Inaelezwa kuwa uamuzi huo wa kufukuza wanadiplomasia hao utatekelezwa ndani ya kipindi cha wiki moja na hii ni kutokana na Uingereza kufukuza Wanadiplomasia 23 wa Urusi waliokuwa nchi Uingereza.
Suala hili linakuja baada ya tukio la March 4, 2018 ambapo Mpelelezi wa zamani wa Urusi Sergei Skripal alikutwa na mwanaye Yulia wako kwenye hali mbaya baada ya kupewa sumu ya kemikali na watu wasiojulikana nyumbani kwao Salisbury England.
Kwa mujibu wa Waziri Mkuu wa Uingereza Theresa May, wanaamini tukio hilo limefanywa na watu wa Urusi na hivyo kuamua kuwafukuza wanadiplomasia hao 23 wa Urusi nchini humo Uingereza.
Kutokana na hilo, Urusi imejibu mapigo hayo. Skripal na mwanaye huyo Yulia bado wako hospitalini wakipatiwa matibabu.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni