Ijumaa, 4 Juni 2021

Mwenyekiti ccm Mkoa wa wa morogoro bi Doroth mwamsiku amewataka wanachama wa chama cha mapinduzi ccm, mkoani morogoro kujenga umoja wa chama hicho na kuendelea kumuunga mkono mh rais Samia suluhu hassani pamoja na juhudi zinazofanywa na serikali katika kuwaletea maendeleo watanzania.
Bi doroth ameyasema hayo akiwa ziara yake yakutembelea wanachama wa ccm katika halmashauri ya wilaya zote mkoani morogoro ,
ambapo akiwa katika kata ya mlimba june 2 ,2021 , halmashauri ya mlimba amehaidi kufuatilia kero ya wananchi wa mlimba ikiwemo ubovu wa barabara ifakara mlimba,na kero ya maji ambayo inawasumbua wakazi wa mji mdogo wa mlimba kwa miongo kadhaa licha ya kuwepo kwa mradi mkubwa wa maji ambao unasuasua,pamoja nakuhaidi kufuatilia mchakato wa kupewa mamlaka kamili ya mlimba kuwa wilaya inayojitegemea .
Aidha mwenyekiti huyo wa ccm ameongeza kuwa mara baada ya kukamilisha ziara hiyo atakwenda kuwaona baadhi ya wafanyabiashara wa mlimba ambao wapo mahabusu toka mwezi decemba 2020 ambao wanatuhumiwa kwa kesi ya uhujumu,mara baada ya kukutwa wakifanya shughuli za kilimo katika bonde la kilombero na makosa mengine ya utakatishaji wa fedha , ambapo pia ameowaomba wananchi waendeleee kutoa ushirikiano kwa mbunge wa jimbo la mlimba bwana godwin kunambi kwani ni mchapakazi,
Hata hivyo katika mkutano huo baadhi ya watendaji wa serikali ambao walieleza baadhi ya kero za wananchi wa kata ya mlimba na tarafa ya mlimba kwa ujumla .
Bi doroth mwamsiku pia amekabidhi vitendea kazi kwa makatibu kata wa chama cha ccm jimbo la mlimba rim paper zenye dhamani ya shilingi 390,000.


 

diwani wa igima awashukuru wananchi wake

 

 
 
Wananchi wa halmashauri ya wilaya ya mlimba mkoani
morogoro wametakiwa kuwaunga mkono viongozi wao
wakiwemo madiwani pamoja mbunge wa jimbo hilo ili kuleta
maendeleo katika halmashauri hiyo.
Rai hiyo imetolewa na mwenyekiti wa
halmashauri ya mlimba innocent saimon mwangasa ambaye
pia mwenyekiti wa ALAT mkoa wa morogoro , katika mkutano
wa hadhara uliyofanyika kata ya igima ambayo anahudumu
kama diwani wa kata hiyo,
Bwana mwangasa amesema kuwa anaendelea kufuatilia miradi
ya maendeleo katika kata hiyo ,na kutatua kero mbalimbali za
kata hiyo kwa upande wa huduma za kijamii ikiwemo ujenzi wa
kituo cha afya, barabara , na miradi ya maji,
Aidha diwani huyo amekemea baadhi ya lugha za maudhi
kwa baadhi watumishi wa halmashauri hiyo ,dhidi ya wananchi
,ambapo amewasihi maafisa wa serikali wakiwemo ,walimu na
maafisa watendaji kuwaheshimu wananchi
Aidha katika mkutano huo ulidhuriwa na kaimu mkurugenzi
wa halmashauri ya wilaya ya mlimba bwana colex m




wakyelu
ambaye alitumia nafasi hiyo kuzungumza na wananchi wa kata
ya igima na kutoa taarifa juu ya kusitisha ushuru wa halma
shauri uliokusudia kuwatoza wakulima wa zao la mpunga
,shilingi 2500 kwa gunia moja pindi wanapopeleka ghalani.
Mkurugenzi mwakyelu amesema kuwa ushuru huo umesitishwa
kwakua lengo la serikali ya awamu ya sita si kutoza ushuru
wakulima bali wafanya biashara
Kwa upande wake katibu wa mbunge wa jimbo la mlimba
bwana bundo lebeli amewaomba wananchi wa jimbo hilo
kuendelea kuwa na imani na madiwani wao,pamoja na mbunge
huku akizunguzumzia ujenzi wa barabara ya ifakara mlimba
,kwa kiwango cha lami kwa km 50 ,za awali.
wananchi wa kata ya igima wametumia nafasi hiyo
,kumpongeza diwani wao kwa jitihada za kuwaletea wananchi
wake maendeleo

KESHO YETU INAANZA NA LEO

 

 

 
 
 
 
KESHO YETU INAANZA NA LEO: Lengo letu ni kurudisha mazingira kwa ajili ya kesho yetu iliyo njema zaidi.
Tunaadhimisha Maadhimisho ya siku ya mazingira duniani yenye kauli mbiu “Kurejesha Mfumo wa Ikolojia” kwa kupitia mkakati wetu wa #TigoGreenForKili tunarejesha (1
 
 Safisha bahari & mitaa unamoishi Universal recycling symbolRejeleza Sake bottle and cupUsitumie plastiki FishKula vyakula vinavyozalishwa kwa uendelevu

Jumatatu, 18 Januari 2021

kunambi achangia ujenzi wa vituo vya afya ,shule jimboni kwake

 

 

 





ziara ya Mbunge wa Jimbo la Mlimba, Godwin Kunambi kwenye jimbo lake umekua na neema katika kata za Idete na Fumo baada ya mbunge huyo kuchangia Sh Milioni Sita kwenye ujenzi wa Kituo cha Afya, Zahanati, Miundombinu ya Barabara na ujenzi wa Hosteli ya Sekondari Matundu Hill.

Akizungumza katika kata ya Idete ambayo wananchi wake walimueleza changamoto yao ya ujenzi wa kituo cha afya na hostel ya shule hiyo Mbunge huyo aliahidi kutoa Sh Milioni 2.8 kwenye kata hiyo ili ielekezwe kwenye ununuzi wa mifuko 50 kwa ajili ya kituo cha afya na mifuko mingine 50 ya ujenzi wa hostel hiyo huku akitoa Sh Laki Tatu ili inunue Projector ya kufundishia shuleni hapo.
Mbunge Kunambi amesema anafahamu umuhimu wa elimu ni mkubwa na yeye kama kiongozi ambaye anaunga mkono juhudi za serikali ya Rais Dk John Magufuli ya kutoa elimu bila malipo ana wajibu wa kuchangia ujenzi huo ili kuendelea kuzalisha kizazi cha wasomi nchini.
" Wakati wa kampeni nilipita na mkanieleza shida zenu, nimekuja hapa ili tuanze na zile changamoto kubwa kwetu lakini lengo letu ni ndani ya miaka mitano hii mliyotupa dhamana kuhakikisha tunakamilisha kwa kiasi kikubwa Ilani ya Chama cha Mapinduzi kama ambavyo ilituelekeza," Amesema Mbunge Kunambi akiwa katika kata ya Idete.
Amesema hii ni ziara yake ya kwanza tangu aapishwe kuwa Mbunge na mpaka sasa ameshatembelea kata 11 kati ya 16 zilizopo kwenye jimbo lake huku akitatua changamoto mbalimbali kwenye kata zote alizozitembelea.
" Ziara yangu ina sura mbili moja ni kuwashukuru kwa kumchagua kwa kishindo Rais wetu Dk Magufuli, mimi mbunge wenu na madiwani wa CCM, tulianzia Kata ya Uchindile na bado tuna kata tano ili tuhitimishe kata zote 16, lakini sura ya pili ni kuanza kutatua changamoto na kero zetu, niwaahidi zipo ambazo tutazimaliza ndani ya mwezi mmoja, zipo tutakazochukua mwaka mzima na zipo ambazo tutazimaliza ndani ya miaka mitano, lakini niwahakikishie hatutoacha sehemu," Amesema Mbunge Kunambi.
Akiwa katika kata ya Fomu, Kunambi pia amechangia Sh Milioni 3.5 ili zielekezwe kwenye kumalizia boma la ujenzi wa kituo cha afya pamoja na kusaidia kivuko cha awali kwenye barabara ya kata hiyo ili wananchi waweze kupata bila kupata shida.
Akizungumza baada ya mchango ya mbunge huyo mmoja wa wanufaikaji ambaye ni Mkuu wa Shule ya Sekondari ya matundu Hills Kasmiri Stephano amempongeza Mbunge huyo kwa jitihada zake hizo huku akisema zitasaidia kuongeza ufaulu kwa wanafunzi hasa wa kike ambao watakua wakikaa kwenye hostel hizo huku akimuomba kuzidi kuiangalie shule hiyo.
" Namshukuru sana Mbunge wetu, kumalizia ujenzi wa hostel yetu kutakua ni msaada kwetu sisi wanafunzi wa kike lakini pia ametoa fedha za kununulia projector kitu ambacho tunaamini kitakua ni msaada kwa walimu wetu katika kutufundishia," Amesema mmoja wa wanafunzi wa shule hiyo.

Jumatano, 12 Septemba 2018

Vijue vinywaji vya ajabu vinavyotamba duniani


1. The Sourtoe Cocktail
Hicho ni kinywaji kinachopatikana katika Jiji la Dawson, Canada, maeneo ya Yukon.  Kinywaji hicho huwa kina kidole cha mguu wa binadamu ndani yake ambacho kimekolezwa chumvi.  Kiuhalisia, hutakiwi kukila kidole hicho, japokuwa wengine huvila kwa bahati mbaya.  Lakini wakati unamalizia kinywaji hicho kwenye bilauri, ni dhahiri kidole hicho kitagusa midomo yako!

2. Snake Wine
Hiyo ni divai (wine) inayopatikana nchini Vietnam, ambayo ndani yake huwekwa nyoka wazima, wakabakia humo wakiwa wazima au wamekufa.  Wanywaji wasioogopa, hunywa divai hiyo na kuwala nyoka hao.

3. Seagull Wine
Hii ni divai inayotumiwa na Waeskimo ambapo ndani yake hutumbukizwa ndege wa baharini aliyekufa kwa ajili ya kuikoleza.  Kwa hiyo, wanywaji huamua wenyewe matumizi ya ndege huyo.

4. Lizard Wine
Hii ni divai inayotokana na mchele ambayo inatumiwa nchini China.  Ndani yake hujazwa mijusi ambapo mchanganyiko huo hudaiwa kumlinda mnywaji dhidi ya mapepo mabaya.

5. Chicha de Muko
Hii ni pombe ya mahindi ambayo kutayarishwa kwake ni pamoja na kuyatafuna mahindi na kisha kuyatemea kwenye chombo maalum ambamo huwekwa na kuchanganywa na vitu vingine hadi inakuwa pombe.

6. Kumis (Fermented Mare’s Milk)
Hii ni pombe itokanayo na maziwa ya farasi yaliyowekwa hadi yakachachuka, inatumiwa na watu wa Mongolia.

7. Yak Butter Tea
Hii ni chai inayotumiwa huko Tibet ikiwa ni mchanganyiko wa siagi, majani ya chai na chumvi ambavyo huongezewa ngano iliyokaangwa na maziwa ya mtindi.

8. Bilk (Milk Beer)
Hii ni bia inayotumiwa nchini Japan ikiwa ni mchanganyiko wa maziwa, shayiri na mimea ya mihopi (hop).

9. The Aunt Roberta cocktail
Hiki ni kinywaji cha mchanganyiko wa gin,  vodka, brandy, matunda aina ya absinthe  na blackberry.  Kinatumika pia kusafishia vyombo ikiwa ni pamoja na kudeki sakafu.

