Teknolojia ya VAR inayotumika kuwasaidia waamuzi kuangalia replay na kufanya maamuzi yaliyokuwa sahihi, tayari ilikuwa imeshakubalika kutumika Africa katika mchezo wa CAF Super Cup na sasa FIFA wamethibitisha kuwa teknolojia hiyo itatumika katika game za World Cup 2018.
Rais wa FIFA Gianni Infantino amethibitisha taarifa hizo wakati wa kikao cha FIFA kilichofanyika Bogota Colombia “Tunatakiwa tuishi kwa kuangalia nyakati, tunataka kuwapa waamuzi vifaa ambavyo vitawasaidia kufanya maamuzi sahihi katika Kombe la Dunia nchini Urusi”
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni