mwana wa liganga blog ni blog ya kutoa taarifa, matukio, yaliyotokea katika ulimwengu hususani katika nchi yaTanzania blog hii inasimamiwa na mwandishi wa habari kitaaluma bwana Deus Thomas liganga.lengo ni kutoa taarifa kwa umma,kwa maendeleo ya taifa na Dunia kwa ujumla kwa mawasiliano kuhusu mtangazo, habari, wasiliana nasi 0659944423,deusliganga@yahoo.com,mzeeliganga@gmail.com
Ijumaa, 30 Juni 2017
Jeshi la Laua Majambazi wanne Kibiti usiku wa kuamkia leo
Jeshil la Polisi limeua Watu wanne wanaozaniwa kuwa ni majambazi kwenye kijiji cha Pagae , Kibiti Mkoani Pwani
Taarifa iliyotolewa kwa Vyombo vya Habari na DCP Lebaratus Sabas Mkuu wa Opereshini Maalumu ya Jeshi hilo Tanzania ambapo amesema kuwa majambazi hao wameuwa jana Majira ya Usiku
kwenye barabara inayotoka Pagae kuelekea Nyambunda.
taarifa hiyo ya DCP Sabas inasema kuwa Askari Polisi wakiwa doria walikutana na kikundi cha watu kinachokadiriwa kuwa na watu sita wakitokea barabara kuu ya lami wakifuata barabara hiyo inayoelekea Nyambunda kilomita 100 kutoka barabara kuu.
"Watu hao walipogundua kuwa watu waliokuwa mbele yao ni Askari Polisi walikimbia vichakani na ghafla wakaanza kuwashambulia askari kwa risasi.
Askari Polisi walijibu mapigo na kuanza kupambana na watu hao. "
Katika mapambano hayo askari Polisi walifanikiwa kuwajeruhi kwa risasi watu wanne katika kundi hilo la wahalifu hao.
Aidha katika mapambano hayo zilipatikana silaha mbili aina ya Smg na magazine mbili pamoja na risasi 17 zilizokuwa zinatumiwa na wahalifu hao.
Watu hao wanne ambao wanasadikiwa kuwa miongoni mwa wahalifu wanaendesha vitendo vya mauaji katika wilaya za Mkoa wa Pwani.
Majeruhi hao walifariki dunia wakiwa njiani kupelekwa hospitali kutokana na kuvuja damu nyingi zilizotokana na majeraha ya risasi waliyopata, milli ya marehemu imehifadhiwa katika hospitali ya Taifa Muhimbili.
Jeshi la Polisi linaendelea kutoa wito kwa wananchi kutoa taarifa kwa Jeshi la Polisi zitakazosaidia kuwakamata watu wanaojihusisha na vitendo hivi vya kihalifu kwenye wilaya za Mkoa wa Pwani.
Taarifa iliyotolewa kwa Vyombo vya Habari na DCP Lebaratus Sabas Mkuu wa Opereshini Maalumu ya Jeshi hilo Tanzania ambapo amesema kuwa majambazi hao wameuwa jana Majira ya Usiku
kwenye barabara inayotoka Pagae kuelekea Nyambunda.
taarifa hiyo ya DCP Sabas inasema kuwa Askari Polisi wakiwa doria walikutana na kikundi cha watu kinachokadiriwa kuwa na watu sita wakitokea barabara kuu ya lami wakifuata barabara hiyo inayoelekea Nyambunda kilomita 100 kutoka barabara kuu.
"Watu hao walipogundua kuwa watu waliokuwa mbele yao ni Askari Polisi walikimbia vichakani na ghafla wakaanza kuwashambulia askari kwa risasi.
Askari Polisi walijibu mapigo na kuanza kupambana na watu hao. "
Katika mapambano hayo askari Polisi walifanikiwa kuwajeruhi kwa risasi watu wanne katika kundi hilo la wahalifu hao.
Aidha katika mapambano hayo zilipatikana silaha mbili aina ya Smg na magazine mbili pamoja na risasi 17 zilizokuwa zinatumiwa na wahalifu hao.
Watu hao wanne ambao wanasadikiwa kuwa miongoni mwa wahalifu wanaendesha vitendo vya mauaji katika wilaya za Mkoa wa Pwani.
Majeruhi hao walifariki dunia wakiwa njiani kupelekwa hospitali kutokana na kuvuja damu nyingi zilizotokana na majeraha ya risasi waliyopata, milli ya marehemu imehifadhiwa katika hospitali ya Taifa Muhimbili.
Jeshi la Polisi linaendelea kutoa wito kwa wananchi kutoa taarifa kwa Jeshi la Polisi zitakazosaidia kuwakamata watu wanaojihusisha na vitendo hivi vya kihalifu kwenye wilaya za Mkoa wa Pwani.
Ni marufuku matangazo kwenye miito ya simu- TCRA
Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA), imepiga marufuku matangazo ya
biashara yanayowekwa mtumiaji anapopiga simu ili kutoa fursa kwa
watumiaji kupata mawasiliano bila usumbufu.
Mkurugenzi wa TCRA, Mhandisi James Kilaba amesema leo (Ijumaa) kuwa
mamlaka hiyo imepokea malalamiko mengi kutoka kwa watumiaji wa simu
wakilalamikia matangazo hayo yanayotolewa na kampuni za simu.
Amesema tayari TCRA imeshaziandikia barua kampuni zote za simu kusitisha
matangazo hayo na itakutana nazo kwa majadiliano ya kina Julai 6.
Amesema mamlaka haitambui utaratibu huo na inauchukulia kama kero kwa
watumiaji wa simu ambao hutegemea kutumia njia hiyo ya mawasiliano
kurahisisha mambo.
“Tuna imani mtu anapopiga simu ana shida ya haraka na anahitaji afanye
mawasiliano, unapomuwekea matangazo kwa dakika tatu au nne ni usumbufu,”
amesema.
Katika siku za karibuni imekuwa ni kawaida kwa mtu anayepiga simu
kusikiliza wimbo au matangazo ya biashara na baadaye kuambiwa namba
anayopiga haipatikani.
Kutoka Simba kuhusu Rais wao na Makamu kuwa rumande
Hakimu Victoria Nongwa aliamua kuiarisha kesi hiyo hadi July 13 ndio itasikilizwa tena, huku Aveva na Kaburu wakirudishwa rumande, Simba leo wametoa taarifa kuwa kamati ya utendaji ya club hiyo itakutana kesho July 1 kwa ajili ya kikao ambacho kitaangalia shughuli za club zisikwame.
Amuua mpenziwe kwa ''mzaha'' katika YouTube
Mwanamke mmoja mjini Minesesotta
nchini Marekani amehukumiwa kwa kumpiga risasi na kumuua mpenzi wake
katika kile kinachosemekana ni mgogoro wa mtandaoni.
Monalisa
Perez mwenye umri wa miaka 19 aliwekwa kizuizini baada ya kumpiga risasi
Pedro Ruiz alipokuwa akshikilia kitabu katika kifua chake akidhani
kitazuia risasi hiyo.Wawili hao wana mtoto wa miaka mitatu na takriban watu 30 walikuwa wakiangalia video hiyo ya YuTube alipompiga risasi mpenziwe.
Shangazie Ruiz anasema kuwa walifanya kitendo hicho ili kuimarisha ufuasi wao katika katika mitandao ya kijamii.
Claudia Ruiz aliambia runinga ya WDAY-TV kwamba binamu yake alimwambia kwamba alitaka kufanya kitendo hicho '' kwa sababu walihitaji kupata wafuasi zaidi''. ''tunataka kuwa maarufu''.
''Aliniambia kuhusu wazo hilo na nikamwambia'',''Musafanye hivyo''.
''Kwa nini utumie bunduki? Kwa nini?'', Claudia Ruiz aliambia chombo hicho cha habari.
''Walikuwa wakipendana sana'',alisema.''ulikuwa mzaha uliofanyika kimakosa''.
chanzo na bbc
Fahamu Mambo muhimu kuhusu Treni za umeme zinazoletwa Tanzania ingia hapa
Rais JPM April 12, 2017 alizindua ujenzi wa reli ya kisasa ‘standard gauge’ kutoka DSM hadi Mwanza ambayo itakamilika Oct 2019 jambo lililozua gumzo kwa baadhi ya Wananchi wakiwa na wasiwasi kuhusu train hizo kutokana na tatizo la umeme.
Mhandisi wa Miundombinu ya Reli ambaye pia ni Mkuu wa Mradi huu Maizo Mgeni kutoka Kampuni inayojihusisha na ujenzi wa reli Tanzania RAHCO na kuelezeea mambo makubwa manane yanayohusiana na Standard Gauge.
Mambo manane hayo ni:
1: Treni itakuwa inasimama kwenye vituo sita kutoka Dar es Salaam hadi Morogoro ambapo itasimama Pugu, Soga, ruvu, Stesheni ya Ngerengere na mwisho Treni itasimama Morogoro.
2: Kutokana na Treni kutumia umeme Serikali imejipanga kutoa umeme wa uhakika kwa 100% na wananchi wasiwe na shaka yoyote kwani umeme wa Treni hujengewa nyaya zake maalum zinazotofautiana na nyaya za umeme wa kawaida.
3: Treni hii itakuwa na uwezo wa kusafirisha wagonjwa mahututi kwani ni za kisasa na zina mwendo wa haraka ambapo itatumia saa moja na nusu kutoka Morogoro hadi Dar es Salaam.
4: Umeme utatumia vyanzo vyenye nguvu kutoa umeme wa Treni kama vyanzo vya maji na makaa ya mawe.
5: Kwa tathmini ya sasa nauli ya Treni hizi haitokuwa sawa na Treni za mita kwani ni Treni zinazotumia teknolojia kubwa na za kisasa, hivyo nauli itakuwa juu zaidi ya Treni za kawaida.
6: Treni haitosimama kama umeme kutoka Tanesco ukikatika ghafla.
7: Kiwango cha nauli kwa wanafunzi bado kinafanyiwa kazi.
8: Kwa sasa watu binafsi hawataruhusiwa kuwa na Treni binafsi kwani Shirika la Reli ndilo litakuwa msimamizi mkuu.
CHANZO MITANDAO.
JPM abadili ratiba za Ufunguzi wa Sabasaba
Rais John Pombe Magufuli atafungua rasmi maonyesho ya 41 ya Kimataifa ya Biashara maarufu kama Sabasaba kesho saa 4 asubuhi badala ya saa 8 mchana kama ilivyotangazwa awali.
Waziri wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji, Charles Mwijage amesema mabadiliko hayo yamekuja leo (Ijumaa) baada ya wizara kupokea maombi ya Mhamasishaji Mkuu wa Viwanda ambaye ni Rais Magufuli.
“Rais Magufuli amesema anataka kuzunguka kwenye mabanda ya wajasiriamali wadogo na kuwauliza wafanyabiashara wakubwa kama na wao walianza kwa mitaji midogo,” amesema Mwijage.
Lowassa: Demokrasi imeshaanza na Itaendelea....Hakuna wa kuizuia
Waziri Mkuu wa zamani, Edward Lowassa, amesema gurudumu la demokrasia limekwisha kuanza nchini hivyo ni vigumu kulizuia.
Lowassa
ambaye pia ni mjumbe wa Kamati Kuu ya Chadema, alirejea Makao Makuu
ya Polisi Dar es Salaam jana baada Juni 27 kuhojiwa na Ofisi ya
Mkurugenzi wa Upelelezi wa Makosa ya Jinai (DCI).
Alihojiwa
kwa takriban saa nne juu ya kauli alizozitoa kuhusu viongozi wa dini wa
kundi la Uamsho na akatakiwa kurudi jana saa 6.00 mchana.
Akizungumza
ofisini kwake Mikocheni, Lowassa alisema baada ya kuitikia wito wa
polisi jana, hakuna mengi aliyoambiwa zaidi ya kuelezwa kuwa upelelezi
wa suala hilo unaendelea hivyo arejee ofisini hapo Julai 13.
Alipoulizwa analichukuliaje suala hilo la kutakiwa kwenda polisi mara kwa mara alisema: “Njoo kesho, njoo kesho kutwa ni sehemu ya kazi yao (polisi).
“Kuhusu maoni yangu nitawaambia baada ya kumaliza hili, isionekana naingilia.
“Lakini nieleze jambo moja, demokrasia ikishaanza kuizuia ni taabu sana.
“Unaweza ukapunguza spidi ya gurudumu la demokrasia lakini huwezi kuiondoa, demokrsia imeshaanza, inaendelea, ni vigumu kuizuia.
“La
pili, nichukue nafasi hii kuwaomba wanachama wa chama chetu na wananchi
na wanaotutakia mema wasiwe na shaka kila kitu kipo chini ya utaratibu
mzuri.
“Tuko
sawasawa, tuko sahihi na tunatekeleza kama alivyosema (Mwenyekiti
Chadema, Freeman Mbowe). Tunatekeleza sera ya chama chetu, wasiogope
wawe na amani, watulie,” alisema Lowassa.
Alivyoulizwa kama wakati anatoa kauli kuhusu viongozi hao wa Uamsho labda aliteleza, Lowassa alisema, “I stand by what I said” (naisimamia kauli yangu).
Alisema anaamini alichosema ni sahihi kama alivyoeleza Mbowe na kwamba suala la msingi ni kuachiwa kwa Masheikh wa Uamsho.
Lowassa
alisema Chadema kama chama hakisemi kama viongozi hao wa dini wana
makosa ama hawana, ila wamekaa ndani kwa muda mrefu bila kesi zao
kusikilizwa.
“Wamekaa
vya kutosha, hilo ndilo la msingi tunaloomba… katika hotuba yangu
nilisema na kwenye magazeti waliandika vizuri, wale walioko madarakani
wana mamlaka.
“Mtu mwenye dhamana ya kuwatoa ni Rais. Nikawaeleza wajipange wakaongee na Rais wamwambie ‘mzee, wenzetu tunaomba waachiliwe’.
“Mwenye
madaraka ya mwisho ni Rais, mkiendelea na mahakama miaka minne, nane
siyo… kwa hiyo narudia, ni vema wakamuombe Rais awaachilie.
“Sintoshangaa
akitekeleza (akawaachia) kwa sababu juzi ametekeleza moja ya uamuzi
wetu wa kuunda tume ya kuchunguza madini, tulivyokuwa Kahama tulisema
tutaunda tume.
“Waendelee na uchunguzi wao (juu ya kauli yake), lakini narudia, gurudumu la demokrasia likianza kulizuia ni taabu sana.
“Narudia mwenye mamlaka ya mwisho kuombwa na kushawishiwa ni Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,”alisema Lowassa.
RC Anna Mghwira ashuhudia magari 103 yakiwa na shehena ya mahindi njia panda ya Himo
ENEO la njia Panda linalounganisha barabara za Moshi/Arusha,Tanga/Dar es Salaam na ile ya Holili
mpakani mwa nchi jirani ya Kenya linatajwa kama kituo kikuu cha Malori yanayosafirisha Nafaka kwenda nchi jirani ya Kenya.
Uchunguzi uliofanywa umebaini kuwepo kwa maeneo yasiyo rasmi ya kuegesha Malori hayo ,mengine yakiwa na Matela yake ,ambako shughuli za kupakua mahindi na kupakia katika Magari Madogo aina ya fuso zinazotoka nchi jirani ya Kenya hufanyika.
Maeneo mengine yanayotajwa kuwepo na Magulio ya Mahindi ni katika sehemu za maegesho ya magari zilizopo katika vituo mbalimbali vya kuuza Mafuta ,pamoja na baadhi ya nyumba za wageni ambazo zimegeuzwa Maghala ya kuhifadhia Mahindi.
Magari zaidi ya 103 yanashikiiwa katika maeneo ya Njia Panda na Himo yakiwa yamebeba Shehena ya Mahindi tayari kusafirishwa huku baadhi ya madereva wakiyatelekeza Malori yao kwa siku ya tano sasa na kwenda kusiko julikana .
Hatua iliwasukuma Wafanyabiashara wa Mahindi pamoja na Madereva kufika ofisi za Mkuu wa mkoa kuwasilisha malalamiko yao juu ya kukamatwa kwa Malori hayo yakiwa Njia Panda badala ya mpakani kama alivyo agiza Waziri Mkuu,Kassim Majaliwa.
Wakizungumza nje ya jingo la ofisi ya Mkuu wa Mkoa,Wafanyabiashara hao ,Laurance Kanyota,Nuru Madai na Mariam Ramadhan walisema wameshangazwa na hatua ya jeshi la Polisi kushikilia magari yao yalikuwa na Mahindi yakisafirishwa kuelekea mikoa ya Arusha na Moshi.
“Magari yetu yapo pale Sheli Maount Meru,yalitokea Tunduma kwenda Arusha,yalipofika pale siku ya Jumamosi madereva walienda kula siku kuu ya Idd,jana (Juzi) asubuhi Matandiboi wakapiga simu kwamba tumezungukwa na Polisi ,tukaenda pale tukaonana na OCD tukaliza kwanini mnatushikia magari ambayo yako Njia Panda yanayoenda Arusha au Moshi ,wakajibu tumetumwa kushika magari yote ya Mahindi.”alisema Mfanyabiashara Mariam.
Mwalimu Afumaniwa Akifanya Mapenzi na Mwanafunzi Darasani
Mkuu
wa Wilaya ya Wanging'ombe, Mkoani Njombe, Ally Kasinge ameagiza
kushikiliwa kwa Makamu Mkuu wa shule ya sekondari Wanike, iliyopo katika
wilaya hiyo baada ya kukamatwa akifanya mapenzi na mwanafunzi wake
darasani usiku.
Kasinge
ametoa agizo hilo baada ya kuwepo taarifa ya kuwepo kwa watu wanaotaka
kumsaidia mwalimu huyo kuvuruga ushahidi kwa kupanga na wanafunzi wenye
ushahidi huo kuongea tofauti na tukio.
"Kuanzia
wanafunzi waliotimuliwa wahojiwe na polisi na wale wanafunzi wengine
waliotajwa pia wahojiwe na polisi na mwalimu mwenyewe pia aendelee
kushikiliwa .Huyo ambaye anatuhumiwa aendelee kushiliwa na polisi mpaka
tupate majibu, kwa sababu akibaki nje ataendelea kutengeneza mazingira
ya kutengeneza mtandao wa kutaka kumsaidia na kupotosha ushaidi" alisema Mkuu wa Wilaya Ally Kasinge
Mbali
na hilo shule ya sekondari ya Wanging'ombe pamoja na Wanike
zimepandishwa hadhi na sasa zitapokea wanafunzi wa kidato cha tano,
walimu wa shule hizo wameweka wazi kuwa shule hizo zinachangamoto ya
walimu wa sayansi ambao ni wachache ukilinganisha na walimu wa masomo ya
sanaa.
Jumatano, 28 Juni 2017
Mwanamke raia wa China azirai baada ya kuvunja bangili ya dola 44,000
Mwanamke mmoja raia wa China
alizirai akiwa kwenye duka la kuuza vito vya thamani baada ya kuvunja
kimakosa bangili ghali ya thamani ya dola 44,000
Mtalii huyo
kutoka mkoa wa Jiangxi, alikuwa akijaribu kuvaa bangili hiyo kwenye duka
moja lililo mkoa wa Yunnam karibu na mpaka na Myanmar.Alipoambiwa thamani na bangili hiyo aliifua kwa haraka lakini ikaanguka kimakosa,
Hakuna makubaliano yameafikiwa kuhusu vile bangili hiyo itafidiwa.,
Wafanyakazi wa duka walijaribu kumtuliza baada ya kisa lakini mara alianza kutokwa na jasho na kisha akazirai.
Alipata nafuu wakati wateja wangine ambao walikuja kumsaidia walipomfinya pua lake.
Wafanyakazi wa duka walimwambia alipe dola 25,000 ili kutatua suala hilo lakini akasema alikuwa na dola 1,500 tu.
Polisi walishindwa kushawishi pande zote kuafikia makubaliano na suala hilo huenda likaelekea mahakamani.
Chama kimoja cha kuuza vito vya thamani kilisema kuwa bangili hiyo ni ya thamani ya dola 26,000.
Marekani: Ujenzi wa jiwe la amri 10 za Mungu wapingwa
Wanaharakati katika jimbo la Arkansas nchini Marekani, wanapinga ujenzi wa jiwe moja kubwa lililo na maandishi ya amri 10 za Mungu, kwenye uwanja wa makao makuu ya bunge la jimbo hilo.
Wanasiasa walipitisha kauli ya ujenzi wa mnara huo wa jiwe wenye urefu wa futi sita, katika eneo la Little Rock mnamo mwaka wa 2015.
Muungano wa haki na uhuru wa raia nchini Marekani ACLU, umewasilisha kesi mahakamani kutaka kuondolewa mara moja kwa mnara huo, ukisema kuwa unaleta mgawanyiko na unakiuka ahadi ya uhuru wa kidini kwa wote, katika katiba ya Marekani.
Seneta wa chama tawala cha Republican, Jayson Rapert, ambaye alikuwa katika mstari wa mbele wa kutaka kuwekwa kwa jiwe hilo , alisema kuwa hatua hiyo inaenda sambamba na msimamo wa mahakama kuu ya Marekani, na hivyo ni jambo zuri kwa jimbo la Arkansas.
Jengo lateketea kwa moto Dar
Jengo moja lililopo mtaa wa India jirani na Sabodo Parking Tower jijini Dar es salaam limeshika moto mchana huu ambapo vikosi vya zimamoto vimefika eneo la tukio na kufanikiwa kuuzima. Chanzo na madhara yaliyotokana na moto huo bado kujulikana
Rayvanny Awasili, Apokelewa na Mafuriko
Msanii wa kizazi kipya, Rayvanny aliyeshinda tuzo ya BET kipengele cha International Viewers Act 2017, amewasili alasiri hii katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere (JNIA)
Rayvanny alipata tuzo hiyo nchini Marekani Juni 25 na kuwa msanii wa kwanza kushinda tuzo hizo kubwa.
Rayvanny ameambatana na Babutale ambaye ni mmoja wa mameneja wa Kundi la WCB.
Uwanjani hapo Kulifulika Mashabiki wa Msanii huyo walikuja Kumla
Wabunge wanawake watengewa chumba maalum cha kunyonyeshea
Bunge
limetenga chumba maalum kwa ajili ya wabunge wenye watoto wachanga
kunyonyesha watoto wao wakati vipindi vya bunge vinaendelea.
Uamuzi
huo umetangazwa leo (Jumatano) bungeni na Naibu Spika Dk Tulia Ackson
mara baada ya kipindi cha maswali na majibu bungeni.
"Ofisi ya Bunge inataarifu kuwa imetenga chumba maalum kwa ajili ya kunyonyeshea kwa wabunge wenye watoto wachanga,"amesema.
Amewasihi
wabunge wenye watoto wachanga kuwanyonyesha watoto wao angalau miaka
miwili kama inavyoshauriwa na Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii,
Jinsia, Wazee na Watoto.
Mtoto wa miaka mitano abakwa Mwanza
Mtoto mmoja mwenye umri wa miaka mitano anasadikiwa kubakwa katika eneo la Kabuholo kata ya Kirumba wilayani Ilemela ijini Mwanza na kijana mmoja ambaye jina lake limehifadhiwa kisha kutokomea kusikojulikana.
Wakizungumzia
tukio hilo baadhi ya wananchi katika eneo la tukio wamesikitishwa na
kitendo hicho cha kikatili dhidi ya mtoto huyo.
“Kitendo
cha kikatili jamani kwani sisi wakazi wa Mwanza tumekumbwa na nini
hatuelewi kwani vitendo vya kinyama vimeshamiri tofuati na miaka ya
zamani,” walisema Wananchi.
Kwa
upande wake Kamanda wa Jeshi la Polisi mkoani Mwanza, Ahmed Msangi
amesema kuwa kutokana na kijana huyo kufanya unyama huo kisha kutokomea
kusikojulikana amesema jeshi la polisi linaendelea kumtafuta mtuhumiwa
huyo na kwamba atakapokamatwa sheria itafuata mkondo wake.
Kamanda Msangi amewataka wananchi kutoa ushirikiano kwa jeshi la polisi ili kuhakikisha mtuhumiwa huyo anatiwa nguvuni.
Mbunge mwingine CHADEMA asimamishwa kuhudhuria vikao vya Bunge
Siku kadhaa zilizopita kutoka Bungeni Dodoma Wabunge wa CHADEMA Halima Mdee wa Kawe na Ester Bulaya wa Bunda Mjini walisimamishwa kutohudhuria vikao vya Bunge, leo June 28, 2018 Mbunge Conchesta Rwamlaza wa Viti Maalum CHADEMA amesimamishwa.
Conchesta Rwamlaza amesimamishwa kutohudhuria Vikao vitatu vya Bunge linaloendelea kwa kosa la kusema uongo mbele ya Bunge akimtuhumu Mbunge wa Muleba Kusini Prof. Anna Tibaijuka kujimilikisha ardhi yenye ukubwa wa ekari 400 kinyume cha sheria taarifa ambazo sio za kweli.
Aidha, Kamati ya Haki, Maadili na Madaraka ya Bunge imetoa msamaha kwa Mbunge wa Arumeru Mashariki Joshua Nassari kwa kosa alilolifanya May 30, 2017 kudharau mamlaka ya Spika ikiwemo kupiga kelele Bungeni na kutupa karatasi ovyo.
Nassari amepata msamaha huo kwa kuwa imeonesha ni mara yake ya kwanza kutenda kosa kama hilo kisha kupelekwa mbele ya Kamati.
Nchi 33 kushiriki maonesho ya sabasaba yanayoanza kesho
Nchi 33 pamoja na taasisi na kampuni zaidi ya 2800 zimethbitisha
kushirikimaonesho ya 41 biashara ya kimataifa ya Dar es Salaam maarufu
kama sabasaba yatakayoanza kesho jijini Dar es Salaam katika viwanja vya
mwalimu Julius Nyerere.
Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam, Waziri wa
Viwanda, Biashara na uwekezaji Charles Mwijage amesema katika maonesho
ya mwaka huu kumekuwa na maboresho kadhaa ikiwemo kufungwa Camera maalum
za ulinzi.
Mmoja kati ya washiriki wa maonesho hayo kutoka wizara ya fedha na
mipango ambaye ni msemaji wa wizara hiyo Ben Mwaipaja amesema wizara
hiyo na taasisi zilizo chini yake zimepanga kuyatumia maonesho hayo
kutoa elimu kwa jamii.
News Alert: Rais wa TFF na katibu wake wakamatwa
Taarifa iliyotufikia asubuhi hii inaeleza kuwa, Rais wa Shirikisho la Soka nchini, Jamal Malinzi na Katibu Mkuu wake, Selestine Mwesigwa wanashikiliwa na Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) na wapo katika Kituo cha Polisi Salander Bridge ili kupisha uchunguzi dhidi yao. hilo limethibitisha na Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano wa Takukuru, Mussa Misalaba alipokuwa akihojiwa na kituo cha Radio EFM leo. Misalaba amesema ni kweli wanawashikilia na taarifa zaidi wataitoa baada ya kumaliza uchunguzi wao, kwa sasa ifahamike kuwa viongozi hao wanawashikilia.
Mapacha wafa maji, mama ajitupa baharini siku ya Eid
MAPACHA wawili waliokuwa wakiishi kata ya Kashai katika Manispaa ya Bukoba mkoani Kagera walikufa maji juzi kwenye ufukwe za Ziwa Victoria wakati wakiogelea kusherehekea Eid, katika siku ambayo mama mmoja alijitupa baharini kutoka kwenye pantoni Feri, jijini Dar es Salaam kwa wivu wa mapenzi.
Kamanda wa Polisi mkoa wa Kagera, Agustino Ollomi alithibitisha kutokea kwa tukio hilo.
Kamanda Ulomi alisema juzi majira ya saa 11:30 jioni, mapacha hao walikuwa wakiogelea ziwani katika eneo la Kiloyela lililopo katika Manispaa ya Bukoba mkoani humo.
Marehemu mapacha hao walitajwa kuwa ni Hussein Hamis (12) na Hassan Hamis(12), na kwamba walikuwa wanafunzi wa darasa la saba katika Shule ya Msingi Kashai.
“Watoto hao walikuwa wa askari mwenzetu(wa) kitengo cha Usalama Barabarani," alisema Kamanda Ollomi na kwamba "walikuwa wakisoma darasa la saba.”
Alisema sababu ya kifo cha marehemu hao ni kuzidiwa na nguvu ya maji na kupelekea kuzama ambapo waliopolewa wakiwa wamefariki.
"Watoto wenzao baada ya kuona wenzao wakiendelea kuzama walipiga kelele ili kuomba msaada, lakini jitihada za kuwaokoa wakiwa hai zilishindikana," alisema.
"Tayari watoto hawa wamezikwa Juni 27 mwaka huu (jana) katika makaburi ya Kishenge, yaliyoko katika Manispaa ya Bukoba.
“Tunaendelea kuwasihi wazazi, kuendelea kuangalia usalama wa watoto wao hasa katika siku za sikukuu ili kuepusha madhara kama haya."
Jijini Dar es Salaam, mwanamke aitwaye Asha Yahya(30), mkazi wa Zanzibar anadaiwa kujirusha baharini akiwa katika kivuko cha MV Magogoni kwa lengo la kujiua, lakini wananchi waliwahi kumuokoa.
Kamanda wa Polisi mkoa wa Kipolisi Temeke, Andrew Satta alisema tukio hilo lilitokea majira ya 2:10 asubuhi wakati akitokea Kigamboni kuelekea Ilala na kwamba sababu za kutaka kujiua ni wivu wa kimapenzi.
"Baada ya kumhoji alituambia kwamba sababu ya kutaka kujiua, eti mume wake anataka kuoa mwanamke mwingine," alisema Satta.
Katika tukio jingine katika kipindi cha sikukuu, Jeshi la Polisi jana liliokota mwili wa mtumishi wa Mamlaka ya Bandari (TPA), Masoud Abdulrahman(27) katika ufukwe wa Kisiwa cha Mbutu, kilichopo Kigamboni.
Kamanda Satta alisema marehemu kabla ya kukutwa na umauti huo alikuwa na wafanyakazi wenzake 20 ambao walikwenda katika ufukwe huo kwa ajili ya kufurahia sikukuu ya Eid, lakini wakati wakiogelea wimbi kubwa la maji liliwapiga na hivyo wote kupotea.
Alisema hata hivyo, baada ya Jeshi la Polisi kufanya msako baada ya kugundua kwamba kuna watu waliosombwa na maji, waliwapata wenzake 20 ambao waliokolewa na kukimbizwa hospitali.
Kwa upande wa mkoa wa kipolisi wa Ilala, mtu mmoja ambaye jina lake halikujulikana mara moja aligongwa na basi la mwendokasi katika Barabara ya Uhuru na kufariki papohapo juzi pia.
Kamanda wa Polisi wa Ilala, Salum Hamdani, alisema mtu huyo aligongwa na gari hilo baada ya kuingilia barabara ya mwendokasi na kwamba mwili wa marehemu umehifadhiwa katika Hospitali ya Taifa Muhimbili.
Kibiti: Wawili wauawa kwa kupigwa risasi
Kibiti. Watu wawili wameuawa kwa kupigwa risasi katika kijiji cha Mangwi kilichopo Kata ya Mchukwi wilayani Kibiti usiku wa kuamkia leo (Jumatano).
Waliouawa wametajwa kuwa ni Mtendaji wa kijiji hicho, Shamte Makawa na mwenyekiti wa Kitongoji cha Mangwi, Maiko Nicholaus.
Habari za awali zinaeleza maiti ya mwenyekiti huyo wa kitongoji bado haijaonekana na nyumba zao zimechomwa moto.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Pwani, Onesmo Lyanga amekiri kutokea kwa mauaji hayo.
Amesema polisi wameenda eneo la tukio kwa ajili ya ufuatiliaji na ukaguzi.
chanzo na muungwana blog
je wajua?: Ndege kubwa kuwahi kutengenezwa duniani ingia hapa
Ndege ni chombo cha usafiri unaotumika kusafirisha au kwa ajili ya
shughuli mbalimbali kutumia anga. Ikiwemo vita, fahamu ndege kumi
zilizowahi kutumika katika vita kuu ya kwanza ya dunia na vita ya pili
kuu ya dunia.
Ndege kubwa zaidi wakati wa Vita Vikuu vya Kwanza vya Dunia ilikuwa Zeppelin-Staaken R.VI, ndege ambayo ilizifanya ndege za wakati huo zionekane kama mifano tu ya ndege. (Picha: San Diego Air and Space Museum)
Ndege nyingine kubwa kutoka Ujerumani ilikuwa Dornier Do X, ilifanana na meli na ilikuwa injini 12. Iliweza kubeba abiria hadi 100. Ilikuwa na uzani wa tani 56. (Picha: Bundesarchiv)
ANT-20 iliyoundwa na Tupolev ilitumiwa kama chombo cha propaganda, ilikuwa na kituo cha redio, ukumbi wa sinema na chumba cha kutoleshea picha. Ilikuwa na injini kubwa juu ya mgongo wa ndege kuiwezesha kupaa. (Picha: Wikimedia Commons)
Ndege kubwa zaidi wakati wa Vita Vikuu vya Pili vya Dunia ilikuwa B-29 iliyoundwa na Boeing. Ndiyo iliyoangusha mabomu ya atomiki Japan. Ilifungua ukurasa mpya wa ndege za kuangusha mabomu za kusafiri masafa marefu.
H-4 Hercules iliyoundwa na Howard Hughes ina mabawa marefu zaidi duniani kuliko ndege nyingine yoyote. Hata hivyo ilipaa angani mara chache tu.
Convair B-36 Peacemaker ilikuwa ndege ya kwanza duniani ya kuangusha mabomu kuweza kusafiri kutoka bara moja hadi bara jingine. Ilitumiwa injini kadha za jeti na rafadha kadha kuweza kupaa. (Picha: Clemens Vaster)
B-52 Stratofortress iliyoundwa na Boeing inasalia kuwa moja ya ndege kubwa zaidi kuwahi kuundwa duniani. Ilitumia injini nane kubwa. (Picha: Getty Images)
Tu-160 ya Tupolev ingeweza kubeba jumla ya tani 275 ikipaa, na ilikuwa na mabawa makubwa zaidi yaliyoweza kujipinda kuwahi kuundwa.
Ingawa Boeing 747 ilikuwa ndege ya kwanza kuitwa Jumbo Jet, A380 ya Airbus ni kubwa kuliko Boeing 747. Ndege hii inaweza kuwabeba watu 850.
Ndege kubwa zaidi kuwahi kuundwa duniani ni An-225 ya Antonov ambayo ina injini sita na urefu wake ni mita 84. Ndege hii ina uwezo wa kubeba karibu tani 250
chanzo cha habari mitandao mbalimbali.
Ndege kubwa zaidi wakati wa Vita Vikuu vya Kwanza vya Dunia ilikuwa Zeppelin-Staaken R.VI, ndege ambayo ilizifanya ndege za wakati huo zionekane kama mifano tu ya ndege. (Picha: San Diego Air and Space Museum)
Ndege nyingine kubwa kutoka Ujerumani ilikuwa Dornier Do X, ilifanana na meli na ilikuwa injini 12. Iliweza kubeba abiria hadi 100. Ilikuwa na uzani wa tani 56. (Picha: Bundesarchiv)
ANT-20 iliyoundwa na Tupolev ilitumiwa kama chombo cha propaganda, ilikuwa na kituo cha redio, ukumbi wa sinema na chumba cha kutoleshea picha. Ilikuwa na injini kubwa juu ya mgongo wa ndege kuiwezesha kupaa. (Picha: Wikimedia Commons)
Ndege kubwa zaidi wakati wa Vita Vikuu vya Pili vya Dunia ilikuwa B-29 iliyoundwa na Boeing. Ndiyo iliyoangusha mabomu ya atomiki Japan. Ilifungua ukurasa mpya wa ndege za kuangusha mabomu za kusafiri masafa marefu.
H-4 Hercules iliyoundwa na Howard Hughes ina mabawa marefu zaidi duniani kuliko ndege nyingine yoyote. Hata hivyo ilipaa angani mara chache tu.
Convair B-36 Peacemaker ilikuwa ndege ya kwanza duniani ya kuangusha mabomu kuweza kusafiri kutoka bara moja hadi bara jingine. Ilitumiwa injini kadha za jeti na rafadha kadha kuweza kupaa. (Picha: Clemens Vaster)
B-52 Stratofortress iliyoundwa na Boeing inasalia kuwa moja ya ndege kubwa zaidi kuwahi kuundwa duniani. Ilitumia injini nane kubwa. (Picha: Getty Images)
Tu-160 ya Tupolev ingeweza kubeba jumla ya tani 275 ikipaa, na ilikuwa na mabawa makubwa zaidi yaliyoweza kujipinda kuwahi kuundwa.
Ingawa Boeing 747 ilikuwa ndege ya kwanza kuitwa Jumbo Jet, A380 ya Airbus ni kubwa kuliko Boeing 747. Ndege hii inaweza kuwabeba watu 850.
Ndege kubwa zaidi kuwahi kuundwa duniani ni An-225 ya Antonov ambayo ina injini sita na urefu wake ni mita 84. Ndege hii ina uwezo wa kubeba karibu tani 250
chanzo cha habari mitandao mbalimbali.
Kampuni ya Google yapigwa faini ya dola bilioni 2.7
Google imepigwa faini ya dola bilioni 2.7 na tume ya ulaya baada ya tume hiyo kudai kuwa kampuni hiyo ilikuwa imekiuka mamlaka yake ya kuweka matangazo yake binafasi kuwa ya kwanza.
Faini hiyo ndiyo kubwa zaidi iliyotolewa na tume ya ulaya hadi leo, kwa kampuni ambayo imelaumiwa kwa kukiuka sheria za biashara.
Amri hiyo pia inataka Google kundoa vizingiti vinavyozuia ushindani ndani ya kipindi cha siku 90 la sivyo ichukuliwe hatua zaidi.
Kampuni hiyo ya Marekani inasema huenda ikakata rufaa.
Tume ya Ulaya ilisema inaiachia Google jukumu la kuamua ni mabadiliko yapi itafanyia mifumo yake ya mauzo.
“Kile ambacho Google imekifanya na haramu chini ya sheria za EU,” alisema Margrethe Vestager, kamishina wa ushindanii wa kibiashara wa tume ya EU.
Tume ya Ulaya imekuwa ikichunguza mifumo ya bioshara ya Google tangu mwaka 2010
Mbunifu wa Android azindua simu mpya
Hata hivyo Microsoft hajatoa tamko lolote kufuatia uamuzi huo baada ya mahasimu hao kufikia makubaliano ya kujaribu kuzuia kesi mahakamani siku za usoni.
chanzo bongo 5
Mazishi ya walioungua yafanyika Pakistan
Mazishi ya pamoja yamefanyika
Pakistan baada ya watu 120 kufariki katika ajali ya moto uliolipuka
kutokana na kusuka kwa mpira wa mafuta siku ya Jumapili.
Maombi kwa waliojeruhiwa yalifanyika na kwa waliozikwa pia.Ulinzi uliimarishwa wakati wa mazishi huku watu hao wakizikwa katika makaburi sita ya pamoja yaliyochimbwa katika kijiji cha Bahawalpur.
Waliozikwa katika makaburi hayo ya pamoja ni wale ambao hawakuweza kufahamika kutokana na kuungua vibaya.
Vipimo zaidi vimechukuliwa na iwapo vitaendana na vya ndugu waliopoteza wapendwa wao wahusika watachukua mwili na kwenda kuuzika tena.
CHANZO BBC.
Marekani yachunguza shambulio kubwa la mtandao
Mamlaka nchini Marekani imesema inachunguza shambulio kubwa la kimtandao ambalo limekumba mifumo ya kompyuta duniani kote.
Baraza
la Taifa la Usalama jijini Washington limesema Marekani imedhamiria
kuwachukulia hatua wahusika wa uhalifu huo wa mtandaoni.Mashirika mbalimbali ikiwemo taasisi za kifedha, idara za serikali, makampuni makubwa, na kampuni za usafirishaji ni miongoni mwa zilizoathirika.
Watumiaji wameambiwa komputa zao zimenasa mpaka walipe kiasi cha dola mia tatu katika akaunti isiyofahamika.
Wizara ya mambo ya ndani ya Marekani imewashauri watu wasilipe fedha hizo.
Huku ikisema hakuna uhakika kwamba, mafaili yaliyofungwa yatafunguka baada ya malipo hayo kufanyika.
Shambulio hilo la kimtandao lilianza nchini Ukraine na linaendelea sehemu nyengine duniani.
Timu ya Taifa ya Tanzania Taifa Stars imeshindwa kupata ushindi katika game ya pili ya #COSAFACup2017 vs Angola FT 0-0
Michuano ya COSAFA 2017 bado inaendelea nchini Afrika Kusini kwa michezo ya Kundi A lenye timu za Tanzania, Angola, Mauritius na Malawi kucheza michezo yao ya pili jana.
Tanzania jana imecheza dhidi ya Angola wakati Malawi ambayo ilipoteza mchezo wake wa kwanza dhidi ya Tanzania kwa magoli 2-0, imecheza dhidi ya Mauritius ambayo pia ilipoteza mchezo wa kwanza dhidi ya Angola huku staa wa Tanzania Mzamiru Yassin akiibuka mchezaji bora wa mechi kati ya Tanzania na Angola.
Katika michezo ya jana Tanzania ililazimishwa sare na Angola huku pia Malawi na Mauritius zimemaliza dakika 90 bila kufungana. Kwa matokeo hayo Tanzania bado inaendelea kuongoza Kundi A kwa kuwa na point nne sawa na Angola ila anaongoza kwa tofauti ya magoli. Katika michuano hii timu vinara wa makundi ndio watafuzu kucheza robo fainali.
Jumanne, 27 Juni 2017
Lowassa ahojiwa masaa manne: Kabla ya kuachiwa kwa dhamana
Waziri Mkuu mstaafu, Mh. Edward Lowassa ameachiwa kwa dhamana baada ya kuhojiwa kwa saa manne katika Ofisi ya Mkurugenzi wa Upelelezi wa Makosa ya Jinai (DCI) leo jijini Dar es salaam.
Akizungumza na waandishi wa Habari mapema baada ya mahojiano hayo Mwanasheria wa Chama cha
Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Peter Kibatala amesema Lowassa amejidhamini mwenyewe na ametakiwa kuripoti tena Alhamisi ya wiki hii saa 6.00 mchana.
Kibatala amesema Lowassa amehojiwa kwa kosa la uchochezi na ameandika maelezo ya onyo juu ya kauli aliyoitoa wakati wa futari iliyoandaliwa na mbunge wa Ukonga, Mwita Waitara.
“Mzee amehojiwa kwa kile wanachokiita kauli ya uchochezi aliyoitoa Juni 23, mwaka huu wakati wa futari iliyoandaliwa na Waitara. Baada ya kuhojiwa ameandika Maelezo ya Onyo na atatakiwa kuripoti tena Alhamisi, Juni 29,” amesema Kibatala.
Mourinho awasili Ureno kwa mazishi ya baba yake mzazi
Kocha wa Manchester United, Jose Mourinho tayari ameshafika nchini Ureno kwa ajili ya mazishi ya baba yake mzazi.
Baba yake Mourinho aitwae Jose Manuel Mourinho Felix 79 amefariki Dunia wikiendi iliyopita baada ya kuugua kwa muda mrefu na mazishi yanatarajiwa kufanyika leo huko jijini Setubal nchini Ureno.
Mapema jana Mourinho kupitia ukurasa wake wa Instagram aliweka picha ya baba yake huku ikiwa na rangi nyeusi na nyeupe (B&W) na hakuandika kitu huku maoni ya mashabiki wakionekana kumpa pole kwa msiba uliompata.
MGAO WA VIUADUDU VYA KUTOKOMEZA MBU WA MALARIA LITA 100,000 NCHINI
Tarehe 22 June 2017, Mhe. Dkt.
John Pombe Magufuli Rais wa Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania alilipia
VIUADUDU vya kutokomeza Mbu wa Malaria lita 100,000 na kuagiza
vigawanywe kwenye Halmashauri zote nchini.
Waziri wa Afya,Maendeleo ya
Jamii,Jinsia,Wazee na Watoto Mhe Ummy Mwalimu anapenda kuwatanganzia
Wakurugenzi wa Halmashauri zote nchini kuwa VIUADUDU hivi vitaanza
kugawiwa leo kwa Halmashauri za Mikoa 14 yenye kiwango kikubwa cha
Maambukizi ya Ugonjwa wa Malaria. Mikoa hii (na kiwango cha maambukizi
ya malaria kimeonyeshwa kwenye mabano) ni;- Kagera (41%), Geita (38%),
Kigoma (38%), Ruvuma (23%), Tabora (20%), Mtwara (20%), Mara (19%),
Morogoro (14%), Shinyanga (17%), Lindi (17%), Pwani (15%), Mwanza (15%),
Katavi (14%) na Simiyu (13%),
Mikoa mingine ambayo haijatajwa itagawia Viuadudu katika Awamu ijayo.
Idadi ya Lita zitakazogawanywa kwa kila Halmashauri zilizo katika Mikoa hii tayari imeshaainishwa.
Wizara inawakumbusha Waganga
Wakuu wa Mikoa/Wilaya kufanya Upuliziaji wa Viuadudu kwa kuzingatia
Miongozo ya Wizara ya Afya. Hii itawezesha kupata matokeo tarajiwa ya
kutokomeza mbu ili kudhibiti ugonjwa wa Malaria nchini.
Aidha, Wizara ya Afya inapenda
kumshukuru kwa dhati na kumpongeza Mhe.Rais Dkt. Magufuli kwa kuongeza
chachu katika Mapambano dhidi ya Malaria Nchini.
Imetolewa na;
Catherine Sungura
Kaimu Msemaji- Idara Kuu Afya
26 June 2017
Nje ya Makao Makuu ya Jeshi la Polisi baada ya Lowassa kuripoti
Mjumbe wa Kamati Kuu CHADEMA na Waziri Mkuu wa zamani, Edward Lowassa jana June 26 2017 alipata wito kutoka kwa Mkurugenzi wa Makosa ya Jinai (DCI) kumtaka kufika Makao Makuu ya Jeshi la Polisi kwa ajili ya mahojiano.
Asubuhi ya leo June 27, 2017 majira ya Saa nne Lowassa amefika kuitikia wito huo na hii ni hali ya ulinzi ulivyo nje ya Makao Makuu ya Jeshi hilo.
chanzo millardayo blog.
Jisajili kwenye:
Machapisho (Atom)