Jumatano, 28 Juni 2017

Mtoto wa miaka mitano abakwa Mwanza



 Mtoto mmoja mwenye umri wa miaka mitano anasadikiwa kubakwa katika eneo la Kabuholo kata ya Kirumba wilayani Ilemela ijini Mwanza na kijana mmoja ambaye jina lake limehifadhiwa kisha kutokomea kusikojulikana.

Wakizungumzia tukio hilo baadhi ya wananchi katika eneo la tukio wamesikitishwa na kitendo hicho cha kikatili dhidi ya mtoto huyo.

“Kitendo cha kikatili jamani kwani sisi wakazi wa Mwanza tumekumbwa na nini hatuelewi kwani vitendo vya kinyama vimeshamiri tofuati na miaka ya zamani,” walisema Wananchi.

Kwa upande wake Kamanda wa Jeshi la Polisi mkoani Mwanza, Ahmed Msangi amesema kuwa kutokana na kijana huyo kufanya unyama huo kisha kutokomea kusikojulikana amesema jeshi la polisi linaendelea kumtafuta mtuhumiwa huyo na kwamba atakapokamatwa sheria itafuata mkondo wake.

Kamanda Msangi amewataka wananchi kutoa ushirikiano kwa jeshi la polisi ili kuhakikisha mtuhumiwa huyo anatiwa nguvuni.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni