mwana wa liganga blog ni blog ya kutoa taarifa, matukio, yaliyotokea katika ulimwengu hususani katika nchi yaTanzania blog hii inasimamiwa na mwandishi wa habari kitaaluma bwana Deus Thomas liganga.lengo ni kutoa taarifa kwa umma,kwa maendeleo ya taifa na Dunia kwa ujumla kwa mawasiliano kuhusu mtangazo, habari, wasiliana nasi 0659944423,deusliganga@yahoo.com,mzeeliganga@gmail.com
Ijumaa, 28 Julai 2017
Mwanariadha, Francis Damian aitoa kimasomaso Tanzania Jumuia ya Madola
Timu ya taifa ya Tanzania ya mchezo wa riadha ya vijana walio na umri chini ya miaka 17 imerejea kwa kishindo leo baada ya kutwaa medali ya shaba ya michuano ya sita ya dunia ya vijana ya Jumuia ya Madola (Bahamas 2017 Commonwealth Youth Games) yaliyomalizika hivi karibuni huko nchini India.
Mwanariadha wa Tanzania, Francis Damian amefanikiwa kushika nafasi ya tatu katika mashindano hayo na kupata medali ya shaba kwenye mbio hizo kwa upande wa wavulana baada ya kukimbia umbali wa mita 3000 akitumia muda wa 8.37.51 wakipishana kwa sekunde 13.55 na mshindi wa kwanza Mkenya na sekunde 2.36 kwa mshindi wa nafasi ya pili ambaye ni raia wa Canada.
Kwa kutwaa medali hiyo, Damasi Francis ameiwezesha Tanzania kushika nafasi 19 kwenye ushindi wa jumla wa riadha nakufungana na Botswana, Cyprus, pamoja na Afrika Kusini.
Na kufanikiwa kushika nafasi ya 31 kwa ushindi wa jumla wa michezo yote na kufungana na Nchi za Grenada,Namibia na Rwanda.
Katibu mkuu wa wizara ya Habari , Utamaduni ,Sanaa na Michezo, Elisante Ole Gabriel ameongoza mapokezi ya viongozi na wachezaji hao waliowasili katika uwanja wa ndege wa kimataifa wa Mwl Julius k . Nyerere hii leo.
Jisajili kwenye:
Chapisha Maoni (Atom)
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni