Serikali
imekanusha taarifa zilizotolewa na baadhi ya vyombo vya habari kwamba,
imekizuia Kiwanda cha Sukari Zanzibar, ZSFL, kuuza Sukari yake Tanzania
Bara.
Akizungumza
jana jijini Arusha, Mkurugenzi wa Idara ya Habari Maelezo ambaye pia ni
Msemaji Mkuu wa Serikali, Dk. Hassan Abbas, amefafanua kwamba, kiwanda
hicho kinapaswa kukidhi soko la Zanzibar la tani elfu 10 badala ya
kulalamika kimezuiwa kuuza Sukari nje.
Dk.
Abbas alisema, mahitaji ya kawaida Zanzibar ya sukari ni Tani 17,000
hadi 20,000 kwa mwaka, lakini kiwanda hicho, kina uwezo wa kuzalisha
tani elfu 10 japo kwa sasa uzalishaji umeshuka hadi tani elfu 8 hivyo
kufanya Zanzibar kuwa na upungufu wa tani elfu 9 hadi elfu 12.
Mapema
wiki hii Kaimu Mkurugenzi Mkuu Kiwanda hicho cha Sukari Zanzibar, Bi.
Fatma Salum Ali, alisema kiwanda hicho kinapata hasara ya shilingi
387,000 kwa kila tani moja ya Sukari inayozalishwa kutokana na kushindwa
kupata kibali cha kuuza Sukari Tanzania Bara ambako kuna soko shindani
kwa misingi ya gharama za uzalishaji na bei.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni