjkSZi/s1600/Colosseum-Rome-Historical-Photo.jpg
2. The Colosseum, Rome, Italy
Colosseum ni ukumbi uliopo  mashariki mwa Jukwaa la Kirumi. Ujenzi ulianza chini ya mfalme Vespasian katika 72 BK, na kukamilika mwaka 80 AD chini ya mrithi wake na mrithi Titus. marekebisho zaidi yalifanywa wakati wa utawala wa Domitian (81-96).Hawa watawala watatu hujulikana kama Flavian nasaba, na amphitheater alitajwa katika Amerika kwa uhusiano wake na familia zao jina (Flavius).

Colosseum unaweza kushikilia, inakadiriwa, kati ya watazamaji  50,000 na 80,000  kuwa watazamaji wastani wa baadhi 65,000 ilitumika kwa ajili ya mashindano gladiatorial na Miwani ya umma kama vile vita maskhara bahari,kuwinda wanyama, kunyonga, re-enactments ya vita maarufu, na michezo ya kuigiza kulingana na Classical Mythology. Jengo wakaacha kutumika kwa ajili ya burudani katika mapema zama medieval. BaadaAye tena kwa madhumuni kama vile nyumba, warsha, robo kwa utaratibu wa kidini, ngome, machimbo, na kaburi la Kikristo.

Ingawa sehemu imeharibiwa na tetemeko la ardhi na jiwe-majambazi, Colosseum bado ni ishara iconic ya Imperial Roma. Ni moja ya vivutio Roma maarufu ya utalii na pia viungo Kanisa Katoliki, kama kila Ijumaa njema Papa inaongoza torchlit "Njia ya Msalaba" maandamano kwamba kuanza katika eneo karibu na Koloseo
Colosseum pia taswira juu ya toleo Italia ya-cent 5 € sarafu.

 

 https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEgA1H20GVW52xzrwAK8orHZyG9i1AB2IC6S53rOiO0SwnSLVC0iO2_ST_89JdigUs6YMrsTsqTHCniN64VozXbXvsmM1Z0vPkD8h-81BaA3PDEk3f4jn5MBbZlqSp5lHdicr6tnFaDH6wq7/s1600/petra2.jpg
3. Makumbusho ya Petra, Jordan
Petra (Kiarabu: البترا, Al-Batrā'; kale Kigiriki: Πέτρα) ni mji wa kihistoria na akiolojia kusini mwa Jordan jimbo la Ma'an na ni maarufu kama mwamba-katwa kwa sababu ya  usanifu wake na mfumo wa maji katika  mfereji. Jinalingine la Petra ni Rose City kutokana na rangi ya mawe yaliyochongoka

Ilianzishwa yakadiliwa mnamo miaka ya  312 BC kama mji mkuu wa Kiarabu Nabataeans, ni ishara ya Jordan, ikiwa ni pamoja na Jordanwatu wengi-hutembelea kama kivutio cha utalii  katika bonde kati ya milima ambayo fomu ubavu mashariki ya Araba (Wadi Araba), bonde kubwa linalotokea  Bahari ya Chumvi na Ghuba ya Akaba. Petra imekuwa chini ya usimamizi wa  UNESCO tangu 1985.

Petra  haikujulikana  kwa ulimwengu wa Magharibi hadi 1812, Hadi ilipogunduliwa na mpelelezi wa Uswisi Johann Ludwig Burckhardt. Ilikuwa kama ilivyoelezwa "rose-nyekundu mji nusu mzee kama wakati." katika Newdigate Tuzo-kushinda shairi na John William Burgon. UNESCO ina alielezea kama "moja ya mali ya thamani zaidi utamaduni wa urithi wa utamaduni wa mtu."
 https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEg-cJ_zYIhkS9cUQ1b6eE4foZs0UpZbFPwU4cY_aV9TvNB3zA1VCjQg4vskSZvSZpMveCAHAOrV1xvZYR0ys1aCFk7p4iH7svm1CUXZN5Jq8dpXJdxkHAdkw8DwU2pb_QzDV-IR0RirnrY1/s1600/View_of_Machu_Picchu_from_Intipunku_the_Sun_Gate_copy.jpg
4. Machu Picchu, Peru
Ni hali ya mgongo mlima juu Valley Mtakatifu, ambao una 80 kilometres (50 mi) kaskazini magharibi ya Cuzco na njia ambayo ni mtiriko wa  Mto Urubamba . Archaeologists wengi wanaamini kwamba Machu Picchu ilijengwa kama isiyohamishika kwa Inca mfalme Pachacuti (1438-1472). Mara nyingi makosa inajulikana kama "Jiji la  Lost ya Incas" (jina kwa usahihi zaidi kutumika kwa Vilcabamba), ni alama  maarufu sana ya ustaarabu ya watu wa Inca. Incas kujengwa isiyohamishika karibu 1450, lakini kutelekezwa karne moja baadaye wakati wa uvamizi wa Hispania . Ingawa unaojulikana kienyeji, haikuwa inajulikana kwa Hispania wakati wa ukoloni na ilibakia haijulikani duniani ya nje kabla ya kufikishwa kwa tahadhari ya kimataifa mwaka 1911 na mwanahistoria wa Marekani Hiram Bingham. Wengi wa waliojenga karibu na eneo hilo mikoani wamehamishwa  ili kupisha watalii  https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEjDRDwgPLb4BWjkUODQiFCaFFm7gAQW_hylrFaQf6Wx5dQZPcGmJE_xOBYaX87jbPbCzdxF7z_OMfY_N132NszKsPEwhAwdFsmTvAIaSokmoNWyYuZuigGJ6DYi6_Q7BW1pZuu2AkOK-2qB/s1600/Chichen_Itza_3.jpg
5. Chichén Itzá, Mexico
Chichen Itza ilikuwa moja ya miji kubwa Maya na kulikuwa na uwezekano wa kuwa mmoja wa miji mythical kubwa, au Tollans, iliyotajwa katika baadaye Mesoamerican maandiko.mji huenda ilikuwa na idadi ya watu  wengi wa aina mbalimbali duniani Maya, sababu ambayo inaweza kuwa na mchango na aina ya usanifu mitindo katika Magofu ya Chichen Itza ni mali ya serikali.

Mpangilio wa Chichen Itza tovuti ya msingi na maendeleo wakati wa awamu yake ya awali ya kazi, kati ya 750 na 900 AD. mpangilio wake wa mwisho ilitengenezwa baada ya 900 AD, na karne ya 10 ulishuhudia kuongezeka ya mji kama mji mkuu wa mkoa kudhibiti eneo kutoka Yucatán kati ya pwani ya kaskazini, kwa uwezo wake kupanua chini mashariki na magharibi pande za peninsula.  mwanzo hieroglyphic tarehe aligundua katika Chichen Itza ni sawa na 832 AD, wakati mwisho inayojulikana tarehe ilikuwa kumbukumbu katika Osario hekalu katika 998.
 https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEgIWZi157c39n6NzOaiOx2ESs1_wuyv4qJSUj5ZlApPTDC3uh8zTlleRGO4N4iraNySc33fYjkOM3GjZA11qFzLPhSmVSFUxnLuHDUnxZHMIQEd9CkKY8eY-vZbl6hjQXpz7-qoVfLALTGb/s1600/taj-mahal-3.jpg
​6. Taj Mahal, India
Taj Mahal ni neno kutoka Kiajemi na Kiarabu, lenye maana ya  "taji ya majumba",  ni jengo lililojengwa na mawe yenye rangi nyeupe  juu benki ya kusini ya Mto Yamuna katika mji wa India wa Agra. Ni alikuwa utakamilika katika 1632 na Mughal kaizari Shah Jahan (ilitawala 1628-1658) hadi nyumba kaburi la mke wake favorite wa watoto watatu, Mumtaz Mahal.

Ujenzi wa mausoleum ulikamilika mwaka 1643 lakini kazi aliendelea na awamu nyingine ya mradi kwa ajili ya nyongeza ya miaka kumi. Tata Taj Mahal ni kuamini yamekamilika katika ukamilifu wake katika 1653 kwa gharama inakadiriwa kuwa muda wa kuwa karibu milioni 32 rupia India, ambayo mwaka 2015 itakuwa yenye thamani ya karibu bilioni 52.8 Hindi rupia ($ milioni 827 za Marekani). Mradi wa ujenzi walioajiriwa karibu 20,000 mafundi chini ya uongozi wa bodi ya wasanifu wakiongozwa na Ustad Ahmad Lahauri. Kaburi domed jiwe ni sehemu ya tata jumuishi yenye bustani na mbili majengo nyekundu-mchanga kuzungukwa na ukuta crenellated pande tatu.

Taj Mahal ni kuonekana kwa wengi kama mfano bora wa usanifu Mughal na ni alitambua sana kama "kito cha Kiislam sanaa nchini India". Ni moja ya miundo wengi zaidi duniani sherehe na ishara ya matajiri historia ya India. Mteule UNESCO mwaka 1983, Taj Mahal huvutia baadhi ya watu milioni 3 wageni kwa mwaka. Tarehe 7 Julai 2007 ilikuwa alitangaza mmoja wa washindi saba wa New7Wonders ya Dunia (2000-2007) mpango katika Lisbon.

Jumanne, 25 Julai 2017

MWANAJALI AZIDI KUTAKATA AFRIKA KUSINI, AREJEA KATIKA KIWANGO KIZURI

Image result for MWANJALI MCHEZAJI WA SIMBA IMAGES


Beki wa kati wa Simba, Method Mwanjale ameanza kurejea katika kiwango chake kutokana na kuwa fiti.

Mwanjale yuko katika kikosi cha Simba kilichoweka kambi nchini Afrika Kusini kujiandaa na msimu mpya.

Awali, Mwanjale raia wa Zimbabwe alikuwa aachwe lakini baadaye kamati ya usajili ya Simba iliamua kumbakiza.

Beki huyo alitoa msaada mkubwa katika safu ya ulinzi ya Simba hasa mechi za mwanzo wa msimu hadi alipoumia katikati ya msimu.

Uamuzi wa Simba kumbakiza ulichagizwa na kuwa kiungo mzuri wa kuwaunganisha wachezaji na uongozi kwa kuwa ana ushawishi unaotokana na kukubalika na wachezaji wengi.

Lakini uwezo wake wa kucheza pia uliwavutia Simba kwamba anaweza kuwa na mwaka mmoja zaidi wa kucheza na kutoa msaada.


RAYON SPORTS YAKUBALI OMBI LA KUCHEZA NA SIMBA, SIKU YA SIMBA DAY




Kikosi cha Rayon Sports cha Rwanda ndicho kitakachocheza na Simba katika mechi ya Simba Day kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam.

Kawaida tamasha hilo hufanyika Agosti 8. Rayon imekubali kushiriki tamasha hilo maarufu la Simba Day ambalo hufanyika mara moja kila mwaka.

Nchini Rwanda, Rayon ndiyo timu yenye mashabiki wengi zaidi ikifuatiwa na APR ambayo inamilikiwa na jeshi.


Kwa misimu miwili iliyopita, Rayon imeonyesha kiwango kizuri kisoka na kufanikiwa zaiid ya APR.

Suala la mazingira ni kipengee muhimu, utekelezaji wa SDGs- UNEP




Uhusiano kati ya malengo ya maendeleo endelevu, SDGs na mazingira ni dhahiri na hivyo ili kufikia malengo hayo lazima suala la mazingira litiliwe maanani, amesema Naibu Mkurugenzi mtendaji wa Shirika la Umoja wa Mataifa la mpango wa mazingira UNEP Ibrahim Thiaw.
Akizungumza katika mahojiano maalum na Idhaa ya Umoja wa Mataifa, bwana Thiaw [Chow] amesema malengo yote kumi na saba yana kipengee cha suala la mazingira, kwa mfano kuhusu lengo la kwanza la kutokomeza umaskini amesema..


"Watu masikini zaidi katika nchi zinazoendelea hawana mabenki, hawana nyumba za kifahari na hawana mali kando na mashamba yao na ardhi zao wanakoishi au wanyamapori walio karibu nao, kwa hiyo tunachokitaja kama pato la taifa la watu masikini kinaweza kuzalishwa kutoka kwa mazingira na iwapo unataka kukabiliana na umasikini uliokithiri ni lazima kutilia hilo maanani."
Ameongeza kuwa kila mtu ana jukumu katika kulinda mazingira iwe ni serikali, mashirika binafsi na jamii kwa ujumla na hivyo…
 "Tungependa kukumbusha kila mtu kwamba, mabadiliko ya tabianchi ni suala la kimataifa na sio tu jambo linalokabili nchi maskini au zile za kipato cha wastani bali ni changamoto kwa kila mtu. Wakati majanga yanaibuka hamna taifa licha ya uchumi wake linaloweza kuepuka majanga na mizozo, huenda likawa na idadi ndogo ya wahanga lakini kutakuwepo na athari."

Kushambulia watu waliokimbia vita ni ukatili usiokubalika:Guterres




Vitendo vya kigaidi vya kuwalenga watu ambao tayari wameshazikimbia nyumba zao kutokana na machafuko ya Boko Haram ni ukatili usiokubalika.
Hayo yamesemwa na Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres wakati akilaani vikali mashambulizi ya kujitoa muhanga yaliyotokea jana katika kambi mbili za wakimbizi wa ndani karibu na Maiduguri , jimbo la Borno, nchini Nigeria.
Kupitia taarifa iliyotolewa na msemaji wa Umoja wa Mataifa , Guterres ametuma salamu za rambirambi kwa watu na serikali ya Nigeria kufutia vifo vilivyotokama na mashambulizi hayo, amewatakia ahuweni ya haraka majeruhi na kutoa wito wa waliohusika na ukatili huo kufikishwa mbele ya sheria.
Amesisitiza msaada wa Umoja wa Mataifa kwa serikali ya Nigeria katika mapambano dhidi ya ugaidi na machafuko ya itikadi kali kwa kuzingatia sheria za kimataifa, haki za binadamu na sheria za wakimbizi.


TRA yaanika deni la Acacia, ni sawa na 'bajeti ya miaka 13'




Mamlaka ya Mapato (TRA) imeitaka Kampuni ya Acacia kulipa zaidi ya Sh424 trilioni kutokana na ukwepaji kodi ilioufanya kuanzia mwaka 2000. Kwa kutumia bajeti ya sasa, fedha hizo ni sawa na bajeti ya Tanzania ya miaka 13.
Deni hilo, ambalo ni sawa na dola 190 bilioni za Kimarekani limetokana na hesabu zilizopigwa kwa kutumia taarifa iliyotolewa na kamati mbili zilizoundwa na Rais John Magufuli kuchunguza usafirishaji wa mchanga wa madini unaofanywa na kampuni hiyo kutoka migodi ya Bulyanhulu na Buzwagi.
Taarifa iliyotolewa jana na kampuni hiyo imekataa kulipa deni hilo kwa maelezo kwamba haijapewa ripoti ya kamati zote mbili.
“Hatuyakubali makadirio haya. Kampuni itaangaalia haki na namna zote zilizopo kuhusu suala hili,” inasema taarifa hiyo.
Kwa mujibu wa Acacia, deni hilo limeelekezwa kwa kampuni zake tanzu ambazo ni Bulyanhulu Gold Mine (BGML) inayoendesha mgodi wa Bulyanhulu, na Pangea Minerals (PML) inayosimamia mgodi wa Buzwagi.
Taarifa hiyo iliyopokelewa jana kutoka TRA inadai kodi hiyo ni kuanzia mwaka 2000 mpaka 2017 kwa BMGL na kati ya mwaka 2007 hadi 2017 kwa PML. Katika deni hilo, kodi ambayo haikulipwa ni dola40 bilioni za Kimarekani (zaidi ya Sh88 trilioni) pamoja na dola 150 bilioni (zaidi ya Sh330 trilioni) ambazo ni  faini na riba.
Bajeti ya mwaka 2017/18 ya Serikali ya Tanzania ni Sh31.7 trilioni na hivyo fedha hizo zinaweza kugharimia bajeti ya miaka 13 na miezi mitatu bila kutegemea misaada ya wahisani.
Endapo kila Mtanzania atapewa mgao kutoka kwenye fedha hizo, kati ya wananchi milioni 56 (kwa mujibu wa Benki ya Dunia) kila mmoja angepata zaidi ya Sh7.57 milioni. Fedha hizo pia ni zaidi ya mara nane ya deni la taifa ambalo ni takribani Sh51 trilioni ka sasa.
Mkurugenzi wa Elimu ya Mlipakodi wa TRA, Richard Kayombo hakuwa tayari kuzungumzia suala hilo.
“Kwa sasa siwezi kutoa maoni yoyote kwa sababu mawasiliano hufanyika kati yetu na mteja. Hata hivyo, sina waraka wowote ninaoweza kuutumia,” alisema Kayombo.
Sakata la Acacia lilianza wakati Rais John Magufuli alipozuia usafirishaji wa mchanga nje mwaka jana na baadaye Machi mwaka huu.
Makontena 277 yaliyokuwa bandarini kusubiri kupelekwa nje kwa ajili ya kuyeyushwa, yalizuiwa na baadaye Rais kuunda kamati kwa ajili ya kuchunguza kiwango cha madini kilichokuwa kwenye mchanga huo.
Siku chache baadaye, Rais aliunda kamati nyingine iliyopewa jukumu la kuangalia athari za kiuchumi ambazo nchi ilipata kutokana na kusafirisha mchanga huo nje.
Acacia inasafirisha mchanga huo nje kwa ajili ya kuuyeyusha kupata mabaki ya madini ya dhahabu na shaba ambayo yalishindikana katika hatua ya awali ya uchenjuaji ambayo hufanyika mgodini.
Acacia inadai kuwa kiwango cha dhahabu kilichomo kwenye mchanga huo ni takriban asilimia 0.3, lakini kamati iliyoundwa na Magufuli ilisema kuwa kiwango cha dhahabu ni mara kumi ya kile kilichotangazwa na wawekezaji hao kutoka Canada.
Matokeo hayo yalimfanya Rais Magufuli kutengua uteuzi wa Waziri wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo, kumsimamisha kazi mkurugenzi mkuu wa Wakala wa Ukaguzi wa Madini (TMAA) pamoja na kamishna wa madini.
Pia aliagiza wafanyakazi wa TMAA kutoendelea kufanya kazi kwenye migodi hiyo hadi hapo utakapotolewa uamuzi mwingine.
Rais pia alimuagiza Waziri wa Sheria na Katiba, Profesa Palamagamba Kabudi kuunda jopo la wanasheria kwa ajili ya kuangalia mabadiliko ya sheria ya madini na kuwasilisha bungeni mapendekezo ya mabadiliko hayo.
Tayari mabadiliko hayo yameshapitishwa na Bunge, ambayo yanaipa mamlaka Serikali kufanya mazungumzo upya na kampuni za uwekezaji kwenye madini na pia kuongeza mrabaha kutoka asilimia nne hadi sita.
Kamati ya pili iliibuka na matokeo yaliyoonyesha kuwa Tanzania imepoteza zaidi ya Sh108 trilioni kwa kusafirisha mchanga huo kwa miaka 20.
Kamati hiyo pia ilidai kuwa Acacia haijasajiliwa nchini na haina leseni ya kufanya biashara nchini na hivyo shughuli zake ni kinyume cha sheria.
Kamati hiyo pia ilinyooshea vidole wanasiasa na watumishi wa umma walioshiriki kuingia mikataba na kampuni za uwekezaji kwenye madini na pia walioshughulikia mabadiliko ya sheria ya madini ambayo yalilenga kuipunja nchi.
Hata hivyo, Acacia imekataa kuzikubali ripoti za kamati zote mbili ikisema haikushirikishwa na kwamba kamati hizo hazikuwa huru.
Acacia imekuwa ikisisitiza kuwa uchunguzi huo haukufanywa na kamati huru na hivyo kutaka iundwe kamati huru kufanya uchunguzi huo.
Pia imekuwa ikijitetea kuwa imekuwa ikitoa taarifa sahihi kuhusu kiwango cha madini kilichomo kwenye mchanga huo kuwa ni sahihi na kwamba kama matokeo ya uchunguzi wa kamati ya kwanza yangekuwa sahihi, Tanzania ingekuwa mzalishaji mkubwa wa dhahabu duniani.
Kuhusu matokeo ya kamati ya pili, Acacia imesema pia inaipinga kwa kuwa ilifanya tathmini yake kwa kuzingatia matokeo ya kamati ya kwanza, ambayo haikubaliani nayo.
Pamoja na hayo, mwenyekiti mtendaji wa Barrick Gold, ambayo ni kampuni mama ya Acacia, Profesa John Thornton (pichani) alikuja nchini kwa ndege ya kukodi kutoka Canada kwa ajili ya kuzungumza na Rais Magufuli.
Baada ya mazungumzo hayo, Rais aliwaambia waandishi wa habari kuwa Acacia imekubali kuwa ilifanya makosa na kwamba imeahidi kulipa fedha ambazo zitabainika kuwa hazikulipwa.
Alisema Serikali na kampuni hiyo zimekubaliana kuunda timu ya kufanya mazungumzo ya kutafuta muafaka wa suala hilo.
Hata hivyo, Acacia imesema haitashiriki kwenye mazungumzo hayo na badala yake Barrick ndiyo itahusika isipokuwa makubaliano yoyote yatakayofikiwa ni lazima yaridhiwe na kampuni hiyo.
Acacia pia imeshatoa notisi mahakamani kuonyesha nia yake ya kufungua kesi kupinga maamuzi hayo ya Serikali.


Ma-RC Ma-DC Watakao lia Njaa watangaziwa kiama



 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania John Magufuli amewambia Wakuu wa Mikoa na Wilaya watakao  Dhihirisha Mikoa/wilaya zao kuwa zina njaa hawafai kuwa Mkuu wa Mkoa wilaya hiyo

hayo yameelezwa leo na Rais Magufuli alipokuwa Ziarani Mkaoni Sindida ambapo ameeleza kuwa Serikali haitatoa Chakula kwa Wilaya au Mkoa utakao kuwa na Njaa na kwamba Ma-DC na ma-RC, wa sehemu husika hawatafaa kuwa kwenye nafasi hizo

 Rais Magufuli ameeleza kuwa Ma-Dc na Ma-RC wanatakiwa kuwa mstari wa mbele kuhamasisha kazi kwa wananchi

TCU yasitisha udahili kwa vyuo 19 nchini



 Tume ya Vyuo Vikuu Tanzania (TCU) imesema kuwa imefanya uhakiki wa vyuo vyote vya elimu ya juu nchini ili kuhakiki ubora wa elimu inayotolewa vyuoni hapo, ripoti ya uhakiki huo ilionyesha mapungufu kadhaa katika baadhi vyuo.

Hivyo tume imeamua kuchukua uamuzi wa kusitisha udahili wa wanafunzi wa mwaka wa kwanza kwa mwaka wa masomo 2017/18 kwa vyuo hivyo.

Aidha, Tume hiyo imevitaja vyuo hivyo kuwa ni pamoja na:
    1. Eckenforde Tanga University
    2. Jomo Kenyatta University, Arusha
    3. Kenyatta University, Arusha
    4. United African University of Tanzania
    5. International Medical and Technological University (IMTU)
    6. University of Bagamoyo
    7. Francis University College of Health and Allied Sciences
    8. Archibishop James University College
    9. Archibishop Mihayo University College
    10. Cardinal Rugambwa Memorial University College
    11. Kampala International University Dsm College
    12. Marian University College
    13. Johns University of Tanzania Msalato Centre
    14. Johns University of Tanzania, Marks Centre
    15. Joseph University College of Engineering and Technology
    16. Teofilo Kisanji University
    17. Teofilo Kisanji University Tabora Centre
    18. Tumaini University, Mbeya Centre
    19. Kilimanjaro Christian Medical University College (KCMCo)

Aidha, kutokana na mapungufu hayo katika vyuo mbalimbali imeamriwa kuwa jumla ya programu 75 kutoka vyuo 22 nchini zimesitishwa kudahili wanafunzi wa mwaka wa kwanza kwa mwaka wa masomo 2017/18.

UTAFITI: Jaribio la kinga ya HIV kwa wanawake lafanikiwa



 Watafiti nchini Marekani wanasema kuwa jaribio ambalo vijana wa Marekani walitumia mpira wa mviringo kujilinda na virusi vya HIV limefanikiwa.


Utafiti zaidi sasa utafanyiwa vijana barani Afrika.
Wasichana walitumia mviringo wa plastiki uliowekwa dawa za kujilinda na ukimwi , ambao hulibadilishwa kila mwezi baada ya kipindi cha miezi sita.
Ni mojawapo ya mipango ya kutengeza kifaa ambacho wanawake watatumia kujilinda dhidi ya maambukizi ya HIV ili wasiweze kuwategemea wanaume kuvaa mipira ya kondomu.
Wakiripoti ugunduzi huo mpya kuhusu virusi vya HIV mjini Paris, watafiti walisema kuwa wanafurahi kwamba wasichana hao walitumia mvirongo huo na kusema kuwa wameupenda.
Wanawake na wasichana walio na kati ya umri wa miaka 15-24 wanadaiwa kuwa moja kwa tano ya visa vyote vya maambukizi ya HIV duniani.
Takriban wanawake 1000 huambukizwa virusi kila siku katika Afrika ya jangwa la sahara.

Kijana Mdogo wa Kiafrika aushanga Ulimwengu kwa Kugundua Sachi Injini inayoitishia google



 Kijana wa Chuo Kikuu cha Ghana Gabriel Opare mwenye Umri wa Miaka 19 uashangaza ulimwengu kwa kugundua Sachi injini ambayo inauwezo unaofafania na Google.

Kijana huyo mdogo Raia wa Ghana ambaye anasomea Shahada ya Pili ya Sosholojia  kwenye chuo hicho amegundua Searchi Ingene hiyo yenye jina la 'Mudclo'

Yanga yamsajili golikipa wa Serengeti Boys



 Klabu ya Yanga yenye maskani yake mitaa ya Jangwani jijini Dar es salaam, imefanikiwa kunasa saini ya Golikipa wa timu ya taifa ya vijana chini ya umri wa miaka 17, Ramadhani Kabwili.


Yanga SC wametoa taarifa hizo kupitia kwenye mitandao yake ya kijamii kuwa amesaini kwa kandarasi ya miaka mitano.
“Ramadhani Kabwili,golikipa wa timu ya Taifa ya Vijana ya Tanzania (Serengeti Boys) amejiunga na Yanga kwa mkataba wa miaka mitano”,imesomeka ripoti iliyotolewa na Yanga.
Klabu ya Yanga ni miongoni mwa klabu zilizosajili wachezaji wengi msimu hii ni kutokana na nguvu ya pesa walizopata baada ya udhamini wa Kampuni ya kubashiri ya SportPesa.

Jumamosi, 22 Julai 2017

Magoli ya Mbwana Samatta na Wayne Rooney timu zao zilipokutana leo



 
Jumamosi ya July 22 2017 mtanzania Mbwana Samatta alipata nafasi ya kuiongoza safu ya ushambuliaji ya timu yake ya KRC Genk ya Ubelgiji katika mchezo wa kirafiki dhidi ya Everton FC inayodhaminiwa na kampuni ya michezo ya kubashiri ya SportPesa.




Mchezo wa Everton dhidi ya KRC Genk uliyochezwa nchini Ubelgiji katika uwanja wa Luminus Arena, umempa nafasi nahodha wa Tanzania Mbwana Samatta kuonesha uwezo wake dhidi ya Everton ambayo ni miongoni mwa vilabu saba England ambavyo havijawahi kushuka daraja toka kuanzishwa kwa mfumo wa Ligi Kuu England 1992.


Mbwana Samatta ambaye ndio mshambuliaji tegemeo wa KRC Genk baada ya kuumia kwa mgiriki Nikolaos Karelis aliifungia KRC Genk goli la kusawazisha dakika ya 55, hiyo ni baada ya Wayne Rooney kuifungia Everton goli la kwanza dakika ya 45 kwa kutumia vyema assist ya Sandro Ramirez.



Rais Magufuli Atishia Kuifunga Migodi ya Madini Endapo Barrick Watachelewa Katika Mazungumzo




Wakati Kampuni ya Acacia ikisema imepoteza mapato ya Sh385 bilioni katika kipindi cha miezi sita kutokana na kuzuiwa kusafirisha mchanga wa madini nje, Rais John Magufuli ametishia kufunga migodi ya wawekezaji iwapo hawatajitokeza mapema katika mazungumzo.

Rais Magufuli amesema hayo takriban wiki moja baada ya kudokeza kuwa Serikali ingeanza mazungumzo “na waliokuwa wanatuibia” mapema wiki hii.

Jana, Rais Magufuli alisema Serikali haitasita kufunga migodi yote ya madini ambayo wamiliki walitakiwa kufanya mazungumzo na Serikali kuhusu ulipaji kodi.

 Akizungumza katika ziara yake mkoani Kigoma ambako alizindua Barabara ya Kibondo-Nyakanazi, Rais Magufuli alisema Taifa linapoteza fedha nyingi kutokana na upotevu wa madini.

“Ni matrilioni ya fedha ambayo yanapotea, na sasa hivi tumewaita tufanye mazungumzo lakini wakichelewachelewa nitafunga migodi yote,” alisema.

Alisema ni bora migodi hiyo ikakabidhiwa kwa Watanzania kuliko wawekezaji ambao hawalipi kodi.

Rais Magafuli alipiga marufuku usafirishaji wa mchanga huo nje ya nchi, na baadaye kuunda kamati mbili; moja ya kuchunguza kiwango cha madini kilichokuwa katika makontena 277 yaliyozuiwa Bandari ya Dar es Salaam na nyingine kuangalia athari za kiuchumi na kisheria tangu mchanga huo uanze kusafirishwa mwaka 1998.

Ripoti ya kamati ya kwanza ilisema kuwa Acacia, inayoendesha migodi ya Bulyanhulu na Buzwagi, haikusema ukweli kuhusu kiwango cha dhahabu, ikidai kuwa imebaini mchanga huo una madini hayo mara kumi ya kiwango kilichotangazwa na wawekezaji hao.

Ripoti ya kamati ya pili ilionyesha kuwa katika kipindi cha miaka 20, Serikali ilipoteza zaidi ya Sh108 trilioni na kwamba Acacia haijasajiliwa nchini na hivyo inafanya kazi kinyume cha sheria.

Hata hivyo, Acacia haijakubaliana na matokeo ya ripoti hizo, ikisema inataka uchunguzi wa kamati huru na kwamba kama matokeo hayo ni ya kweli, Tanzania ingekuwa moja ya nchi tatu zinazozalisha dhahabu kwa wingi duniani.

Jana, Acacia ilisema imepoteza Sh385 bilioni katika kipindi cha miezi sita. Acacia pia imesema endapo hali itaendelea kuwa hivyo, italazimika kuufunga mgodi wake wa Bulyanhulu na kusitisha mikataba ya ajira kwa wafanyakazi.

Hata hivyo, katika taarifa yake ya jana inayozungumzia kipindi cha Januari mpaka Juni, Acacia imesema  imepata changamoto kubwa katika utendaji wake nchini.

 “Nusu (ya kwanza), imetupa changamoto kubwa katika shughuli zetu Tanzania baada ya kuwekewa zuio la usafirishaji wa makinikia kuanzia Machi,” alisema Mkurugenzi Mtendaji wa Acacia, Brad Gordon. “Mapato yetu yameshuka mpaka dola 175 milioni za Kimarekani kutoka dola 318 milioni tulizotarajia.”

Licha ya kushindwa kuingiza Dola 175 milioni za Marekani (zaidi ya Sh385 bilioni) zilizotarajiwa, Acacia inasema imelipa dola51 milioni za Kodi ya Ongezeko la Thamani (VAT), ambazo ni zaidi ya Sh112.2 bilioni.

Ili kulinda masilahi ya wanahisa wake, Acacia imewasilisha notisi kwa msuluhishi kwa ajili ya migodi ya Bulyanhulu na Buzwagi ambayo ndiyo inayozalisha mchanga wa madini kwa sasa.

Buzwagi imekuwa ikisafirisha mchanga huo kwenda nje ya nchi kwa ajili ya kuuyeyusha ili kupata mabaki ya dhahabu, shaba na fedha kutokana na teknolojia hiyo kutokuwapo mgodini.

Hatua ya kwanza ya kuchenjua dhahabu hufanyika mgodini na mchanga unaosalia ndio unaosafirishwa nje. Acacia imekuwa ikieleza kuwa mchanga huo una asilimia 0.02 ya dhahabu wakati shaba ni asilimia 10.

Acacia pia imekanusha taarifa ya kuwapo amri ya kutakiwa kuondoka nchini kwa mmoja wa wafanyakazi wake wa kigeni.

“Hatuna taarifa za kutolewa kwa amri hiyo kwa mfanyakazi wetu yeyote wa kigeni aliyepo Tanzania. Tunashirikiana vizuri na Serikali kwenye mazungumzo yanayoendelea na hakuna aliyekamatwa habari hiyo si sahihi,” inasema taarifa hiyo.

Tandika: Daladala yagonga treni, wawili wafariki dunia




 Watu wawili wamekufa na wengine kadhaa wamejeruhiwa katika ajali iliyotokea leo asubuhi ikihusisha gari ya abiria aina ya coaster kukigonga kichwa cha treni maeneo ya Yombo Devis Kona.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Temeke, Gilles Muroto amesema watu wawili wamefariki dunia akiwamo mwanamke mmoja na mwanaume mmoja ambaye ni kondakta wa daladala hiyo.
Muroto amesema mbali na watu wawili kufariki pia kuna majeruhi 36 wanne kati yao wakiwa mahututi.
Amesema majeruhi mahututi ni wanawake watatu na mwanaume mmoja.
“Majeruhi wite wanapatiwa matibabu katika hospitali ya Temeke na miongoni mwa majeruhi hao wanne wapo katika hali mbaya”amesema Kamanda Muroto.

Mfanyabiashara wa Madini Kilimanjaro aliyehukumiwa maisha jela



 Moja ya habari ambayo imekuwa gumzo ni hii inayotokea Kilimanjaro ambako Mahakama ya Hakimu Mkazi Mkoa wa Kilimanjaro imemhukumu kifungo cha maisha jela mfanyabiashara wa Madini Benedict Kimario kwa makosa mawili ya ubakaji na ulawiti.

Ijumaa, 21 Julai 2017

Tundu Lissu agoma Kupimwa mkojo





 Tundu Lissu(Mb) amekataa kupimwa mkojo baada ya kufikishwa kwa Mkemia  
Asema kipimo hicho hakihusiani na tuhuma za uchochezi

Taarifa za awali ziliarifu kuwa, Mkurugenzi wa Itifaki, Mawasiliano na Mambo ya Nje wa Chadema, John Mrema amesema baada ya Tundu Lissu kutolewa Kituo cha Polisi cha Kati leo mchana, amefikishwa kwa Mkemia Mkuu wa Serikali na kupimwa mkojo.

Mapema asubuhi, mawakili akiwamo Fatma Karume walizuiliwa kuonana naye huku Jeshi la Polisi likisema litaendelea kumshikilia hadi uchunguzi utakapokamilika.

Mbunge huyo wa Singida Mashariki amekamatwa Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere (JNIA), akielekea Kigali, Rwanda kwenye kikao cha Halmashauri ya EALS kilichoanza jana.

"Kabla ya kuelekea nyumbani kwake Tegeta, wamempeleka kwa mkemia mkuu na ameshapimwa mkojo, sasa sijui ni kitu gani wanachunguza, kwa sasa wameshaelekea nyumbani kwake kwa ajili ya kumpekua,"amesema Mrema.

Licha ya kulala rumande hakuna aliyeruhusiwa kuingia na kumuona Tundu Lissu wakiwamo wanasheria wake. Mbali na Fatma, wengine waliokuwapo ni Peter Kibatala na Frederick Kihwelo.

Agosti 8 ni Yanga Vs Singida United




Ikiwa ni maandalizi ya kujiandaa na Ligi Kuu Bara, Yanga itaivaa Singida United katika mechi ya kirafiki itakayopigwa Agosti 8 kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar.
Tayari uongozi wa Singida United umethibitisha kuwepo kwa mechi hiyo kwenye Uwanja wa Taifa.
Timu zote mbili zinadhaminiwa na kampuni ya michezo ya kubashiri ya SportPesa.


UPDATE: Polisi wameondoka na Tundu Lissu kituoni




Jana jioni Mwanasheria wa CHADEMA na Mbunge kutokea mkoa wa Singida Tundu Lissu alikamatwa na Polisi uwanja wa ndege Dar es salaam akiwa anaelekea Rwanda ambapo alichukuliwa na kuendelea kushikiliwa na Polisi hadi leo.
Taarifa ambayo imetolewa mchana huu na Afisa habari wa CHADEMA ni kwamba Polisi wamemchukua  Tundu Lissu kutoka kituo kikuu cha polisi na wanaelekea nyumbani kwake kwa ajili ya kupekuliwa ambapo taarifa hiyo ya CHADEMA imesema hadi muda inapotolewa taarifa hii haujajulikana upekuzi huo unahusu kitu gani.
chanzo milrad blog .

Nitawanyoosha Yanga kulinda heshima yangu- Kichuya

Tokeo la picha la kichuya

 Mshambuliaji wa klabu ya Simba, Shiza Kichuya ametamba kuendeleza ubabe dhidi ya Yanga kwa kutupia magoli kama msimu uliopita ili kulinda heshima yake.


Kichuya amesema hayo baada ya mashabiki wengi wa Klabu ya Yanga kuonekana wenye hofu naye hususani katika mchezo unaokuja wa ngao ya jamii utakaochezwa katika dimba la uwanja wa taifa.
Sipendi kuwa mwongeaji sana, ila napenda kufanya sana kazi uwanjani, naendelea kujipanga na naahidi kulinda heshima yangu, hata kama sitafunga lakini lazima nitoe pasi ya bao ili kuibeba Simba timu inayonifanya niishi mjini,” amesema Kichuya kwenye mahojiano yake na Gazeti la Mwanaspoti.
Kichuya ambaye yupo nchini Rwanda na timu ya taifa ya Tanzania, Taifa Stars kwa ajili ya mechi ya marudiano ya kufuzu michuano ya CHAN, alifunga bao la kusawazisha katika mechi iliyojaa utata ya Oktoba Mosi, 2016 dhidi ya Simba, kabla ya kufunga bao la ushindi mechi ya marudiano na kuwazima kabisa Yanga kwenye mechi zote mbili za msimu uliopita.
Simba na Yanga zitavaana Agosti 23 mwaka huu kwenye mchezo wa ngao ya jamii utakaopigwa uwanja wa Taifa, jijini Dare se salaam.