Jumatano, 28 Juni 2017

je wajua?: Ndege kubwa kuwahi kutengenezwa duniani ingia hapa

Ndege ni chombo cha usafiri unaotumika kusafirisha au kwa ajili ya shughuli mbalimbali kutumia anga. Ikiwemo vita, fahamu ndege kumi zilizowahi kutumika katika vita kuu ya kwanza ya dunia na vita ya pili kuu ya dunia.


 



Ndege kubwa zaidi wakati wa Vita Vikuu vya Kwanza vya Dunia ilikuwa Zeppelin-Staaken R.VI, ndege ambayo ilizifanya ndege za wakati huo zionekane kama mifano tu ya ndege. (Picha: San Diego Air and Space Museum)


Ndege nyingine kubwa kutoka Ujerumani ilikuwa Dornier Do X, ilifanana na meli na ilikuwa injini 12. Iliweza kubeba abiria hadi 100. Ilikuwa na uzani wa tani 56. (Picha: Bundesarchiv)



ANT-20 iliyoundwa na Tupolev ilitumiwa kama chombo cha propaganda, ilikuwa na kituo cha redio, ukumbi wa sinema na chumba cha kutoleshea picha. Ilikuwa na injini kubwa juu ya mgongo wa ndege kuiwezesha kupaa. (Picha: Wikimedia Commons)


Ndege kubwa zaidi wakati wa Vita Vikuu vya Pili vya Dunia ilikuwa B-29 iliyoundwa na Boeing. Ndiyo iliyoangusha mabomu ya atomiki Japan. Ilifungua ukurasa mpya wa ndege za kuangusha mabomu za kusafiri masafa marefu.

 H-4 Hercules iliyoundwa na Howard Hughes ina mabawa marefu zaidi duniani kuliko ndege nyingine yoyote. Hata hivyo ilipaa angani mara chache tu.

 Convair B-36 Peacemaker ilikuwa ndege ya kwanza duniani ya kuangusha mabomu kuweza kusafiri kutoka bara moja hadi bara jingine. Ilitumiwa injini kadha za jeti na rafadha kadha kuweza kupaa. (Picha: Clemens Vaster)

B-52 Stratofortress iliyoundwa na Boeing inasalia kuwa moja ya ndege kubwa zaidi kuwahi kuundwa duniani. Ilitumia injini nane kubwa. (Picha: Getty Images)


 Tu-160 ya Tupolev ingeweza kubeba jumla ya tani 275 ikipaa, na ilikuwa na mabawa makubwa zaidi yaliyoweza kujipinda kuwahi kuundwa.



Ingawa Boeing 747 ilikuwa ndege ya kwanza kuitwa Jumbo Jet, A380 ya Airbus ni kubwa kuliko Boeing 747. Ndege hii inaweza kuwabeba watu 850.


Ndege kubwa zaidi kuwahi kuundwa duniani ni An-225 ya Antonov ambayo ina injini sita na urefu wake ni mita 84. Ndege hii ina uwezo wa kubeba karibu tani 250

chanzo cha habari mitandao mbalimbali.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni