Jumatano, 28 Juni 2017

Timu ya Taifa ya Tanzania Taifa Stars imeshindwa kupata ushindi katika game ya pili ya #COSAFACup2017 vs Angola FT 0-0



Michuano ya COSAFA 2017 bado inaendelea nchini Afrika Kusini kwa michezo ya Kundi A lenye timu za Tanzania, Angola, Mauritius na Malawi kucheza michezo yao ya pili jana.
Tanzania jana imecheza dhidi ya Angola wakati Malawi ambayo ilipoteza mchezo wake wa kwanza dhidi ya Tanzania kwa magoli 2-0, imecheza dhidi ya Mauritius ambayo pia ilipoteza mchezo wa kwanza dhidi ya Angola huku staa wa Tanzania Mzamiru Yassin akiibuka mchezaji bora wa mechi kati ya Tanzania na Angola.
Katika michezo ya jana Tanzania ililazimishwa sare na Angola huku pia Malawi na Mauritius zimemaliza dakika 90 bila kufungana. Kwa matokeo hayo Tanzania bado inaendelea kuongoza Kundi A kwa kuwa na point nne sawa na Angola ila anaongoza kwa tofauti ya magoli. Katika michuano hii timu vinara wa makundi ndio watafuzu kucheza robo fainali.

 

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni