Rais anayemaliza muda wake wa
nchini Botswana Ian Khama amemshukia Rais wa Marekani Donald Trump kuwa
anahimiza shughuli za ujangili Afrika.
Ameyasema hayo akiwa anafanyiwa mahojiano na Shirika la Utangazaji la
BBC katika Mkutano wa Masuala ya Kupinga Ujangili (Anti-poaching
Summit) nchini Botswana ikiwa ni wiki mbili kabla ya kuachia madaraka
rasmi.Rais Khama ameeleza kuwa hiyo ni kutokana na Rais Trump kukataa marufuku ya kuingiza nchini Marekani nyara za uwindaji kutoka Bara la Afrika.
“Tatizo sio mtazamo wa Trump kwenye suala zima la wanyamapori tu bali hata mtazamo wake kwa sayari nzima. Serikali yake ilishakataza kuingiza nchini nyara hizo, yeye kukataa marufuku hiyo ni kuchochea ujangili.” – Ian Khama
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni