Ijumaa, 30 Juni 2017

JPM abadili ratiba za Ufunguzi wa Sabasaba



 Rais John Pombe Magufuli atafungua rasmi maonyesho ya 41 ya Kimataifa ya Biashara maarufu kama  Sabasaba kesho saa 4 asubuhi badala ya saa 8 mchana kama ilivyotangazwa awali.


Waziri wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji, Charles Mwijage amesema mabadiliko hayo yamekuja leo (Ijumaa) baada ya wizara kupokea maombi ya Mhamasishaji Mkuu wa Viwanda ambaye ni Rais Magufuli.



“Rais Magufuli amesema anataka kuzunguka kwenye mabanda ya wajasiriamali wadogo na kuwauliza wafanyabiashara wakubwa kama na wao walianza kwa mitaji midogo,” amesema Mwijage.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni