Ijumaa, 21 Julai 2017

Nitawanyoosha Yanga kulinda heshima yangu- Kichuya

Tokeo la picha la kichuya

 Mshambuliaji wa klabu ya Simba, Shiza Kichuya ametamba kuendeleza ubabe dhidi ya Yanga kwa kutupia magoli kama msimu uliopita ili kulinda heshima yake.


Kichuya amesema hayo baada ya mashabiki wengi wa Klabu ya Yanga kuonekana wenye hofu naye hususani katika mchezo unaokuja wa ngao ya jamii utakaochezwa katika dimba la uwanja wa taifa.
Sipendi kuwa mwongeaji sana, ila napenda kufanya sana kazi uwanjani, naendelea kujipanga na naahidi kulinda heshima yangu, hata kama sitafunga lakini lazima nitoe pasi ya bao ili kuibeba Simba timu inayonifanya niishi mjini,” amesema Kichuya kwenye mahojiano yake na Gazeti la Mwanaspoti.
Kichuya ambaye yupo nchini Rwanda na timu ya taifa ya Tanzania, Taifa Stars kwa ajili ya mechi ya marudiano ya kufuzu michuano ya CHAN, alifunga bao la kusawazisha katika mechi iliyojaa utata ya Oktoba Mosi, 2016 dhidi ya Simba, kabla ya kufunga bao la ushindi mechi ya marudiano na kuwazima kabisa Yanga kwenye mechi zote mbili za msimu uliopita.
Simba na Yanga zitavaana Agosti 23 mwaka huu kwenye mchezo wa ngao ya jamii utakaopigwa uwanja wa Taifa, jijini Dare se salaam.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni