Jumapili, 25 Machi 2018

Breaking News: Jokate apigwa chini UVCCM

Kamati ya Utekelezaji ya Umoja wa Vijana wa CCM iliyokutana kwa dharura mchana huu chini ya Mwenyekiti wa Umoja wa Vijana wa CCM Kheir Denis Jemes imetengua uteuzi wa Kaimu Katibu wa Hamasa na Chipukizi UVCCM Taifa Jokate  U. Mwengelo kuanzia leo

Taarifa hiyo iliyotolewa kupitia mtandao wa twitter wa UVCCM imesema kuwa Jokate Mwegelo ametenguliwa katika nafasi hiyo ambapo amehudumu katika nafasi hiyo kwa takribani miezi 11 toka amelipoteuliwa April 2017.

Kikao hicho kilichomtengua Jokate kiliendeshwa na Mwenyekiti wa Umoja wa Vijana wa Chama cha Mapinduzi Ndg.  Kheri Denis James (MCC) katika ukumbi wa secretariet  White house Mjini Dodoma lakini bado hawajaweka wazi sababu zilizopelekea kutengua uteuzi wa Jokate Mwegelo.

Maagizo ya Rais Magufuli kwa Vyombo vya Dola baada ya ajali kuua watu 26

Rais Magufuli ametoa pole kufuatia vifo vya watu 26 vilivyotokea Wilayani Mkuranga, Pwani baada ya Hiace kugongana na Lori. Amevitaka vyombo vinavyoshughulikia usalama barabarani kuchunguza chanzo cha ajali hiyo na kuchukua hatua stahiki.
“Nimesikitishwa sana na taarifa ya vifo vya watu 26 waliopoteza maisha katika ajali ya barabarani iliyotokea huko Mkuranga Mkoani Pwani, tumepoteza idadi kubwa ya Watanzania wenzetu na nguvu kazi ya Taifa.” -JPM

Watu 26 wamefariki katika ajali mkoani Pwani

Usiku wa kuamkia leo March 25, 2018 Watu 26 wamefariki dunia na wengine 10 kujeruhiwa baada ya Hiace iliyokuwa ikitokea DSM kwenda Mkuranga Pwani, kugongana na lori lililokuwa likitokea Mtwara kuelekea DSM.
Akizungumza na blog hiiKaimu kamanda wa Polisi Kanda Maalumu ya Kibiti, Mohamed Likwata amethibitisha  kutokea ajali hiyo na kwamba majeruhi wote wamepelekwa katika Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH) Dar es Salaam

Jumamosi, 17 Machi 2018

#CafCC Mpira umemalizika kwa suluhu nchini Misri. Al Masry 0-0 Simba SC. Simba wanatupwa nje ya michuano hiyo kutokana na matokeo ya sare ya mabao 2-2 iliyopatikana katika mchezo wa kwanza uliopigwa Machi 7, 2018 jijini Dar es Salaam.

No automatic alt text available.

Dakika ya 80: #CafCC Al Masry 0-0 Simba SC.

Dakika ya 60: #CafCC Al Masry 0-0 Simba SC.

Image may contain: text

Mapumziko: #CafCC Al Masry 0-0 Simba SC

No automatic alt text available.

Dakika ya 30: #LaLiga Real Sociedad 1-0 Getafe.

Image may contain: text

Dakika ya 10: #CafCC Al Masry 0-0 Simba SC.

Image may contain: text

Dakika ya 65': #CafCL Township Rollers 0-0 Yanga SC.

No automatic alt text available.

Rais Khama: “Trump anachochea Ujangili Afrika”

Rais anayemaliza muda wake wa nchini Botswana Ian Khama amemshukia Rais wa Marekani Donald Trump kuwa anahimiza shughuli za ujangili Afrika.
Ameyasema hayo akiwa anafanyiwa mahojiano na Shirika la Utangazaji la BBC katika Mkutano wa Masuala ya Kupinga Ujangili (Anti-poaching Summit) nchini Botswana ikiwa ni wiki mbili kabla ya kuachia madaraka rasmi.
Rais Khama ameeleza kuwa hiyo ni kutokana na Rais Trump kukataa marufuku ya kuingiza nchini Marekani nyara za uwindaji kutoka Bara la Afrika.
“Tatizo sio mtazamo wa Trump kwenye suala zima la wanyamapori tu bali hata mtazamo wake kwa sayari nzima. Serikali yake ilishakataza kuingiza nchini nyara hizo, yeye kukataa marufuku hiyo ni kuchochea ujangili.” – Ian Khama

Mapumziko: #CafCL Township Rollers 0-0 Yanga SC.

Madaktari wamchoma mtoto sindano kichwani kimakosa chaanza kuoza



Leo March 17, 2018 stori ninayokusogezea ni kuhusu matukio ya kutokuwa makini katika idara ya afya hasa kwa madaktari yanazidi kuzua wasiwasi kwa wananchi nchini Kenya, tukio lililotokea siku za hivi karibuni  ni la mtoto kuchomwa dawa isiyofaa na kumfanya aanze kuoza kichwa.
Tukio hili limefanyika katika hospitali ya Malava General Hospital katika jimbo la Kakamega na linatokea huku kukiwa na kesi dhidi ya Madaktari wa hospital ya Kenyatta inaendelea baada ya Daktari kumfanyia upasuaji mgonjwa asiyestahili. 
Mtoto huyo aliyejulikana kwa  jina Clinton Luchivya alikuwa amepelekwa katika hospitali hiyo baada ya kuwa mgonjwa na madaktari kumchoma kichwani baada ya kukosa mshipa wa kumwekea dawa.
Kulingana na mama wa mtoto huyo, mwanae alikuwa na ugonjwa wa Malaria kabla ya kupokea matibabu katika hospitali hiyo.  Alisema kuwa mwanae alikuwa ameanza kubadilika badilika kabla ya kufahamu kuwa kichwa chake kinaoza.

‘Nabii Shillah anaegawa Pesa’ afunguka chanzo cha utajiri, amtaja TB Joshua, Masanja

Baba alieshtakiwa Polisi na Mwanae azungumzia kifo cha Mama Anthony, watoto 20

Soma na hizi

Tupia Comments

Advertisement

RC Makonda atoa kibali cha kuruhusu wasanii kurekodi Video na Movie eneo lolote wanalotaka


Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Mhe. Paul Makonda amepiga marufuku baadhi ya watendaji wanaozuia Wasanii kurekodi Video za Nyimbo au Movie kwenye mandhari (location) mbalimbali za jiji hilo kwakuwa   linalorudisha nyuma Utalii.

Haiwezekani msanii akitaka kurekodi Video au Movie kwenye mitaro ya maji machafu ambayo inatoa taswira mbaya kwa jiji letu hasumbuliwi vibali lakini akirekodi kwenye Hotel, Majengo Marefu, fukwe au kwenye mazingira mazuri anasumbuliwa kibali,  hili haliwezekani, kuanzia sasa wasanii mtarekodi Video Location yoyote mnayotaka isipokuwa Ikulu, Mahakama, Maeneo ya jeshi na vituo vya polisi ambapo panahitaji vibali maalumu* Alisema RC Makonda.


Waarabu waigomea Azam Tv kurusha mchezo wa Al Masry dhidi ya Simba

Mchezo wa Kombe la Shirikisho Afrika kati ya Al Masry SC dhidi ya Simba Sc hautorushwa hewani na kituo chochote cha Runinga.

Awali kulikuwa na matarajio ya mechi kuoneshwa na kituo cha Azam TV baada ya kutangaza kurusha mechi ya Township Rollers dhidi ya Yanga.

Kwa mujibu wa Afisa Habari wa Simba, Haji Manara, amesema uongozi wa Al Masry umeigomea Azam TV kurusha mechi hiyo itakayoanza saa 2:30 usiku ambapo sababu hazijajulikana.

Teknolojia iliyothibitishwa kutumika World Cup 2018 Urusi

Shirikisho la soka Ulimwenguni FIFA leo limetangaza rasmi taarifa maalum kuhusiana na teknolojia mpya ya kuwasaidia waamuzi kuwa itatumika katika fainali za Kombe la Dunia 2018 nchini Urusi.
Teknolojia ya VAR inayotumika kuwasaidia waamuzi kuangalia replay na kufanya maamuzi yaliyokuwa sahihi, tayari ilikuwa imeshakubalika kutumika Africa katika mchezo wa CAF Super Cup na sasa FIFA wamethibitisha kuwa teknolojia hiyo itatumika katika game za World Cup  2018.

Rais wa FIFA Gianni Infantino amethibitisha taarifa hizo wakati wa kikao cha FIFA kilichofanyika Bogota Colombia “Tunatakiwa tuishi kwa kuangalia nyakati, tunataka kuwapa waamuzi vifaa ambavyo vitawasaidia kufanya maamuzi sahihi katika Kombe la Dunia nchini Urusi”

Urusi yamfukuza Balozi wa Uingereza na wengine 22 ‘kujibu mapigo’….kisa?

Kutoka nchini Urusi leo March 17, 2018 inaelezwa kuwa serikali ya nchi hiyo inatarajia kuwafukuza wanadiplomasia 23 wa kutoka nchini Uingereza ambao walikuwa wakifanya kazi nchini humo Urusi.
Inaelezwa kuwa uamuzi huo wa kufukuza wanadiplomasia hao utatekelezwa ndani ya kipindi cha wiki moja na hii ni kutokana na Uingereza kufukuza Wanadiplomasia 23 wa Urusi waliokuwa nchi Uingereza.
Suala hili linakuja baada ya tukio la March 4, 2018 ambapo Mpelelezi wa zamani wa Urusi Sergei Skripal alikutwa na mwanaye Yulia wako kwenye hali mbaya baada ya kupewa sumu ya kemikali na watu wasiojulikana nyumbani kwao Salisbury England.
Kwa mujibu wa Waziri Mkuu wa Uingereza Theresa May, wanaamini tukio hilo limefanywa na watu wa Urusi na hivyo kuamua kuwafukuza wanadiplomasia hao 23 wa Urusi nchini humo Uingereza.
Kutokana na hilo, Urusi imejibu mapigo hayo. Skripal na mwanaye huyo Yulia bado wako hospitalini wakipatiwa matibabu.

Kikosi cha Yanga dhidi ya Township Rollers

Kikosi cha Yanga kitakachoanza dhidi ya Township Rollers leo

1. Youthe Rostand
2. Juma Abdul
3. Gadiel Michael
4. Vicent Andrew
5. Kelvin Yondani
6. Said Juma Makapu
7. Yusuph Mhilu
8. Papy Tshishimbi
9. Obrey Chirwa
10. Pius Buswita
11. Thaban Kamusoko

Kikosi cha akiba

12. Ramadhani Kabwili
13. Abdalah Shaibu
14. Nadir Haroub
15. Raphael Daudi
17. Geofrey Mwashiuya
18. Ibrahim Ajibu
19. Juma Mahadhi

Waziri Mwakyembe amlilia mpiga picha wa ITV, Evarist Ottaro

Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Dk. Harrison Mwakyembe kilichotokea Machi 16, mwaka huu katika Hospitali ya Taifa Muhimbili jijini Dar Es Salaam.

Waziri Mwakyembe kupitia taarifa yake aliyoitoa kwa vyombo vya habari ameeleza kupokea kwa masikitiko kifo cha mpiga picha huyo Mkongwe wa ITV.
Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Dk. Harrison Mwakyembe amepokea kwa masikitiko taarifa ya kifo cha Mpiga Picha mkongwe Bw. Evarist Ottaro kilichotokea jana tarehe 16 Machi, 2018 katika Hospitali ya Taifa Muhimbili jijini Dar Es Salaam.
Dkt. Mwakyembe ameeleza kuwa kifo cha Bw. Ottaro kimeipokonya tasnia ya Habari mmoja wa Wapiga Picha mahiri waliokuwa tegemeo kubwa la maendeleo ya tasnia hiyo nchini.
Dkt. Mwakyembe ametoa pole kwa familia, uongozi wa Kituo cha Televisheni cha ITV, ndugu, jamaa, marafiki na wanahabari wote nchini na kuwaombea Mungu awape faraja katika kipindi hiki kigumu cha msiba.
Wakati wa uhai wake Bw. Ottaro amewahi kufanya kazi na vituo vya Televisheni vya Channel Ten na DTV kabla ya kuhamia katika kituo cha Televisheni cha ITV ambapo amefanya kazi kwa miaka kumi na saba hadi alipofikwa na umauti.
Imetolewa na:
Lorietha Laurence
Kaimu Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano Serikalini
Wizara ya Habari,Utamaduni,Sanaa na Michezo.
17/03/2018.

Kikosi Cha Simba kitakachocheza dhidi ya Al Masry

Mrisho Mpoto akoshwa na programu ya umilikishaji ardhi ya Mhe. Lukuvi Morogoro

Msanii wa muziki wa asili, Mrisho Mpoto ambaye amekuwa kioo cha jamii kwa muda mrefu kutokana na kutoa nyimbo za kijamii zenye kuwataka wananchi kuwa wazalendo kwa kufanya kazi kwa bidii ili kujipatia kipato cha halali, kukemea rushwa na uonevu, Ijuma hii amefurahishwa na Programu ya Umilikishaji Ardhi (Land Tenure Support Programme – LTSP).

Mhe. Lukuvi akiwa kwenye mradi huo
Programu hiyo ambayo inatakelezwa katika Wilaya za Kilombero, Ulanga na Malinyi mkoani Morogoro chini ya Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi chini ya Waziri wake, Mhe. William Lukuvi  ili kukabiliana na migogoro ya ardhi ambayo imekuwa ikiibuka katika maeneo mbalimbali nchini Tanzania.
Programu hii ni mahsusi kwa wilaya za Kilombero, Ulanga na Malinyi ambapo takribani vijiji 160 vitanufaika. Hadi sasa, Programu imehakiki na kupima vipande vya ardhi 84,795 katika vijiji 40 vya Wilaya za Kilombero na Ulanga.
Kati ya vipande vilivyohakikiwa na kupimwa, jumla ya Hati za Hakimiliki ya Kimila 24,650 zimeandaliwa.
Mpoto ambaye amekuwa akitembea katika maeneo mbalimbali ya nchi kusoma mazingira na kuwasikiliza wananchi wanasema nini juu ya maisha yao ili anapoandika nyimbo zake ziwe na kero za wananchi ambazo amezishuhudia kwa macho yake, wiki hii alipita mkoani Morogoro na kuzungumza na wananchi kuhusu maisha yao ndipo lilipo ibuka suala la programu ya Umilikishaji Ardhi (Land Tenure Support Programme – LTSP).

Mshairi huyo amesema baada ya kuzungumza na wananchi kadhaa ambao wamepitiwa na Programu hiyo aligundua nyuso zao jinsi zilivyokuwa na furaha baada ya kukabidhiwa hati zao ambazo zimeongeza thamani zaidi ya ardhi yao (viwanja na mashamba) kwa kuwa tayari vinatambulika kisheria.
“Kwa miaka mingi nchi yetu imekua na migogoro ya ardhi kati ya mtu na mtu,kijiji na Kijiji, wakulima na wafugaji, hata wawekezaji na wana nchi, Wizara ya Ardhi kupitia Mpango wa Land Tenure Support Programme (LTSP) inayotekelezwa katika Wilaya Tatu za Kilombero, Ulanga na Malinyi baadae kusambazwa Nchi nzima imefanya kazi kubwa sana,” alisema Mrisho Mpoto.

“Binafsi kama kawaida yangu kuzunguka kila koja na nchi yangu na kuzungumza na wananchi, nimeona ukubwa wa hii Programu, imeona thamani ya hii programu, wananchi wanaongea kwa furaha ya hali ya juu kutokana na hii programu. Mimi sio msemaji wa serikali lakini wakati nikiwa katika harakati za kutembea kwa ajili ya shughuli zangu za sanaa huwa napata fursa ya kuongea na wananchi wa eneo husika, wakazi wa Morogoro wanaishukuru sana serikali pamoja na Waziri Lukuvi, naamini hii programu inaweza kuwa mwarobaini wa haya matatizo ya ardhi, maana kila kipande cha ardhi kitapimwa na mwananchi kupewa hati yake ya umiliki, naamini itaweza kuondoa kabisa migogoro ya nrdhi nchini Tanzania, hongera Mhe.Lukuvi,” aliongeza Mpoto.

Alisema bado ataendelea kutembea katika maeno mbalimbali ya nchi kwa ajili ya kukutana na mashabiki wake wa muziki na kuzungumza nao kuhusu mambo mbalimbali ya nchi na pale ambako ataona kuna haja ya kutoa msaada atawasiliana wahusika kwaajili ya kutatua kero za wananchi.

Kazi nyingine zilizotekelezwa na programu ya LTSP ni pamoja na kusimika alama za msingi 54 za mtandao wa kijiodesia katika Wilaya za Kilombero, Ulanga, Malinyi na Mufindi, Kupima mipaka ya vijiji 121 na kutatua migogoro 71 ya mipaka ya vijiji iliyodumu kwa muda mrefu, Kuandaa vyeti vya Ardhi ya Kijiji kwa vijiji 57, Kuandaa mipango ya Matumizi ya Ardhi ya Vijiji kwa vijiji 53 na Kuchangia katika ujenzi na ukarabati wa masjala za ardhi na ofisi za vijiji katika vijiji 61.
Viongozi wengi wa Wizara wanaitembelea programu hiyo mara kwa mara na uongozi wa Wilaya na wananchi wanatoa ushirikiano mkubwa sana kwa kuwa programu iko katika Wilaya zao.
Hivi karibuni Katibu Mkuu Bibi. Dorothy Mwanyika mara tu baada ya kuteuliwa na Mhe Rais kuwa Katibu Mkuu wa Wizara alitembelea programu hiyo na kujionea namna programu inavyotumia teknolojia ya kisasa kabisa kupima ardhi ya wananchi vijijini. Pia, Mhe Naibu Waziri Mhe. Angelina Mabula nae alifanya ziara katika eneo la programu.

Breaking News: Mwenyekiti TEF Ajiuzuru



Hii Hapa Ratiba Ya Robo Fainali Europa League

Baada ya shirikisho la soka Ulaya UEFA kuchezesha droo ya UEFA Champions League hatua ya robo fainali, baada ya hapo wamechezesha pia droo ya robo fainali ya UEFA Europa League.

Baada ya droo hiyo kuchezeshwa Arsenal ambao waliwatoa AC Milan katika hatua ya 16 bora, wamepangwa na CSKA Moskva ya Urusi katika robo fainali Arsenal akianzia nyumbani.

 Mechi za kwanza za Robo fainali zitachezwa April 5 na Marudiano itakuwa  April 12 mwaka huu

Serikali Yakanusha kuhusu sukari ya Zanzibar Kuzuiwa Tanzania Bara

SeeBait
Serikali imekanusha taarifa zilizotolewa na baadhi ya vyombo vya habari kwamba, imekizuia Kiwanda cha Sukari Zanzibar, ZSFL, kuuza Sukari yake Tanzania Bara.

Akizungumza jana jijini Arusha, Mkurugenzi wa Idara ya Habari Maelezo ambaye pia ni Msemaji Mkuu wa Serikali, Dk. Hassan Abbas, amefafanua kwamba, kiwanda hicho kinapaswa kukidhi soko la Zanzibar la tani elfu 10 badala ya kulalamika kimezuiwa kuuza Sukari nje.

 Dk. Abbas alisema, mahitaji ya kawaida Zanzibar ya sukari ni Tani 17,000 hadi 20,000 kwa mwaka, lakini kiwanda hicho, kina uwezo wa kuzalisha tani elfu 10 japo kwa sasa uzalishaji umeshuka hadi tani elfu 8 hivyo kufanya Zanzibar kuwa na upungufu wa tani elfu 9 hadi elfu 12.

 Mapema wiki hii Kaimu Mkurugenzi Mkuu Kiwanda hicho cha Sukari Zanzibar, Bi. Fatma Salum Ali, alisema kiwanda hicho kinapata hasara ya shilingi 387,000 kwa kila tani moja ya Sukari inayozalishwa kutokana na kushindwa kupata kibali cha kuuza Sukari Tanzania Bara ambako kuna soko shindani kwa misingi ya gharama za uzalishaji na bei.

Uingereza Yaitaka Tanzania iiunge Mkono Mgogoro Wake na Urusi

Serikali ya Uingereza imeitaka Tanzania na Jumuiya ya Kimataifa kuiunga mkono katika kupinga kitendo cha Urusi kutumia sumu aina ya novichok katika jaribio la kumuua jasusi wa Kirusi, Sergei Skripal na binti yake, Yulia.

Tukio hilo lilitokea mwishoni mwa wiki iliyopita huko Salisbury, Uingereza na kwa sasa Skripal na Yulia wana hali mbaya hospitali.

Akizungumza na vyombo vya habari jijini Dar es Salaam jana, Balozi wa Uingereza nchini, Sarah Cooke alisema nchi yake haitavumilia majaribio yoyote ya mauaji ya watu wasio na hatia ndani ya ardhi yake.

Cooke alisisitiza kwamba ni wazi Urusi ilihusika kwenye jaribio hilo na walipewa nafasi ya kueleza kwa nini waliamua kutumia sumu hiyo ndani ya Uingereza licha ya kwamba matumizi ya kemikali kama silaha ni kinyume cha sheria za kimataifa. Hata hivyo, alisema mpaka sasa hawajatoa maelezo kuhusu suala hilo.

“Baadaye leo (jana) nitaonana na waziri wa mambo ya nje ili kumweleza kuhusu jambo hili na kuomba ushirikiano wa Tanzania. Ninaamini Tanzania iko pamoja nasi katika hili,” alisema balozi huyo.

Alipoulizwa kuhusu msimamo wa Tanzania kuhusu suala hilo, Naibu Waziri wa Mambo ya Nje, Dk Susan Kolimba alisema hawezi kulizungumzia kwa sasa.

Waziri wa Mambo ya Nje, Dk Augustine Mahiga hakupatikana kuzungumzia suala hilo .

Mpaka sasa Uingereza inaungwa mkono na Marekani, Ufaransa, Ujerumani, Austalia na Umoja wa Kujihami wa Nchi za Magharibi (Nato). Pia, imeripoti suala hilo kwenye Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa.

Pia imewatimua maofisa 23 wa intelijensia wa Urusi na imefuta ziara ya Waziri wa Mambo ya Nje wa Urusi, Sergey Lavrov.

Vilevile, Waziri Mkuu wa Uingereza, Theresa May ametangaza kwamba hakuna waziri yeyote au mtu kutoka familia ya kifalme atakayehudhuria Fainali za Kombe la Dunia zinazotarajiwa kufanyika Juni huko Urusi.

Ijumaa, 16 Machi 2018

Baada ya kufungiwa, Wambura aibua mapya TFF

Ukimwaga mboga, namwaga ugali ni miongoni mwa misemo maarufu ya lugha ya Kiswahili ambao unaweza kutimia baada ya Makamu wa Rais wa TFF kufungiwa maisha kujihusisha na masuala ya soka kufuatia kutiwa hatiani na kamati ya maadili ya TFF.

Baada ya hukumu kutangazwa, Michael Wambura alizungumza na vyombo vya habari akitoa ufafanuzi wa baadhi ya mambo lakini amesema kufungiwa kwake ni kwa hila na njama iliyopangwa na watu wachache.

Wambura ameibua hoja kadhaa akiituhumu TFF kuajiri baadhi ya watu bila nafasi hizo kutangazwa kama taratibu na kanuni zinavyoelekea, lakini pia ameituhumu tff kutumia kiasi kikubwa cha pesa kwa muda mfupili lakini hakuna kinachoonekana kufanywa kulingana na kiasi hicho cha pesa.

“Ni kweli kulikuwa na kikao lakini bado nasisitiza kilikuwa cha hila kilikuwa ni kikao ambacho kimeandaliwa kwa ajili ya kutoa maamuzi bila kujali hoja ambazo zitakwenda kujadiliwa. Ninasema hivyo kwa sababu siku ya Jumatatu nilikuwa TFF niliongea na Rais wa TFF pamoja na Katibu, Jumanne niliongea na Rais wa TFF lakini wote hawakuniambia kama kuna jambo lipo TFF linanihusu mpaka Jumanne nasafiri hakuna chochote kutoka TFF kuja kwangu lakini jioni saa 12 wanakwenda nyumbani kwangu kupeleka mashtaka.

“Kwa hiyo tayari kuna hila ambazo nilikuwa nimeziona katika jambo hilo, katika mashtaka yao msingi mkuu umeegemea katika kufoji document hakuna anaebisha walikuwa hawadaiwi, wote wanakiri kudaiwa katika barua mbalimbali za TFF lakini wanasema kwamba document zimefojiwa.

“Kiutaratibu kuna njia mbili, njia moja ni kupeleka polisi wakaangalie kama document imefojiwa baada ya kupata majibu ya polisi mnaelekea katika mkondo washeria ndio msingi wa hizi kamati. Hizi kamati haziwezi kuingia mahali ambapo kosa ni la jinai, ufojaji ni kosa la jinai sio la kimaadili kwa hiyo ilipaswa iende katika mfumo wa sheria ya jinai sio mfumo wa kimaadili.

“Kampuni ambayo wanasema document yake imefojiwa ilipaswa iitwe kwa sababu kampuni inaishi na ina wakurugenzi, kwa hiyo wakurugenzi ndio walipaswa kuitwa ikishajulikana hivyo kinachofuata ni kupelekwa polisi na kushtakiwa kama mhalifu mwingine lakini kwa sababu wameona hawana kesi ya msingi wakaamua kukaa na kamati walizoziunda wenyewe ili wamtoe Wambura katika nafasi kitu ambacho hakikubaliki.

“Kwa hiyo ninachoona yote haya ni kutokana na matatizo yaliyopo ndani ya TFF, jambo la miaka 14 iliyopita unataka kulijadili kwa siku moja kwa kumpa mtu notice usiku asubuhi aje mbele ya kamati, viongozi walikuwepo wengi wamepita hapo katikati wote walitakiwa waje kutoa ushahidi lakini hawakuitwa? Kwa nini walilipa? Au aliyelipwa alivunja ofisi?

“Isije ikawa kuna mtu amejilipa ndani ya TFF kwa jina la ile kampuni na kitu ambacho kipo, kuna watu wamelipwa pesa kwa kutumia jina la hiyo kampuni wakati hizo pesa hazijalipwa kwa kampuni ndiyo maana wanashindwa kutoa hizo document ndiyo maana tunasema walete nyaraka za hayo malipo kama hawajaiba wao wenyewe wanashindwa.

“Kama wanasema nimefoji barua nipo tayari twende polisi na mahakamani ndio maana nasema hili jambo limetengenezwa kimkakati halina mashiko hata kidogo ya kisheria, halina ushahidi ni jambo la uongo na kizandiki limetengenezwa na kikundi cha watu ambao wanaamini nikitoka kama mwenyekiti wa fedha mambo yao yatakuwa mazuri.

“Mimi nimechaguliwa na mkutano mkuu kwa zaidi ya kura asilimia 80, siwezi kuondolewa na watu watatu ambao hawakuchaguliwa hawana dhamana ya mkutano mkuu, haiwezekani. Kama unadhani nina kosa kanishtaki kule.

“Ni kweli kwamba kila uongozi unapokuja unakuwa na taratibu zake , sisi taratibu zetu za kiutendaji ni kwamba, nafasi ya katibu mkuu wa TFF lazima itangazwe kama makatibu wakuu wengine walivyopita, nafasi inatangzwa watanzania wenye sifa wanaomba kupitia makampuni ambayo ni huru, wanafanya usaili wanaajiriwa.

“Sisi pale kwetu kuna shida kidogo kuna watu wengine bado wana kazi mbili, kuna mtu mwinngine ameajiriwa huku anakuja pale kama secondment wakati kuna watanzania wengi wanaweza kuomba na kuajiriwa, sasa mtu ana kazi mbili.

“Suala la katibu mkuu anapaswa kuajiriwa, tulipochaguliwa kaimu katibu mkuu alikuwa Salum Madadi kwa sababu madadi alikuwa majiriwa wa TFF kwa hiyo alikuwa anakaimu nafasi kwa sababu alikuwa mwajiriwa wa TFF baadaye tulipokuja kumpa nafasi Wilfred Kidao yalikuwa ni makosa kwa sababu sheria zinakataza mjumbe wa mkutano mkuu kuajiriwa TFF na kidao ni mwenyekiti wa TAFCA hawezi kuajiriwa akawa mjumbe wa mkutano mkuu wakati huohuo.

“Tuna matatizo mengi, TRA wanatudai lakini bado tunakusanya kodi na tunazitumia, tunamatatizo ya fedha za wafadhili tunazihamisha matokeo yake ligi ya wanawake inasimama, wakati mwingine hata ligi kuu inasimama kwa sababu hakuna pesa lakini Azam wamelipa kwa hiyo tuna shida.

“Tunaposema tunataka tuweke nyumba kwenye mstari masuala ya kodi yaeleweke kodi zinazopokelewa na bodi zikalipwe TRA badala ya kuletwa TFF ndio mgogoro unapotokea. Bodi ya ligi ina kusanya kodi toka Azam, na wadhamini mbalimbali lakini kodi zile zinakuja kwetu TFF zikishakuja na kutumika mwenyekiti wa kamati ya fedha akisema hapana sio sahihi inakuwa issue.

“Matatizo mengi tutakuja kuyaona siku chache zijazo, watanzania watanielewa kwamba ndani ya TFF kuna matatizo makubwa sana na sio madogo kama watu wanavyofikiria, siku chache zijazo tutakuja kuyazungumza.

“Tumeshatumia kiasi cha shilingi 3 bilioni ndani ya miezi nane, kuna nini tumefanya? Zinapita tu. Jambo moja linapoanza uzuri wake linafuata na jingine kwa hiyo tutakwenda mpaka mahali tutakuwa sawa na ninaamini watafuata ninachokisema, bado tunahitaji kusafisha TFF kwa sababu haiko sawa.”

Hakuna kiingilio mchezo wa Ngorongoro, Morocco kesho


Watazamaji wataingia bure katika mchezo wa kirafiki kati ya timu ya taifa ya vijana chini ya umri wa miaka 20, Ngorongoro Heroes na vijana wenzao wa Morocco kesho Uwanja wa Uhuru mjini Dar es Salaam.

Hayo yamesemwa leo mjini Dar es Salaam na Afisa Habari wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), Clifford Ndimbo alipozungumza na Waandishi wa Habari kuhusu maandalizi ya mchezo huo utakoanza  Saa 10:00 jioni.

Ngorongoro iliyo chini ya kocha Ammy Ninje, itakuwa na mechi mbili za kirafiki na mbali na hiyo ya kesho, nyingine itafuatia Jumatano ya Machi 21, dhidi ya Msumbiji.

Kwa Ngorongoro mechi hizo ni maandalizi ya mchezo wa kuwania kufuzu kwa fainali za Kombe la mataifa ta Afrika (AFCON U20) dhidi ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC) Machi 31 Uwanja wa Taifa na marudiano wiki mbili baadaye mjini Kinshasa.

Ngorongoro Heroes imeingia kambini katika Hoteli ya Ndege Beach iliyopo Mbweni ambapo inajiandaa na michezo hiyo miwili ya kirafiki na mchezo wa kuwania kufuzu kwa Fainali za Vijana Afrika wenye umri chini ya miaka 20.

Ninje anapewa Ngorongoro baada ya kuweka rekodi mbaya kwenye Challenge nchini Kenya mwaka jana, Kili Stars ikiondoka bila kushinda hata mechi moja, ikiambulia sare moja na kufungwa mechi zote. Katika michuano hiyo, pamoja na Ninje kuboronga, aliwakera Watanzania kwa majibu yake.

MESSI AMPIKU BEN YEDDER, ABEBA TUZO YA MCHEZAJI BORA LIGI YA MABINGWA ULAYA


Nyota wa FC. Barcelona, Lionel Messi ametangazwa kuwa mchezaji bora wa wiki wa Ligi ya Mabingwa Barani Ulaya.

Messi amewapiku wachezaji Edin Džeko (As Roma), Ben Yedder (Sevilla) na Thomas Müller (Bayern Munchen) waliokuwa kwenye kinyang'anyiro.

Messi ameibeba tuzo hii baada ya kuisaidia Barcelona kuibuka na ushindi wa mabo 3-0 dhidi ya Chelsea, Jumatano ya wiki hii.

Kufuatia ushindi huo, Barcelona imepangwa kucheza na AS Roma ya Italy kwenye hatua ya robo fainali ya mashindano.

TIMU YA TAIFA YA MOROCCO YAWASILI NCHINI, YAPOKELEWA NA BASI LA AZAM FC


Timu ya taifa ya Vijana kutoka Morocco, chini ya miaka 20, imewasili jijini Dar es Salaam, tayari kwa mchezo wa kirafiki.

Morocco itacheza dhidi ya Ngorongoro Heroes kesho Jumamosi ikiwa ni maandalizi ya kuelekea mchezo wa kufuzu kucheza AFCON U20 dhidi ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo.

Mchezo huo wa kirafiki utakuwa wa kwanza, kabla ya kucheza tena na Msumbiji, Jumatano ya Machi 21 2018 .

Mechi ya kufuzu kuelekea dhidi ya Congo, AFCON U20, itachezwa Machi 31 2018 kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam na marudiano yatafanyika baada ya wiki mbili huko jijini Kinshasa, Congo.

Kocha wa Al Masry akiri mchezo wa kesho hautakuwa mrahisi


Ikiwa ni siku moja tu ya leo iliyosalia kuelekea mchezo wa Kombe la Shirikisho Afrika kati ya Al Masry SC dhidi ya Simba SC, Kocha wa Al Masry, Hossam Hassan anaamini mtanange huo hautakuwa mrahisi.

Kwa mujibu wa mtandao 'Kingfut.com' Hassan anatarajia upinzani mgumu kesho Jumamosi dhidi ya Simba kuliko hata walipokutana na Green Buffaloes waliyoiondoa kwenye hatua iliyopita kwa mabao 5-2.

"Tulicheza vizuri mechi ya awali na tungeweza kushinda kirahisi, nawaamini wachezaji wangu kwa kiwango walichonacho japo tunapaswa kupambana kwasababu mechi ya kesho itakuwa ngumu" alisema Hossam.

Hossam aliongeza kwa kusema Simba ni klabu kubwa yenye uzoefu kwenye mashindano haya huku akisisitiza lazima wajitume kwenye mchezo huo wa marudiano.

"Simba ni timu kubwa yenye uzoefu kwenye mashindano, ilionesha vile walivyojipanga katika mchezo wa kwanza. Sisi matarajio yetu ni kupambana ili tuweze kushinda" alisema.

Uchebe na Shilole wafunguka kuhusu ndoa yao


Msanii wa muziki bongo ambaye kwa sasa mjasiriamali anayehakikisha matumbo ya watu yanapata afya, Shilole au Shishi Trump, hatimaye amefunguka kuhusu kuvunjika kwa ndoa yake na mume wake Uchebe.

Akizungumza na mwandishi wa www.eatv.tv, Shilole amesema hajaachana na mume wake na wala hawafikirii kuachana.

Kwa upande wa mume wake Shilole Bwana Uchebe amesema sio kweli kwamba ameachana na mkewe, na kwamba kuna wanafiki wanapenda wasikie wameachana.

Akifunguka kuhusu kupost kwa ua jeusi na caption yenye utata, Uchebe amesema kuna mtu alihack acount yake na kupost hivyo, lakini hawajaachana namkewe na wala sio kiki.

“Sio kweli sijaachana na mke wangu na wala hatufikirii kuachana, kuna watu wanafiki wanapenda kusikia tumeachana, kuhusu ile post kuna mtu alifanikiwa kuhack acount yangu na kupost vile lakini sijamuacha mke wangu, na wala hatuna ugomvi, na niwaambie tu kuwa hatuachani leo hata kiama”, amesema Uchebe.

Tetesi za wawili hao kuachana zimekuja baada ya kupostiwa kwa ua jeusi kwenye ukurasa wa instagram wa Uchebe na caption ambayo ilikuwa na utata, na watu kuhisi labda wawili hao hawako pamoja tena.

Facebook Twitter Google+ Pinterest

Diamond atinga Billboard kwa kishindo


Moja ya ndoto nyingi za mastaa kibao wa muziki ni kupata nafasi Billboard. Diamond Platnumz amepata bahati hiyo baada ya kuandikwa kwenye makala ya mtandao wa Billboard.


Katika picha ambayo imewekwa kwenye makala hiyo, Diamond amewekwa pamoja na wasanii wengine wanne kutoka Afrika Magaribi akiwemo Wizkid, Davido na Tiwa Savage.

Kwenye makala hiyo ambayo imewaonyesha wasanii hao inazungumzia juu ya lebo kubwa za muziki duniani zinavyoangazia Afrika kumpata staa ajaye wa Pop duniani.

Hilo limekuja ikiwa ni siku chache zimepita baada ya kampuni ya Universal Music Group ambayo pia inasimamia kazi za Diamond, kupitia tawi lake la nchini Uholanzi ilitangaza kununua hisa asilimia 70 za lebo ya AI Records ya nchini Kenya.

UMG watakuwa wanafanya kazi za kusambaza kazi za wasanii wa Al Records duniani kote ikiwemo kwenye mitandao mikubwa tofauti tofauti ya muziki.

TFF wajibu hoja za Michael Wambura

Shirikisho la soka nchini TFF limejibu tuhuma zilizotolewa na makamu wa rais wa shirikisho hilo Michael Richard Wambura, baada ya hukumu ya kufungiwa maisha kutangazwa dhidi yake na kamati ya maadili inayoongozwa na mwenyekiti Hamidu Mbwezeleni.

Wambura alizungumza na waandishi wa habari kupinga hukumu iliyotolewa dhidi yake, huku akiweka wazi  baadhi ya mambo ambayo anaamini yamekua mzizi wa yeye kufanyia figisu hadi kuingizwa hatiani.

Mdau huyo wa soka alidai kuwa, kuna mambo mengi yanaendelea ndani ya TFF likiwepo suala la ubadhilifu wa fedha, ambao umekua kinyume na utaratibu, jambo ambalo aliahidi kulitafutia siku la kulianika hadharani kupitia vyombo vya habari.

TFF imejibu tuhuma hizo kwa kutoa ufafanuzi wa kina katika kila kipengele ambacho kilizungumzwa na Wambura alipokutana na waandishi wa habari jijini Dar es salaam.


1.Matumizi mabaya ya fedha za TFF
JIBU : Wambura kama Mwenyekiti wa kamati ya fedha amehudhuria vikao zaidi ya 4 vya kamati na hajawahi kulalamika kokote mpaka amefungiwa.

Bajeti ya TFF iliyopitishwa Dodoma kwa Mwaka Mzima ni Bilioni 8.6 hivyo matumizi anayosema ya Bilioni 3 kwa miezi 7 yanaonyesha jinsi gani TFF inavyopambana na changamoto za kifedha hivyo kuhakikisha inapunguza matumizi.

Mapato yaliyopatikana kwa miezi Saba (7) iliyopita yalitumika katika maeneo yafuatayo :

Timu ya Taifa Taifa stars(Fifa dates),Kilimanjaro Stars  (Challange Cup),Kambi kwa Timu ya Taifa Under23, Kambi U20, U16, Wanawake U20, Ligi za Wanawake, Kombe la Shirikisho la Azam, kozi za makocha,kozi za waamuzi za nje na ndani, vikao vya kamati ya utendaji na  kamati ndogo ndogo, mishahara ya watumishi wa TFF na makocha wa timu za Taifa, kulipa madeni tuliyoyakuta na kuidhinishwa na kamati ya fedha, kozi za Grassroots na Live Your Goal na soka la Ufukweni

2.Ajira za TFF watu kupewa kwa kujuana.
JIBU : TFF haijawahi kuajiri nafasi yoyote ile zaidi ya Wakurugenzi 3 na meneja 1 tofauti na uongo unaozungumzwa,Wakurugenzi walioajiriwa ni Mkurugenzi wa Fedha,Mkurugenzi wa Mashindano,Mkurugenzi wa sheria na Wanachama na Meneja Masoko,katika kupunguza matumizi ya fedha Taasisi imebaki na Wafanyakazi 21 kutoka 44 wa awali waliokutwa na Ndugu Karia.

3.Kumteua Wilfred Kidao kuwa kaimu Katibu Mkuu wa TFF.
JIBU : Kaimu Katibu Mkuu alikaimishwa na Kamati ya Utendaji na yeye Wambura akiwa mmoja wa waliompitisha.

4.Mipira 100 kila mkoa kwamba kuna watu wamepiga fedha za TFF.
JIBU : TFF chini ya Rais wa TFF aliyekuwepo madarakani Ndugu Wallace Karia haijawahi kununua mipira,mipira iliyotolewa ilinunuliwa na uongozi uliopita ilichofanya TFF ni kuigawa kama ilivyofanya.

5.Kuwa na wafanyakazi wawili kwenye nafasi moja.
JIBU : TFF haijawahi kuajiri mfanyakazi zaidi ya mmoja kwenye nafasi moja,wengi waliokuwepo kwenye Shirikisho kwa sasa wanajitolea akiwemo Afisa Habari.

6.Suala la Waamuzi kuondolewa kuchezesha ligi kuu.
JIBU : Ili kuongeza ubora wa uchezeshaji TFF ikaamua kuchaguwa waamuzi wa juu(Elite) tofauti na awali ambako kulikuwa na idadi kubwa mchanganyiko ya waamuzi.

7.Kaimu Katibu kutuma majina ya Makamishina.
JIBU : Jina la Michael Wambura na Ahmed Mgoyi ndio yaliyopelekwa kama utaratibu unavyotaka ya kujaza kwenye fomu moja pekee na TFF haikuwahi kubadilisha wala kukata jina la mtu yeyote.

8.TFF ya sasa mpaka uwe na urafiki na watu 3 Karia, Mgoyi, na Nyamlani.
JIBU : TFF haiendeshwi kwa urafiki bali kwa utaratibu wenye kufuata kanuni.

Kikao kilichotoa maamuzi ni Kamati inayojitegemea (Independent) sio rahisi kuingiliwa kwa kuwa hata Rais wa TFF hawezi kuiingilia

Kumekuwa na upotoshaji mkubwa unaoenezwa kwa maslahi binafsi,ni vyema watu wakajikita kwenye kujibu tuhuma zao bila kuhusisha uongo na vitu visivyo vya kweli kwa Taasisi ambayo kwasasa ipo makini kwenye kuhakikisha kila kitu kinafuata utaratibu ikiwemo masuala ya kifedha pamoja na mambo mengine.

Imetolewa na Idara ya Habari na Mawasiliano TFF

ni huzuniSimanzi na Majonzi Ibada ya Mazishi ya Mmiliki wa Mabasi ya Super Sami Aliyeuawa na Kutupwa Mtoni

Vilio, simanzi na majonzi vimetawala kwa  waombolezaji kutoka jijini Mwanza na maeneo jirani wanaendelea na ibada ya mazishi ya mfanyabiashara Samson Josia yanayofanyika nyumbani kwake mtaa wa majengo mapya wilaya ya Magu mkoani Mwanza.

Mwili wa mfanyabiashara huyo uliokutwa ukiwa umefungwa kwenye viroba ukielea ndani ya Mto Ndabaka mpakani mwa wilaya za Bunda mkoa wa Mara na Busega mkoani Simiyu umewasili asubuhi ya leo Machi 16 ukitokea Hospitali ya Rufaa Mara ulikohifadhiwa kwa ajili ya uchunguzi tangu juzi.

Tangu asubuhi, mamia ya waombolezaji kutoka jijini Mwanza na maeneo jirani wamekuwa wakimiminika nyumbani kwa marehemu wakitumia mabasi ya kampuni aliyokuwa akimiliki.

Mabasi ya kampuni nyingine pia yanatumika kusafirisha waombolezaji kutoka jijini Mwanza bila malipo.

Marehemu Josia aliyezaliwa mwaka 1968 alipotea tangu Februari 27 kabla ya gari lake kukutwa likiwa limeteketezwa kwa moto ndani ya eneo  la hifadhi ya Taifa ya Serengeti mkoani Mara Machi 9.

Ibada ya mazishi inaongozwa na Mchungaji Jackson Meza kutoka Kanisa la African Inland Church of Tanzania (AICT) huku kwaya ya kanisa ambayo marehemu alikuwa mfadhili wake ikiimba nyimbo za maombolezo.

Kwa mujibu wa Kamanda wa Polisi mkoa wa Mara, Jaffari Mohamed, watu wanne wanashikiliwa na jeshi hilo kwa mahojiano kuhusiana na kifo hicho kilichoibua hofu na maswali yasiyo na majibu miongoni mwa ndugu, jamaa, marafiki na wakazi wa jiji la Mwanza ambako marehemu alikuwa akiendesha shughuli zake za kibiashara.

Mtaalamu wa Nyoka auawa na Cobra

Upo msemo unaosema ‘Mganga hajigangi’ na ndio msemo unaoweza kuutumia kwenye tukio moja lililomkuta mwanaume mmoja ambae ni raia wa Malaysia ni maarufu kwa jina la ‘mwanaume anayemudu’ nyoka.
Mwanaume mmoja ajulikanaye kwa jina la Abu Zarin Hussin ambaye taaluma yake alikuwa ni Askari wa Zimamoto akiwa amepitia mafunzo maalumu ya kukabiliana au kuwamudu nyoka, ameripotiwa kufa siku za hivi karibuni kwa kung’atwa na nyoka.
Mtaalamu huyo wa nyoka anadaiwa kung’atwa na nyoka aina ya cobra hadi kupoteza maisha akiwa katika shughuli zake za kila siku, Jumatatu ya March 12, 2018 na kupelekwa hospitali kwa matibabu, lakini akafariki leo March 16, 20

Kumbukumbu ya miaka 50 ya mauaji ya My Lai Vietnam

Siku ya leo March 16, 2018 ni kumbukumbu ya miaka 50 tangu yatokee mauaji makubwa ya yanayofahamika kama My Lai yaliyotokea eneo la Son My nchini Vietnam.
Mnamo March 16, 1968 wanajeshi wa Marekani waliwaua watu 504 ambao walikuwa raia wa Vietnam na tukio hili lilitokea na kutambulika kama tukio la kutisha zaidi ambalo lilitokea wakati wa Vita ya Wavietnam.
Waliuawa wanawake, wanaume na watoto, huku idadi kubwa ya wanawake wakibakwa na kutendewa vitendo vya kikatili.

habari njema Tanzania ya pili katika nchi ambazo uchumi wake unakua kwa kasi Afrika

Leo March 16, 2018 Jarida maarufu la Business Chief limeitaja Tanzania kama taifa la pili lenye uchumi unaokuwa kwa kasi zaidi barani Africa. Tanzania uchumi wake unakua kwa asilimia 7 imeshika nafasi ya pili nyuma ya Ivory Cost ambayo uchumi wake unakuwa kwa asilimia 8.5.
Orodha hiyo inayotangazwa kila mwaka, imesheheni mataifa ya Africa mashariki kwani ndio ukanda ambao umetajwa kuwa na uchumi unaokuwa kwa kasi, huku kilimo, utalii, usafiri, mawasiliano na biashara zikitajwa kama sekta zinazotazamwa na kuingiza vipato vikubwa.

Ukiondoa Tanzania na Ivory Coast mataifa mengine yaliyotajwa ni kama ifuatayo;
Senegal,
Djibout,
Rwanda,
Kenya,
Mozambique,
Central African Republic,
Sierra Leone
Pamoja na Uganda.