Jumamosi, 29 Julai 2017

Neno la Okwi kwa Mashabiki wa Simba



 Mshambuliaji wa kimataifa wa Simba kutoka Uganda, Emmanuel Okwi, ametua kambini Afrika Kusini jana na kuwaambia mashabiki wa timu hiyo wajiandae kuona "vitu vyake" katika mechi ya kirafiki dhidi ya Rayon FC itakayofanyika Agosti 8 (Simba Day).


Okwi amewaambia mashabiki na wanachama wa Simba wawe watulivu, amejiandaa kuwapa kile wanachokitarajia kutoka kwake na anafahamu vizuri ndoto za klabu hiyo yenye makao makuu yake Mtaa wa Msimbazi, Kariakoo jijini.

"Nitakuwa Dar es Salaam siku ya Simba Day, najua watu wanahamu ya kuniona, mashabiki wawe watulivu," alisema mshambuliaji huyo

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni