Ikiwa ni siku moja tu ya leo iliyosalia kuelekea mchezo wa Kombe la Shirikisho Afrika kati ya Al Masry SC dhidi ya Simba SC, Kocha wa Al Masry, Hossam Hassan anaamini mtanange huo hautakuwa mrahisi.
Kwa mujibu wa mtandao 'Kingfut.com' Hassan anatarajia upinzani mgumu kesho Jumamosi dhidi ya Simba kuliko hata walipokutana na Green Buffaloes waliyoiondoa kwenye hatua iliyopita kwa mabao 5-2.
"Tulicheza vizuri mechi ya awali na tungeweza kushinda kirahisi, nawaamini wachezaji wangu kwa kiwango walichonacho japo tunapaswa kupambana kwasababu mechi ya kesho itakuwa ngumu" alisema Hossam.
Hossam aliongeza kwa kusema Simba ni klabu kubwa yenye uzoefu kwenye mashindano haya huku akisisitiza lazima wajitume kwenye mchezo huo wa marudiano.
"Simba ni timu kubwa yenye uzoefu kwenye mashindano, ilionesha vile walivyojipanga katika mchezo wa kwanza. Sisi matarajio yetu ni kupambana ili tuweze kushinda" alisema.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni