Jumatatu, 28 Mei 2018

Wananchi wapiga kura kuruhusu utoaji wa mimba

Tume ya uchaguzi nchini Ireland imetangaza kuwa Wananchi wameanza kupiga kura kuruhusu utoaji mimba baada ya asilimia 66.4 ya wapiga kura kuunga mkono kuondolewa kwa kipengee cha sheria kinachopiga marufuku utoaji mimba.
Asilimia 33.6 pekee ya wapiga kura ndio waliopinga kundolewa kwa kipengee hicho. Mwenyekiti wa tume ya uchaguzi Barry Ryan alitangaza matokeo ya kura hiyo ya maoni mbele ya maelfu ya wananchi waliojawa na furaha.
Kura hiyo ya maoni iliungwa mkono katika eneo bunge 40 nchini humo isipokuwa eneo bunge la Donegal. Mji mkuu wa Dublin uliongoza kwa kuunga mkono kura hiyo ya maoni huku asilimia 51.9 ya wapiga kura wa mji huo wakiunga mkono utoaji mimba

Mahakama yaamuru Youtube kufungwa Misri

Leo May 28, 2018 Nakusogezea stori kutoka katikaambapo  Mahakama ya juu nchini Misri imeamuru mtandao wa YouTube ufungwe kwa mwezi moja nchini humo kwa kuonyesha video inayomkufuru mtume Muhammad.
“Uamuzi huo ni wa mwisho na hakuna anayeweza kukata rufaa,” wakili Mohamed Hamed Salem aliyewakilisha kesi hiyo mahakamani aliambia shirika la habari la Xinhua.
Hapo awali mahakama ya nchini humo iliagiza halmashauri ya mawasiliano nchini Misri (NTRA) kufunga YouTube lakini NTRA ikakata rufaa ikisema kwamba haina uwezo wa kisheria.
Wakili Hamed Salem aliyewakilisha kesi hiyo mahakamani mwaka wa 2013 alipendekeza mahakamani kwamba mtandao huo wa YouTube ufungwe na kupigwa marufuku nchini Misri hadi utakapoondoa video hiyo inayomkufuru mtume Muhammad na video zingine zinazoenda kinyume na imani ya dini ya Kiislamu.

Samatta kaipeleka KRC Genk Europa League usiku wa May 27 2018

Baada ya kushumba katika mechi kadhaa kutokana na kutoka majeruhi nahodha wa timu ya taifa ya Tanzania Taifa Stars anayecheza soka la kulipwa katika club ya KRC Genk ya Ubelgiji Mbwana Samatta usiku wa May 27 2018 amerudi tena kwenye headlines.

Mbwana Samatta amerudi kwenye headlines tena baada ya kuanza katika kikosi cha KRC Genk kilichokuwa kinacheza game za Play Off ya kuwania kupata tiketi ya kucheza michuano ya UEFA Europa League kwa msimu wa 2018/2019 wakicheza dhidi ya Zulte-Waregem.

Mchezo huo KRC Genk walicheza wakiwa nyumbani na kufanikiwa kupata ushindi wa magoli 2-0, Mbwana Samatta ndio alianza kuionesha Genk njia ya kueleka Europa League kwa kufunga goli la kwanza dakika ya 18 ya mchezo kabla ya Jere Uronen kufunga goli la pili dakika ya 28.

Ushindi huo sasa ni wazi unaipeleka KRC Genk kushiriki michuano ya UEFA Europa League ambapo kwa msimu wa 2018/19 itashirikisha pia timu za Chelsea na Arsenal za England, hata hivyo hiyo itakuwa fursa kwa Mbwana Samatta kucheza tena michuano hiyo kwa mara ya pili baada ya kucheza kwa mara ya kwanza msimu wa 2016/2017.

Habari Zilizopo Katika Magazeti ya Leo Jumatatu ya May 28


Jumapili, 27 Mei 2018

Ramos atuma salamu za pole kwa nahodha wa Misri na mshambuliaji wa Liverpool FC Mohamed Salah

Image may contain: 1 person
 Beki wa Real Madrid C.F. Sergio Ramos ametuma salamu za pole nahodha wa Misri na mshambuliaji wa Liverpool FC Mohamed Salah baada kumsababishia majeraha yanayoweza kumuweka nje ya mashindano ya Kombe la Dunia kwenye mchezo wa fainali ya UEFA Champions League

Mtanzania ashinda kwenye mashindano ya kuhifadhi Quran Afrika

KIJANA wa Kitanzania, Shujaa Suleiman Shujaa ameibuka kidedea na kitita cha sh. milioni 15 katika mashindano ya 19 ya Afrika ya kuhifadhi Quran kwenye kundi la washiriki wa juzuu 30.

Shujaa mwenye miaka 23 ambaye ni mkazi wa Morogoro, amejishindia pia laptop, kiwanja chenye hati eneo la Kigamboni kilichotolewa na kampuni ya Property International ya jijini Dar es Salaam pamoja na dola za Marekani 500 kutoka kwa Bw. Ahmed Seif “Magari” aliyetoa dola 500 kwa washindi wote watano.

Akizungumza na maelfu ya waumini na Watanzania waliofurika kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam leo mchana (Jumapili, Mei 27, 2018), Waziri Mkuu Kassim Majaliwa amewataka Watanzania waendelee kuilinda amani iliyopo nchini kwani ikipotea hakuna atakayeweza kufanya ibada.

“Mtakubaliana nami kuwa amani ya nchi yetu, ndiyo inatufanya tutembee vifua mbele dhidi ya wenzetu, ni neema kubwa ambayo kila muumini anapaswa kuilinda kwani ikipotea hata mkusanyiko wetu huu wa leo si rahisi kufanyika mahali kama hapa,” amesema.

“Leo hii tuko hapa uwanjani kwa sababu tuna amani, kama Serikali isingekuwa inashirikisha Watanzania wote kulinda amani, basi tusingeweza kukutanika hapa. Kuna nchi 18 ziko hapa, na watu wake wamekuja hapa uwanjani kwa kuwa wana uhakika na amani tuliyonayo sisi Watanzania,” alisema.

Alisema katika nchi ambazo amani imetoweka, watu wanalazimika kufanya shughuli za ibada majumbani au kwa kujificha. “Wenzetu hao, hawapati fursa adhimu kama hii ya kujumuika pamoja na majirani, ndugu, jamaa na marafiki kusikiliza na kufurahia kisomo cha Quran au kufanya shughuli nyingine za kiuchumi na kijamii,” aliongeza.

Aliwataka Watanzania waendelee kubeza na kupuuza kauli za walio wachache ambao kwao kuzungumzia amani ni kujipendekeza kwa Serikali. “Watu hao wamesahau kwamba tofauti katika Uislamu hazikuanza leo, lakini tofauti hizo hazikuwa sababu ya wema waliotangulia kuacha kuheshimiana na kushirikiana,” alisisitiza.

Mshindi wa pili kwenye kundi hilo la juzuu 30 ni Ahmed Noor wa Sudan ambaye ameshinda sh. 12,564,750 pamoja na laptop akifuatiwa na Muzamil Awadh Mohamed wa Sudan alijishindia sh. milion 7.5 pamoja na laptop zilizotolewa na kampuni ya Camara Education.

Mshindi wa nne ni Abdulally A. Mohammed wa Kenya aliyepata zawadi ya sh. 5,711,000 na wa tano ni Ibrahim Maazur kutoka Niger, aliyepata sh. 3,426,000. Washindi hao wote watano walipewa zawadi ya kwenda hijja na Waziri wa Mambo ya Dini wa Saudi Arabia, Dk. Saleh Ally Sheikh.

Washiriki wengine kwenye kundi la juzuu 30 walitoka nchi za Rwanda, Burundi, Msumbiji Djibouti, Kenya, Ethiopia, Congo DRC, Nigeria, Ghana na Afrika Kusini.

Washiriki wengine waliopewa zawadi ni wale walioweza kuhifadhi Juzuu tatu (washindi watatu), Juzuu tano (washindi watatu); Juzuu 10 (washindi watatu) na Juzuu 20 (washindi watatu).

Viongozi wengine waliohudhuria mashindano hayo ni Makamu wa Rais Mstaafu wa awamu ya nne, Dk. Mohammed Gharib Billal, Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana na mabalozi wanaoziwakilisha nchi zao hapa Tanzania kutoka Saudi Arabia, Comoro, Oman, Uturuki, Kenya, Msumbiji na Nigeria, Mufti na Sheikh Mkuu wa Tanzania, Sheikh Abubakar Zubeir bin Ally na Rais wa taasisi ya Al-Hikma, Sheikh Sharif Abdilkadir Al-Ahdal.

Katika hatua nyingine, Waziri Mkuu amemtaka Sheikh Nurdin Mohammed Ahmad (maarufu kama Sheikh Kishki) akaonane na Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Bw. William Lukuvi ili atoe maamuzi ya kiwanja chao kilichopo eneo la Matumbi ambacho mwaka jana aliagiza kifuatiliwe taratibu zake na kisha wapatiwe.

“Kuhusiana na suala la kiwanja mlichosema, mamlaka ya awali ni Manispaa ya Temeke na ilishakamilisha taratibu zote za kisheria, ikapeleka kwa Afisa Ardhi wa Mkoa kuona kama limepita kwenye vikao vyote ndipo wanaenda wizarani kupata kibali. Hakuna sababu ya wizara kuikatalia manispaa huku eneo lenyewe likiwa kwenye ramani kuu ya manispaa yenyewe, nenda mumuone Waziri mwenye dhamana, awape ardhi,” alisema.

Waziri Mkuu amefikia hatua hiyo baada ya kupewa taarifa akiwa jukwaani kwamba taasisi ya Al-Hikma iliwasiliana na Manispaa ya Temeke, hadi mkoani wakapewa barua zinaonyesha eneo liko sawa lakini walipofika wizarani wamekwamishwa na Afisa mmoja aliyemtaja kwa jina moja la Mama Mpetula.

Juni 11, mwaka jana katika mashindanio ya 18, taasisi ya Al-Hikma waliomba wapatiwe kiwanja na.118 kwenye kitalu E kilichoshikamana na kiwanja na. 117 chenye shule yao ya Al-Hikma Girls iliyoko Temeke ili waweze kujenga zahanati.

Chadema kumuaga Mbunge wao kesho Karimjee


Chama cha Demokrasia na Maendeleo CHADEMA, kimetoa taarifa ya ratiba ya kuaga mwili wa Mbunge wa Buyungu, Kasuku Bilago ambaye pia alikuwa ni Mjumbe wa Kamati Kuu ya Chama na Mwenyekiti wa Chama Kanda ya Magharibi yenye Mikoa ya Kigoma,Katavi na Tabora.

Kwa upande wa Bunge Marehemu alikuwa Naibu  Waziri Kivuli katika wizara ya  Elimu na Mafunzo.

Taarifa hiyo inasema baada ya kikao baina ya familia na Viongozi wakuu wa Chama kilichofanyika leo tarehe 27 Mei,2018 ratiba iliyokubaliwa ni kama ifuatavyo;

Jumatatu tarehe 28 Mei 2018 ni ibada fupi na kuuaga mwili katika viwanja vya Karemjee Dar kuanzia saa sita kamili mchana na mwili kupelekwa uwanja wa ndege, Dar es Salaam.

Tarehe 29 Mei siku ya Jumanne asubuhi mwili utapokelewa uwanja wa ndege, Dodoma na kupelekwa Bungeni ambapo  Wabunge watauaga mwili katika viwanja vya Bunge Dodoma. Baada ya hapo mwili utasafirishwa kwa ndege kuelekea Kibondo.

Tarehe 30 Mei siku ya jumatano wananchi wa Jimbo la Buyungu watapata fursa ya kuuaga mwili katika eneo  litakalotangazwa baadae.

Alhamisi tarehe 31 Mei, ndio siku ya Mazishi rasmi ambayo yatafanyika Nyumbani kwa Marehemu huko Wilayani Kakonko, Kigoma.


Rais Magufuli, Kinana wateta Ikulu





Taarifa iliyotolewa leo na Kurugenzi ya mawasiliano Ikulu inaeleza kuwa Rais John Magufuli ambaye pia ni Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi amekutana na kufanya mazungumzo na Katibu Mkuu wa chama hicho, Abdulrahman Kinana.


Katika mazungumzo hayo Rais amepokea salamu kutoka kwa viongozi wakuu wa vyama tawala vya ANC cha Afrika Kusini na ZANU PF cha nchini Zimbabwe.

Aidha taarifa hiyo imeeleza kuwa Rais na Kinana wamezunguma pia kuhusiana na maandalizi ya vikao vya kamati kuu na halmashauri kuu ya chama hicho vitakavyofanyika Mei 28, 29 mwaka huu jijini Dar es Salaam.

BREAKING: Shabiki wa LIVERPOOL ajinyonga

Leo May 27, 2018 Mwanafunzi wa mwaka wa pili katika chuo cha Saint Augustine Mbeya Moses Mashaka amejinyonga kwa mujibu wa mashuhuda wa eneo analoishi wamesema Mwanafunzi huyo alikuwa shabiki wa Club ya Liverpool na imedaiwa kuwa kitendo cha kufungwa kwa klabu hiyo goli 3-1 ndio sababu.
Hata hivyo wengine wamesema Mwanafunzi huyo alijiingiza katika mchezo wa kamari maarufu kama Betting na kitendo cha kuliwa inawezekana ikawa ndio sababu.
Akithibitisha kutokea kwa kifo hicho Kaimu Kamanda wa Jeshi la Polisi mkoa wa Mbeya Mussa Taibu amesema ni kweli amejinyonga kwa kutumia kanga chumbani kwake na aliyegundua kuwa kajinyonga ni Baba mwenye nyumba.

Kikwete: Alikiba umenipa heshima kubwa


Kuelekea mchezo maalum wa hisani kwaajili ya kuchangia fedha zitakazosaidia mahitaji ya wanafunzi, Mbunge wa Chalinze Mh. Ridhiwani Kikwete amekubali kujiunga na timu ya Alikiba itakayocheza na timu ya Mbwana Samatta.

Ridhiwani amekubali ombi la Alikiba la kuchezea timu yake kwenye mchezo huo kwa kusema heshima aliyopewa na msanii huyo ni kubwa na atashiriki kwani ni hatua muhimu katika kusaidia elimu.

Ridhiwani ameenda mbali zaidi kwa kuifananisha hatua ya Alikiba kumuita kwenye kikosi chake na kitendo cha timu za taifa kuita wachezaji wao kwaajili ya fainali za Kombe la Dunia.

Mchezo huo maalum kwa  kuhamasisha uchangiaji wa vifaa na miundombinu mashuleni utapigwa Juni 9, mwaka huu, kwenye uwanja wa Taifa jijini Dar es salaam. Samatta atakuwa nahodha wa timu ya marafiki zake na Alikiba atakuwa nahodha wa timu itakayoundwa na marafiki zake.

''Umenipa heshima kubwa kama walivyopewa walioitwa kuwakilisha mataifa yao katika kombe la Dunia. Twende tukasaidie Elimu Tanzania. Mwanzo Mzuri . Haya Ndiyo Watu Wema Ufanya'', amesema Ridhiwani.

a Wajumbe wa Kamati ya Uongozi na Wajumbe wa Tume ya Utumishi Ofisi ya Bunge kilichokutana kujadili taratibu za mazishi ya aliyekuwa Mbunge wa Jimbo la Buyungu (CHADEMA), Marehemu Kasuku Bilago aliyefariki jana


Spika wa Bunge, Job Ndugai akiongoza kikao cha pamoja kati ya Wajumbe wa Kamati ya Uongozi na Wajumbe wa Tume ya Utumishi Ofisi ya Bunge kilichokutana kujadili taratibu za mazishi ya aliyekuwa Mbunge wa Jimbo la Buyungu (CHADEMA), Marehemu Kasuku Bilago aliyefariki jana katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili.
Kikao hicho kimefanyika leo tarehe 27 Mei, 2018 katika Ofisi za Bunge Jijini Dodoma

Ridhwan Kikwete afafanua Kinana kujiuzulu

Moja ya stori iliyojitokeza katika magazeti ya Tanzania leo May 27, 2018 ni kuhusu taarifa zinazosema Katibu mkuu wa Chama cha Mapinduzi Abdulrahman Kinana amejiuzulu ambapo taarifa hizo hazikuthibitishwa na mtu yoyote mwenye mamlaka ndani ya CCM.
Mbunge wa Jimbo la Chalinze, Ridhiwani Kikwete baada ya kuona taarifa hizo katika magazeti ambazo zimewaacha watu na sitofahamu ameamua kulitolea ufafanuzi suala hilo katika ukurasa wake wa Instagram.
Ridwan ameandika hivi ‘Habari hii kama INAUKWELI”
“Isiwashtue. Ni utaratibu wa kawaida hasa inapofika kipindi kama hiki cha kuchagua Kamati kuu ya Chama Chetu CCM ( Kwa mujibu wa KATIBA) ; Wajumbe wote wa KAMATI KUU ukiondoa wale wanaoingia kwa Nafasi zao UJIUZULU Ujumbe wao ili kumpa nafasi MWENYEKITI Ateue Majina ambayo yatapelekwa HALMASHAURI KUU kupigiwa kura ili kupata KAMATI KUU Mpya”. ameandika Ridhwan 
“Kiutaratibu hata Sekretarieti nayo inakuwa ndani yake japo kwa mujibu wa KATIBA, Mwenyekiti anapewa Mamlaka ya kutangaza au kutotangaza kama ataendelea nayo ileile au La.”  Ridhwan

Kiumbe ambaye amewashangaza wataalamu Marekani

Experts say its body shape is different from a pure wolf


Wataalamu nchini Marekani wameshangazwa na kiumbe mmoja mfano wa mbwa mwitu aliyeuawa na mkulima huko Montana.
Mkulima huyo karibu na mji wa Donton alimpiga risasi kiumbe huyo wiki iliyopita alipokaribia mifugo wake, kwa mujibu wa maafisa.



Experts say its body shape is different from a pure wolf
Baada ya kumchunguza kiumbe hiyo walisema huenda akawa ni mbwa mwitu kwa sababu meno yake ni mafupi na makucha ni makubwa sana.
"Hatujafahamu hasa huyu mnyama ni wa familia ipi hadi uchunguzi wa DNA ukamilike," msemaji wa shirika ya samaki na wanyamapori alisema.

 Alisema itachukua hadi wiki moja kwa matokeo kujulikana, ambayo yatasaidia kumtambua kiumbe huyo.




Its fur is different from wolves, experts say

 Its front paws abnormally small for a wolf