Leo July
28, 201 7 Mahakama ya Rufaa imeitupa rufani iliyofunguliwa na wapigakura
wa Jimbo la Bunda kwenye kesi ya kupinga matokeo ya uchaguzi yaliyompa
ushindi Mbunge wa Jimbo hilo, Ester Bulaya.
Wapigakura
hao ambao wanampigania aliyekuwa Waziri wa Chakula, Kilimo na Ushirika
na mgombea Ubunge wa CCM Jimbo la Bunda Mjini, Stephen Wasira, ni Magambo Masato, Matwiga Matwiga, Janes Ezekiel na Ascetic Malagila.
Uamuzi huo
umetolewa na Naibu Msajili wa Mahakama hiyo, Elizabeth Mkwizu ambaye
amesema, upande wa walalamikaji uliwasilisha hoja 10 za kupinga ushindi
wa Bulaya, lakini hoja hizo hazikuwa na mashiko, hivyo zinatupiliwa
mbali.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni