Ukimwaga
mboga, namwaga ugali ni miongoni mwa misemo maarufu ya lugha ya
Kiswahili ambao unaweza kutimia baada ya Makamu wa Rais wa TFF kufungiwa
maisha kujihusisha na masuala ya soka kufuatia kutiwa hatiani na kamati
ya maadili ya TFF.
Baada
ya hukumu kutangazwa, Michael Wambura alizungumza na vyombo vya habari
akitoa ufafanuzi wa baadhi ya mambo lakini amesema kufungiwa kwake ni
kwa hila na njama iliyopangwa na watu wachache.
Wambura
ameibua hoja kadhaa akiituhumu TFF kuajiri baadhi ya watu bila nafasi
hizo kutangazwa kama taratibu na kanuni zinavyoelekea, lakini pia
ameituhumu tff kutumia kiasi kikubwa cha pesa kwa muda mfupili lakini
hakuna kinachoonekana kufanywa kulingana na kiasi hicho cha pesa.
“Ni
kweli kulikuwa na kikao lakini bado nasisitiza kilikuwa cha hila
kilikuwa ni kikao ambacho kimeandaliwa kwa ajili ya kutoa maamuzi bila
kujali hoja ambazo zitakwenda kujadiliwa. Ninasema hivyo kwa sababu siku
ya Jumatatu nilikuwa TFF niliongea na Rais wa TFF pamoja na Katibu,
Jumanne niliongea na Rais wa TFF lakini wote hawakuniambia kama kuna
jambo lipo TFF linanihusu mpaka Jumanne nasafiri hakuna chochote kutoka
TFF kuja kwangu lakini jioni saa 12 wanakwenda nyumbani kwangu kupeleka
mashtaka.
“Kwa
hiyo tayari kuna hila ambazo nilikuwa nimeziona katika jambo hilo,
katika mashtaka yao msingi mkuu umeegemea katika kufoji document hakuna
anaebisha walikuwa hawadaiwi, wote wanakiri kudaiwa katika barua
mbalimbali za TFF lakini wanasema kwamba document zimefojiwa.
“Kiutaratibu
kuna njia mbili, njia moja ni kupeleka polisi wakaangalie kama document
imefojiwa baada ya kupata majibu ya polisi mnaelekea katika mkondo
washeria ndio msingi wa hizi kamati. Hizi kamati haziwezi kuingia mahali
ambapo kosa ni la jinai, ufojaji ni kosa la jinai sio la kimaadili kwa
hiyo ilipaswa iende katika mfumo wa sheria ya jinai sio mfumo wa
kimaadili.
“Kampuni
ambayo wanasema document yake imefojiwa ilipaswa iitwe kwa sababu
kampuni inaishi na ina wakurugenzi, kwa hiyo wakurugenzi ndio walipaswa
kuitwa ikishajulikana hivyo kinachofuata ni kupelekwa polisi na
kushtakiwa kama mhalifu mwingine lakini kwa sababu wameona hawana kesi
ya msingi wakaamua kukaa na kamati walizoziunda wenyewe ili wamtoe
Wambura katika nafasi kitu ambacho hakikubaliki.
“Kwa
hiyo ninachoona yote haya ni kutokana na matatizo yaliyopo ndani ya
TFF, jambo la miaka 14 iliyopita unataka kulijadili kwa siku moja kwa
kumpa mtu notice usiku asubuhi aje mbele ya kamati, viongozi walikuwepo
wengi wamepita hapo katikati wote walitakiwa waje kutoa ushahidi lakini
hawakuitwa? Kwa nini walilipa? Au aliyelipwa alivunja ofisi?
“Isije
ikawa kuna mtu amejilipa ndani ya TFF kwa jina la ile kampuni na kitu
ambacho kipo, kuna watu wamelipwa pesa kwa kutumia jina la hiyo kampuni
wakati hizo pesa hazijalipwa kwa kampuni ndiyo maana wanashindwa kutoa
hizo document ndiyo maana tunasema walete nyaraka za hayo malipo kama
hawajaiba wao wenyewe wanashindwa.
“Kama
wanasema nimefoji barua nipo tayari twende polisi na mahakamani ndio
maana nasema hili jambo limetengenezwa kimkakati halina mashiko hata
kidogo ya kisheria, halina ushahidi ni jambo la uongo na kizandiki
limetengenezwa na kikundi cha watu ambao wanaamini nikitoka kama
mwenyekiti wa fedha mambo yao yatakuwa mazuri.
“Mimi
nimechaguliwa na mkutano mkuu kwa zaidi ya kura asilimia 80, siwezi
kuondolewa na watu watatu ambao hawakuchaguliwa hawana dhamana ya
mkutano mkuu, haiwezekani. Kama unadhani nina kosa kanishtaki kule.
“Ni
kweli kwamba kila uongozi unapokuja unakuwa na taratibu zake , sisi
taratibu zetu za kiutendaji ni kwamba, nafasi ya katibu mkuu wa TFF
lazima itangazwe kama makatibu wakuu wengine walivyopita, nafasi
inatangzwa watanzania wenye sifa wanaomba kupitia makampuni ambayo ni
huru, wanafanya usaili wanaajiriwa.
“Sisi
pale kwetu kuna shida kidogo kuna watu wengine bado wana kazi mbili,
kuna mtu mwinngine ameajiriwa huku anakuja pale kama secondment wakati
kuna watanzania wengi wanaweza kuomba na kuajiriwa, sasa mtu ana kazi
mbili.
“Suala
la katibu mkuu anapaswa kuajiriwa, tulipochaguliwa kaimu katibu mkuu
alikuwa Salum Madadi kwa sababu madadi alikuwa majiriwa wa TFF kwa hiyo
alikuwa anakaimu nafasi kwa sababu alikuwa mwajiriwa wa TFF baadaye
tulipokuja kumpa nafasi Wilfred Kidao yalikuwa ni makosa kwa sababu
sheria zinakataza mjumbe wa mkutano mkuu kuajiriwa TFF na kidao ni
mwenyekiti wa TAFCA hawezi kuajiriwa akawa mjumbe wa mkutano mkuu wakati
huohuo.
“Tuna
matatizo mengi, TRA wanatudai lakini bado tunakusanya kodi na
tunazitumia, tunamatatizo ya fedha za wafadhili tunazihamisha matokeo
yake ligi ya wanawake inasimama, wakati mwingine hata ligi kuu inasimama
kwa sababu hakuna pesa lakini Azam wamelipa kwa hiyo tuna shida.
“Tunaposema
tunataka tuweke nyumba kwenye mstari masuala ya kodi yaeleweke kodi
zinazopokelewa na bodi zikalipwe TRA badala ya kuletwa TFF ndio mgogoro
unapotokea. Bodi ya ligi ina kusanya kodi toka Azam, na wadhamini
mbalimbali lakini kodi zile zinakuja kwetu TFF zikishakuja na kutumika
mwenyekiti wa kamati ya fedha akisema hapana sio sahihi inakuwa issue.
“Matatizo
mengi tutakuja kuyaona siku chache zijazo, watanzania watanielewa
kwamba ndani ya TFF kuna matatizo makubwa sana na sio madogo kama watu
wanavyofikiria, siku chache zijazo tutakuja kuyazungumza.
“Tumeshatumia
kiasi cha shilingi 3 bilioni ndani ya miezi nane, kuna nini tumefanya?
Zinapita tu. Jambo moja linapoanza uzuri wake linafuata na jingine kwa
hiyo tutakwenda mpaka mahali tutakuwa sawa na ninaamini watafuata
ninachokisema, bado tunahitaji kusafisha TFF kwa sababu haiko sawa.”
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni