Jumatano, 28 Juni 2017

Mbunge mwingine CHADEMA asimamishwa kuhudhuria vikao vya Bunge




Siku kadhaa zilizopita kutoka Bungeni Dodoma Wabunge wa CHADEMA Halima Mdee wa Kawe na Ester Bulaya wa Bunda Mjini walisimamishwa kutohudhuria vikao vya Bunge, leo June 28, 2018 Mbunge Conchesta Rwamlaza wa Viti Maalum CHADEMA amesimamishwa.
Conchesta Rwamlaza amesimamishwa kutohudhuria Vikao vitatu vya Bunge linaloendelea kwa kosa la kusema uongo mbele ya Bunge akimtuhumu Mbunge wa Muleba Kusini Prof. Anna Tibaijuka kujimilikisha ardhi yenye ukubwa wa ekari 400 kinyume cha sheria taarifa ambazo sio za kweli.
Aidha, Kamati ya Haki, Maadili na Madaraka ya Bunge imetoa msamaha kwa Mbunge wa Arumeru Mashariki Joshua Nassari kwa kosa alilolifanya May 30, 2017 kudharau mamlaka ya Spika ikiwemo kupiga kelele Bungeni  na kutupa karatasi ovyo.
Nassari amepata msamaha huo kwa kuwa imeonesha ni mara yake ya kwanza kutenda kosa kama hilo kisha kupelekwa mbele ya Kamati.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni