Msanii wa muziki wa asili, Mrisho Mpoto ambaye amekuwa kioo cha jamii
kwa muda mrefu kutokana na kutoa nyimbo za kijamii zenye kuwataka
wananchi kuwa wazalendo kwa kufanya kazi kwa bidii ili kujipatia kipato
cha halali, kukemea rushwa na uonevu, Ijuma hii amefurahishwa na
Programu ya Umilikishaji Ardhi (Land Tenure Support Programme – LTSP).
Mhe. Lukuvi akiwa kwenye mradi huo
Programu hiyo ambayo inatakelezwa katika Wilaya za Kilombero, Ulanga
na Malinyi mkoani Morogoro chini ya Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo
ya Makazi chini ya Waziri wake, Mhe. William Lukuvi ili kukabiliana na
migogoro ya ardhi ambayo imekuwa ikiibuka katika maeneo mbalimbali
nchini Tanzania.
Programu hii ni mahsusi kwa wilaya za Kilombero, Ulanga na Malinyi
ambapo takribani vijiji 160 vitanufaika. Hadi sasa, Programu imehakiki
na kupima vipande vya ardhi 84,795 katika vijiji 40 vya Wilaya za
Kilombero na Ulanga.
Kati ya vipande vilivyohakikiwa na kupimwa, jumla ya Hati za Hakimiliki ya Kimila 24,650 zimeandaliwa.
Mpoto ambaye amekuwa akitembea katika maeneo mbalimbali ya nchi
kusoma mazingira na kuwasikiliza wananchi wanasema nini juu ya maisha
yao ili anapoandika nyimbo zake ziwe na kero za wananchi ambazo
amezishuhudia kwa macho yake, wiki hii alipita mkoani Morogoro na
kuzungumza na wananchi kuhusu maisha yao ndipo lilipo ibuka suala la
programu ya Umilikishaji Ardhi (Land Tenure Support Programme – LTSP).
Mshairi huyo amesema baada ya kuzungumza na wananchi kadhaa ambao
wamepitiwa na Programu hiyo aligundua nyuso zao jinsi zilivyokuwa na
furaha baada ya kukabidhiwa hati zao ambazo zimeongeza thamani zaidi ya
ardhi yao (viwanja na mashamba) kwa kuwa tayari vinatambulika kisheria.
“Kwa miaka mingi nchi yetu imekua na migogoro ya ardhi kati ya mtu na
mtu,kijiji na Kijiji, wakulima na wafugaji, hata wawekezaji na wana
nchi, Wizara ya Ardhi kupitia Mpango wa Land Tenure Support Programme
(LTSP) inayotekelezwa katika Wilaya Tatu za Kilombero, Ulanga na Malinyi
baadae kusambazwa Nchi nzima imefanya kazi kubwa sana,” alisema Mrisho
Mpoto.
“Binafsi kama kawaida yangu kuzunguka kila koja na nchi yangu na
kuzungumza na wananchi, nimeona ukubwa wa hii Programu, imeona thamani
ya hii programu, wananchi wanaongea kwa furaha ya hali ya juu kutokana
na hii programu. Mimi sio msemaji wa serikali lakini wakati nikiwa
katika harakati za kutembea kwa ajili ya shughuli zangu za sanaa huwa
napata fursa ya kuongea na wananchi wa eneo husika, wakazi wa Morogoro
wanaishukuru sana serikali pamoja na Waziri Lukuvi, naamini hii programu
inaweza kuwa mwarobaini wa haya matatizo ya ardhi, maana kila kipande
cha ardhi kitapimwa na mwananchi kupewa hati yake ya umiliki, naamini
itaweza kuondoa kabisa migogoro ya nrdhi nchini Tanzania, hongera
Mhe.Lukuvi,” aliongeza Mpoto.
Alisema bado ataendelea kutembea katika maeno mbalimbali ya nchi kwa
ajili ya kukutana na mashabiki wake wa muziki na kuzungumza nao kuhusu
mambo mbalimbali ya nchi na pale ambako ataona kuna haja ya kutoa msaada
atawasiliana wahusika kwaajili ya kutatua kero za wananchi.
Kazi nyingine zilizotekelezwa na programu ya LTSP ni pamoja na
kusimika alama za msingi 54 za mtandao wa kijiodesia katika Wilaya za
Kilombero, Ulanga, Malinyi na Mufindi, Kupima mipaka ya vijiji 121 na
kutatua migogoro 71 ya mipaka ya vijiji iliyodumu kwa muda mrefu,
Kuandaa vyeti vya Ardhi ya Kijiji kwa vijiji 57, Kuandaa mipango ya
Matumizi ya Ardhi ya Vijiji kwa vijiji 53 na Kuchangia katika ujenzi na
ukarabati wa masjala za ardhi na ofisi za vijiji katika vijiji 61.
Viongozi wengi wa Wizara wanaitembelea programu hiyo mara kwa mara na
uongozi wa Wilaya na wananchi wanatoa ushirikiano mkubwa sana kwa kuwa
programu iko katika Wilaya zao.
Hivi karibuni Katibu Mkuu Bibi. Dorothy Mwanyika mara tu baada ya
kuteuliwa na Mhe Rais kuwa Katibu Mkuu wa Wizara alitembelea programu
hiyo na kujionea namna programu inavyotumia teknolojia ya kisasa kabisa
kupima ardhi ya wananchi vijijini. Pia, Mhe Naibu Waziri Mhe. Angelina
Mabula nae alifanya ziara katika eneo la programu.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni