mwana wa liganga blog ni blog ya kutoa taarifa, matukio, yaliyotokea katika ulimwengu hususani katika nchi yaTanzania
blog hii inasimamiwa na mwandishi wa habari kitaaluma bwana Deus Thomas liganga.lengo ni kutoa taarifa kwa umma,kwa maendeleo ya taifa na Dunia kwa ujumla
kwa mawasiliano kuhusu mtangazo, habari, wasiliana nasi 0659944423,deusliganga@yahoo.com,mzeeliganga@gmail.com
Ijumaa, 16 Machi 2018
Hakuna kiingilio mchezo wa Ngorongoro, Morocco kesho
Watazamaji wataingia bure katika mchezo wa kirafiki kati ya timu ya
taifa ya vijana chini ya umri wa miaka 20, Ngorongoro Heroes na vijana
wenzao wa Morocco kesho Uwanja wa Uhuru mjini Dar es Salaam.
Hayo yamesemwa leo mjini Dar es Salaam na Afisa Habari wa Shirikisho la
Soka Tanzania (TFF), Clifford Ndimbo alipozungumza na Waandishi wa
Habari kuhusu maandalizi ya mchezo huo utakoanza Saa 10:00 jioni.
Ngorongoro iliyo chini ya kocha Ammy Ninje, itakuwa na mechi mbili za
kirafiki na mbali na hiyo ya kesho, nyingine itafuatia Jumatano ya Machi
21, dhidi ya Msumbiji.
Kwa Ngorongoro mechi hizo ni maandalizi ya mchezo wa kuwania kufuzu kwa
fainali za Kombe la mataifa ta Afrika (AFCON U20) dhidi ya Jamhuri ya
Kidemokrasia ya Kongo (DRC) Machi 31 Uwanja wa Taifa na marudiano wiki
mbili baadaye mjini Kinshasa.
Ngorongoro Heroes imeingia kambini katika Hoteli ya Ndege Beach iliyopo
Mbweni ambapo inajiandaa na michezo hiyo miwili ya kirafiki na mchezo wa
kuwania kufuzu kwa Fainali za Vijana Afrika wenye umri chini ya miaka
20.
Ninje anapewa Ngorongoro baada ya kuweka rekodi mbaya kwenye Challenge
nchini Kenya mwaka jana, Kili Stars ikiondoka bila kushinda hata mechi
moja, ikiambulia sare moja na kufungwa mechi zote. Katika michuano hiyo,
pamoja na Ninje kuboronga, aliwakera Watanzania kwa majibu yake.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni