Ijumaa, 30 Juni 2017

Kutoka Simba kuhusu Rais wao na Makamu kuwa rumande


Siku moja baada ya Rais wa club ya Simba Evans Aveva na makamu wake Geofrey Nyange Kaburu kukamatwa na kufikishwa mahakamani kwa tuhuma za makosa matano likiwemo kosa la tuhuma ya utakatishaji fedha ambalo halina dhamana kisheria.
Hakimu Victoria Nongwa aliamua kuiarisha kesi  hiyo hadi July 13 ndio itasikilizwa tena, huku Aveva na Kaburu wakirudishwa rumande, Simba leo wametoa taarifa kuwa kamati ya utendaji ya club hiyo itakutana kesho July 1 kwa ajili ya kikao ambacho kitaangalia shughuli za club zisikwame.

 

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni