Jumanne, 25 Julai 2017

Suala la mazingira ni kipengee muhimu, utekelezaji wa SDGs- UNEP




Uhusiano kati ya malengo ya maendeleo endelevu, SDGs na mazingira ni dhahiri na hivyo ili kufikia malengo hayo lazima suala la mazingira litiliwe maanani, amesema Naibu Mkurugenzi mtendaji wa Shirika la Umoja wa Mataifa la mpango wa mazingira UNEP Ibrahim Thiaw.
Akizungumza katika mahojiano maalum na Idhaa ya Umoja wa Mataifa, bwana Thiaw [Chow] amesema malengo yote kumi na saba yana kipengee cha suala la mazingira, kwa mfano kuhusu lengo la kwanza la kutokomeza umaskini amesema..


"Watu masikini zaidi katika nchi zinazoendelea hawana mabenki, hawana nyumba za kifahari na hawana mali kando na mashamba yao na ardhi zao wanakoishi au wanyamapori walio karibu nao, kwa hiyo tunachokitaja kama pato la taifa la watu masikini kinaweza kuzalishwa kutoka kwa mazingira na iwapo unataka kukabiliana na umasikini uliokithiri ni lazima kutilia hilo maanani."
Ameongeza kuwa kila mtu ana jukumu katika kulinda mazingira iwe ni serikali, mashirika binafsi na jamii kwa ujumla na hivyo…
 "Tungependa kukumbusha kila mtu kwamba, mabadiliko ya tabianchi ni suala la kimataifa na sio tu jambo linalokabili nchi maskini au zile za kipato cha wastani bali ni changamoto kwa kila mtu. Wakati majanga yanaibuka hamna taifa licha ya uchumi wake linaloweza kuepuka majanga na mizozo, huenda likawa na idadi ndogo ya wahanga lakini kutakuwepo na athari."

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni