Jumanne, 25 Julai 2017

Kushambulia watu waliokimbia vita ni ukatili usiokubalika:Guterres




Vitendo vya kigaidi vya kuwalenga watu ambao tayari wameshazikimbia nyumba zao kutokana na machafuko ya Boko Haram ni ukatili usiokubalika.
Hayo yamesemwa na Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres wakati akilaani vikali mashambulizi ya kujitoa muhanga yaliyotokea jana katika kambi mbili za wakimbizi wa ndani karibu na Maiduguri , jimbo la Borno, nchini Nigeria.
Kupitia taarifa iliyotolewa na msemaji wa Umoja wa Mataifa , Guterres ametuma salamu za rambirambi kwa watu na serikali ya Nigeria kufutia vifo vilivyotokama na mashambulizi hayo, amewatakia ahuweni ya haraka majeruhi na kutoa wito wa waliohusika na ukatili huo kufikishwa mbele ya sheria.
Amesisitiza msaada wa Umoja wa Mataifa kwa serikali ya Nigeria katika mapambano dhidi ya ugaidi na machafuko ya itikadi kali kwa kuzingatia sheria za kimataifa, haki za binadamu na sheria za wakimbizi.


Hakuna maoni:

Chapisha Maoni