Jumanne, 11 Septemba 2018

MASHINDANO MAPYA ULAYA;




Chama cha Soka Barani Ulaya (UEFA) kimesema kipo kwenye hatua za mwisho kuja na michuano mipya kwa ngazi ya vilabu barani humo, ambayo itakuwa ni michuano ya tatu kwa ukubwa baada ya #UEFAChampionsLeague na #EuropaLeague.
Mkuu wa Chama cha Vilabu barani Ulaya (ECA) Andrea Agnelli ndiye aliyetoa taarifa hiyo kwenye mkutano mkuu wa mwaka wa chama hicho unaofanyika nchini Croatia, lakini hajaweka wazi mfumo wa mashindano hayo utakavyokuwa.

Baada ya kusimama kwa wiki mbili kupisha michuano ya kimataifa, patashika ya Ligi Kuu Tanzania Bara kurudi wikiendi hii kwa mitanange saba kuishuhudia

No automatic alt text available.

Pichani ni Benjamani Mkapa akila kiapo Cha Kuwa Balozi wa Tanzania Nchini Nigeria Mbele ya Rais Julius Kambarage Nyerere IKULU Jijini Dar Tarehe 18-10-1976,Katikati ni Katibu mkuu kiongozi wa Rais Wakati huo Ndugu Timothy Opiyo.



 Pichani ni Benjamani Mkapa akila kiapo Cha Kuwa Balozi wa Tanzania Nchini Nigeria Mbele ya Rais Julius Kambarage Nyerere IKULU Jijini Dar Tarehe 18-10-1976,Katikati ni Katibu wa Rais Wakati huo Ndugu Timothy Opiyo.

GABON: MTANGAZAJI AJIUA BAADA YA KUTOLIPWA MSHAHARA KWA MIEZI 15 (MWAKA 1 NA MIEZI 3)


 

Mtangazaji wa Kituo cha Redio nchini Gabon (Redio Gabon) amejiua baada ya kutolipwa mshahara kwa miezi 15

Marius Pierre Foungues alikuwa Mtangazaji wa kipindi cha “Succès du temps passé” kilichokuwa kikirushwa kila siku za Jumapili asubuhi

Mwanahabari huyo alikuwa akikabiliwa na hali ngumu ya maisha ikiwa ni pamoja na matatizo ya kiafya

SHAMBULIO LA SEPTEMBA 11: MIAKA 17 BAADAYE, BADO MAJERAHA HAYAJAPONA


Miaka 17 imepita tangu dunia ilipotingishika kufuatia mashambulizi makubwa ya kigaidi yaliyolenga jengo refu zaidi duniani, World Trade Centre jijini New York na Jengo la Wizara ya Ulinzi (Pentagon) jijini Washington.

Leo Wamarekani wakiongozwa na Rais Donald Trump, wataadhimisha kumbukumbu ya tukio hilo lililotokea Septemba 11, 2001 ambapo zaidi ya watu 3000 walipoteza maisha, shughuli itakayofanyika Shanksville, Pennsylvania nchini humo.

Japokuwa siku nyingi zimepita, bado jinamizi la tukio hilo linaendelea kuwasumbua Wamarekani wengi, hasa wale waliopoteza ndugu zao kwenye tukio hilo baya zaidi katika historia ya ugaidi duniani huku wengine wakiachwa na ulemavu wa kudumu.

Katika maadhimisho hayo, watu wote watasimama kimya kwa dakika moja kuwaenzi wote waliopoteza maisha katika tukio hilo, huku majina ya watu wote waliopoteza maisha yakitajwa.

Wamarekani wengi wameendelea kuisisitiza serikali yao kuhakikisha tukio kama hilo halijirudii ndani ya ardhi ya nchi hiyo na kufanya kila kinachowezekana kukomesha ugaidi duniani kote.


Mshukiwa mkuu wa matukio hayo, Osama bin Laden aliyekuwa kiongozi wa Kundi la Al Qaeda, aliuawa Mei 2, 2011  Abbottabad, Pakistan na majeshi ya Marekani chini ya Rais Barrack Obama, katika oparesheni iliyopewa jina la Neptune Spear.

Maalimu Seif Kuchukua fomu kupitia Chadema | CUF na CHADEMA ni kitu kimoja


Mwenyekiti waBaraz la wazee Chadema Bw. Hashimu Juma amedai kuwa chadema na CUF ni kitu kimoja hivyo basi kama CCM wakifanikiwa kumtoa maalim seif zanzibar basi kutokana na wao kuwa kitu kimoja maalimu atachukua fomu kupitia chama hiko cha chadema pamoja na viongozi wengine wote wa maalim seif.

Beki wa Manchester United kukosa mechi hizi baada ya kupata majeraha

Beki wa kushoto wa klabu ya Manchester United na timu ya taifa ya England Luke Shaw aliyepata mshtuko baada ya mgongano wa bahati mbaya na beki wa Uhispania Dani Carvajal katika nusu ya pili ya mchezo uliowakutanisha miamba hao wawili ambapo England akiwa nyumbani alifungwa goli 2-1 na Hispania

Baada ya majeraha hayo ya kichwa Shaw alirudi United kwa ajili ya ufuatiliaji zaidi na matibabu siku ya Jumatatu licha ya beki huyo kuumia wakati anaitumikia timu yake ya taifa.

akiongea na wanahabari kocha wa timu ya taifa ya England Gareth Southgate alisema ” Hakuna mtu aliyetamani kuona tukio kama hilo”na kuongeza kuwa Shaw alitolewa uwanjani akiwa amefungwa vifaa vya kumuingizia hewa ya oksijeni lakini alisema kuwa amepata tena ufahamu haraka katika chumba cha matibabu, na hivi karibuni alikuwa akiwasiliana na marafiki na familia.

Baada ya beki huyo kisiki mwenye ustadi wa aina yake kuumia katika mchezo huo wa jumamosi dhidi ya Uhispani huku kocha wake Jose Mourinho akishuhudia jukwaani, msaada wa beki huyo utakosekana katika timu yake ya Manchester United katika mchezo wao wa siku ya jumamosi dhidi ya Watford,hivyo Luke Shaw hatakuwepo kwenye mchezo huo utakaofanyika katika dimba linalomilikiwa na The Golden Boys au jeshi la njano Watford linalojulikana kama Vicarage Road Stadium.

Siku chache kabla, Shaw alikuwa amefungua hadithi ya hofu ya mguu wake uliovunjika, ambalo alikiri alikuwa karibu na kumchukuliwa na kumlazimisha kufikiria kustaafu kutoka mchezo huo kwa umri wa miaka 23 tu.

Ajali ya Gari la Kubeba Mbao Yaua Watu Wanne Rombo

Na Dixon Busagaga,Rombo.
Watu  wanne wakiwemo wawili wa familia moja wamefariki dunia papo hapo baada ya gari walilokuwa wakisafiria aina ya Isuzu kuacha njia na kwenda kugonga gema katika eneo la Kikelelwa wilayani Hai.

Waliofariki dunia wametambulika kwa majina ya Emanual Josephat Silayo (28) ,Viviano silayo (35) wakazi wa Mbomai Juu,Juma Idd (20) maarufu kama mwarabu na mwingine aliyefahamika kwa jina moja la Deolla .

Kamanda wa polisi mkoa wa Kilimanjaro Hamis Issah aliyefika eneo la tukio amethibitisha kutokea kwa ajalo hiyo na kwamba dereva wa Loli hilo lililokuwa limebeba mbao alikimbia kusiko julikana baada ya ajali..

"Jitihada za kumtafuta dereva zinafanyika na chanzo cha ajali ni kupoteza muelekeo kwa Lori hilo na baadae kugonga Gema ndipo watu waliokuwa wanmekaa mbele walichomoka na kwenda kupigiza vichwa katika Gema na kupasuka"alisema Kamanda Issah.

Kamanda Issah amesema gari hilo likiwa na shehena ya mbao lilikuwa likitokea eneo la West Kilimanjaro ,eneo maarufu kwa uchanaji wa mbao na kwamba lilikiwa likielekea Rombo kupitia njia ya Rongai.

"Ni gari la kubeba mbao lilikua linatoka West Kilimanjaro kupitia njia ya Kikelelwa wilayani Rombo ,Gari aina ya Isuzu likiwa na namba za usajili T 889 ACN lilimshinda dereva na kuacha njia na baadae kugonga ngema iliyosababisha watu wanne waliokuwemo katika gari hilo kufa papo hapo." alisema Kamanda Issah.

Miili ya marehemu wote imehifadhiwa katika hosptali ya wilaya ya Rombo kwa ajili ya maandalizi ya mazishi.

Kuna uwezekano mkubwa wa kutokea El Nino mwishoni mwa mwaka huu:WMO





Mwishoni mwa waka huu wa 2018 kuna uwezekano mkubwa wa kuzuka matukio ya El Nino kwa mujibu wa takwimu mpya zilizotolewa leo na shirika la hali ya hewa duniani WMO.

Shirika hilo linasema uwezekano wa kuzuka kwa hali hiyo ni asilimia 70 na taarifa za mapema zitazisaidia jamii kujiandaa na matukio yanayoambatana na hali hiyo kama mvua kubwa, mafuriko na ukame.
Kwa mujibu wa katibu mkuu wa WMO Petteri Taalas, mabadiliko ya tabia nchi yanachangia kwa kiasi kikubwa kubadilisha mzunguko wa matukio ya El Nino na La Nina pamoja na athari zake katika jamii.
Kwa mfano amesema mwaka 2018 ulianza na hali dhaifu ya La Nina lakini hali hiyo haikutosheleza kupunguza mwenendo wa joto Kali lililotawala na hii ikimaanisha kwamba mwaka 2018 uko mbioni kuwa moja ya miaka yenye joto la kupindukiaduniani.
Mabadiliko hayo pia yamesababisha kuendelea kwa matukio mengine kama mafuriko makubwa Japan, India na Kusini mwa Asia, pia moto wa nyikani uliosababisha harasa kubwa Marekani ikiwemo kukatili maisha ya watu.
Hata hivyo WMO inasema haitarajii hali ya El Nino kuwa mbaya zaidi kama ilivyokuwa 2015-216 lakini bado italeta athari kubwa, ingawa shirika hilo linaamini utabiri huu wa mapema utasaidia kuokoa maisha na kupunguza athari za kiuchumi.
Hii ni mara ya kwanza WMO inajumuisha utabiri wa El Nino katika mtazamo wake wa kimataifa wa hali ya hewa kwa msimu wa Septemba hadi Novemba.

Kofi Annan kuzikwa Ghana, Alhamisi








 





Mwili wa aliyewahi kuwa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Kofi Annan, ambaye alifariki mwezi uliopita, umewasili katika nchi aliyozaliwa, Ghana.
Mwili wake uliwasili katika Uwanja wa Ndege wa Kotoka International Airport mjini Accra, ukisindikizwa na familia yake na maafisa wengine wa Umoja wa Mataifa.
Anatarajiwa kuzikwa kitaifa siku ya Alhamisi.


Kulikuwa na hali ya maombolezowakati mwili wake ukiwasili uwanjani hapo na kupokelewa na Rais wa Ghana Akufo Addo na viongozi wa kimila na kwa heshima ya kijeshi.
Mwili wake umehifadhiwa katika Ukumbi wa Kimataifa wa mikutano wa Ghana, wakati ukisubiri kuzikwa.


Akiwa na Malkia wa Uingereza

   kofi Annan alikuwa ni Katibu mkuu wa kwanza wa Umoja wa Mataifa, kutoka katika eneo la kusini mwa jangwa la Sahara na kuleta mafanikio sio tu katika bara la Afrika, lakini pia dunia nzima.
 Aliwahamasisha vijana wengi nchini mwake na waliheshimu kile alichosimamia.

Atandikwa viboko kwa kumpa kichanga pombe kali

Picha ya Mtandao

MKAZI wa Kijiji cha Buzirayombo wilayani Chato, mkoani Geita, Makubi Wanjala (25) amecharazwa viboko vitano kwenye makalio baada ya kubainika kumpa pombe kali mtoto wa miezi minane.

Kijana huyo ambaye ni mvuvi wa samaki kwenye mwalo wa Chato Beach, alikutana na kichapo hicho jana, majira ya saa tatu asubuhi eneo la mwalo huo baada ya kuomba kumbeba mtoto huyo kabla ya kumnywesha pombe kali aina ya "Shimha".

Akizungumza na gazeti hili, Mwenyekiti wa kitongoji cha Kalema, Fares Kabunazi, alisema akiwa kwenye majukumu yake ya kawaida alipokea simu kutoka kwa mmoja wa wavuvi kuwa anahitajika haraka eneo la mwalo wa Chato Beach na kuelezwa kuna dharura imejitokeza eneo hilo.

Baada ya kufika eneo la tukio alimshuhudia mtoto wa miezi minane (jina tunalihifadhi) akiwa amelegea kutokana na kupewa pombe hiyo.

Kiongozi huyo alifanikiwa kunusuru maisha ya kijana huyo baada ya kuuzuia umati wa wananchi waliokuwa wamekusanyika eneo hilo wakiwa na lengo la kumdhuru kijana huyo kutokana na kitendo chake cha kumnywesha pombe mtoto mdogo.

"Kutokana na jazba walizokuwa nazo wananchi na baada ya kumsikiliza mtuhumiwa pamoja na mama mzazi wa mtoto huyo, niliamua kutoa amri ya kucharazwa viboko vitano kwenye makalio yake na kumfukuza kufanya shughuli za uvuvi kwenye mwalo huo," alisema Kabunazi.

Akisimulia mkasa huo, mama mzazi wa mtoto hiyo, Husna Ally (28), alisema kijana huyo alifika dukani kwake na kukaa kwenye moja ya viti vilivyoko eneo hilo, huku akitumia pombe kali iliyoko kwenye kifungashio cha chupa ya plastiki na kuomba kumbeba mtoto huyo.

"Alipofika hapa dukani kwangu pamoja na pombe yake aliniomba kumbeba mtoto wangu...bila kuelewa kinachoendelea, nilimpa mtoto kwa nia njema kabisa, lakini baadaye ndiyo nilishangaa kumwona akimnywesha mwanangu pombe, huku mtoto akiendelea kulegea...ndipo baadhi ya wananchi walivyoona hali hiyo wakampigia simu mwenyekiti wetu wa kitongoji," alisema Husna.

Kwa upande wake kijana huyo, Makubi Wanjala, alikiri kumnywesha mtoto huyo pombe kwa madai hakujua kama ni kosa na kudai alimpa kiasi kidogo tu cha pombe hiyo.

Hata hivyo, alisema anajutia kosa hilo kutokana na kucharazwa bakora tano kwenye makalio kwa kuwa aliamini alikuwa akiburudika baada ya kumaliza kazi ya uvuvi.

Kwa mujibu wa Sheria ya Mtoto ya mwaka 2009 Ibara ya 13 kifungu kidogo cha (1), mtu yeyote haruhusiwi kumtesa mtoto au kumfanyia vitendo vingine vya ukatili, kumpa adhabu za kinyama au kumdhalilisha ikiwa ni pamoja na kumfanyia mambo ya kimila yanayoondoa utu wake au yenye madhara katika ustawi wake kimwili au kiakili.

Mama Samia awataka Wananchi kuchukua tahadhari juu ya ugonjwa wa Ebola


Makamu wa Raisi wa Tanzania Samia Suluhu Hassan amewataka wananchi mkoani Kigoma kuchukua tahadhari ya ugonjwa wa ebola kwa kutopokea wageni kiholela wanaoingia nchini bila kufuata utaratibu wa kisheria.

Samia ametoa wito huo wakati akizungumza na wananchi wa Kijiji cha Mwakizega wilayani Uvinza na kuwataka kufuata ushauri wa wataalamu wa afya juu ya njia za kujikinga na ugonjwa huo.

Aidha amesema ugonjwa huo ni hatari ikilinganishwa na magonjwa mengine na kwamba kwa sasa ugonjwa huo umeripotiwa kushamiri katika nchi ya Kongo Mashariki inayopakana kwa karibu sana na mkoa wa Kigoma.