Taarifa hiyo iliyotolewa kupitia mtandao wa twitter wa UVCCM imesema kuwa Jokate Mwegelo ametenguliwa katika nafasi hiyo ambapo amehudumu katika nafasi hiyo kwa takribani miezi 11 toka amelipoteuliwa April 2017.
Kikao hicho kilichomtengua Jokate kiliendeshwa na Mwenyekiti wa Umoja wa Vijana wa Chama cha Mapinduzi Ndg. Kheri Denis James (MCC) katika ukumbi wa secretariet White house Mjini Dodoma lakini bado hawajaweka wazi sababu zilizopelekea kutengua uteuzi wa Jokate Mwegelo.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni