Ijumaa, 28 Julai 2017

Harbinder Seth na Rugemarila wamefikishwa Mahakamani tena leo




Leo July 28, 2017 Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu imeamuru mmiliki wa Kampuni ya kufua umeme ya IPTL, Harbinder  Singh Sethi apewe matibabu kutokana na matatizo ya kiafya yanayomkabili.
Hayo yameelezwa na Hakimu Mkazi Mkuu, Huruma Shaidi baada ya Seth kudai anahitaji kuwa na nguvu ambayo haitopatikana kama Afya yake itakuwa dhaifu, hivyo ameomba apatiwe matibabu.
Kutokana na kuwa afya ni muhimu kwa binaadam, Mahakama imetoa kibali ili mshtakiwa huyo apate matibabu na keshi imeahirishwa hadi August 3, 2017 k
wa ajili ya kutajwa.
 

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni