Jumatano, 28 Februari 2018

makala Matumizi ya ujumla ya mics kwa wasanii na wengine







Microphone au Mic, ni kifaa muhimu katika uboreshaji na ukuzaji Wa Sanaa jukwaani. Kifaa hiki kimetengenezwa maalum Kwa ajili ya kudaka sauti "capture/pick up sound sources" mbalimbali yaweza ikawa ni ya mzungumzaji-talker, mwimbaji-singer au vyombo mbalimbali-music instruments.
Sasa iko hivi, Mwenyezi Mungu alivyotuumba akampatia kila mmoja wetu sauti (isipokuwa labda Kwa wale tu wenye mitihani) "Sauti". Hivyo basi sauti zetu twaweza kuzitumia Kwa kuzungumzia au Kwa kuimbia pia. Ndani ya miili yetu pia tunatofautiana uwezo Wa kusukuma mawimbi ya sauti na Kwa kudra sake Mola sauti zetu hutofautiana kwenye mawimbi hayo, iwe Kwa kuongea au kuimba. Wapo wenye sauti Kali za juu, wengine za kati wengine nzito, na wapo wenye ving'ng'o, za kukwaruza, kavu, laini na za mitetemo pia..ni maumbile Mungu katuumba nayo! Tushukuru tu..
Kifupi ninachotaka kukielezea hapa ni kuwa sisi Wasanii tuelewe kipi ni cha kufanya na kipi tusikifanye tukiwa mbele ya mics ili tupate kusikika vyema...
Mic ilivyoundwa ina umbile lake la nje na ndani, hapa nitagusia kidogo tu kuhusu tabia ya Mic Kwa umbile la ndani inayoitwa "PROXIMITY EFFECT" ni nini na Kwa nini ni muhimu sisi kuelewa hiyo "effect". Proximity kama neno linavyojieleza lina maana ya Ukaribu, hivyo Kwa kiswahili cha kutohoa tungesema athari za ukaribu/ kukaribia mic (kidaka sauti).
Mic kama iliyo pichani ni " directional mic" -Cardiod, hivyo umbile lake linaruhusu kudaka sauti kutoka upande elekezwa Wa mic, "directional" na hivyo ukitaka usikike vyema wewe kama chanzo cha sauti, isogelee mic Kwa ukaribu zaidi, gusisha mdomo wako kwenye mic (kama kuna "shoti" ya umeme ongea na technicians huwa inatolewa Kwa kuhakiki Earth/ground connections), na tambua wapi inadakia sauti vizuri, tambua umbo lake "polar pattern lake" na uwezo wake Wa kudaka sauti "frequency response"
Kwa nini ni muhimu kufanya hivyo Kwa sound check na performances kwako msanii ?
Kila mtu ana mgawanyo Wa mawimbi ya juu, kati na ya chini kwenye sauti yake-Voice Register, sasa ukiwa karibu na mic hasa hizi directional mics, kama iliyo pichani, zina kawaida ya kukuza -"boost" mawimbi ya chini ya sauti yako "bass frequencies" kama zitawekwa kwenye kwa ukaribu na source na huo mpangilio huitwa "closer proximity to the source" na hivyo kuifanya sauti yako iwe na uhai zaidi, warmer, uhalisia na nguvu zaidi.
Tunachosea sisi wasanii ni kukaa mbali na mics wakati Wa sound check na wakati Wa performances kuzikumbatia, kuzifunika na kuzifutika na mikono yetu "covering mic grille" na hivyo kupunguza uwezo Wa mic kudaka sauti zetu vizuri. Kwani ukifunika "huo wavu-,grille" unazuia mawimbi yasidakwe vyema, na pia Kwa kufutika kwenye mikono, tunatengeneza more room na mikono yetu kugeuka kuwa "resonators" na mic hutoa sauti ya vibuyu hivi.
Zingatia kuwa wewe ndio Source, mic inadaka sauti yako, amplifiers zinakuza sauti yako, speakers zinatamka sauti yako! Huna haja ya kushupaza shiko na kukausha sauti, isogelee mic, wala kuumba sauti kwa kugeuza mic upside down, au kuifunika kwa mikono.
Set pamoja na Fundi kiwango cha usikivu unachotaka, na kiwango utakachosukuma sauti "comfortably" ili onesho lako/ lenu liwe na usikivu mzuri na tones registry mzuri pia...
Audio Tech's ni kuwaambia kile Msanii unataka, hawajui colour wala tone ya kazi yako! Wao wanajua namna ya kuongoza mashonevza kukuzia sauti, Wewe ndio unajua Muziki au Sanaa yako inasikikaje? Au "inaliaje"don't compromise!..Jizoeshe kuisogelea mic upate Proximity effect kwenye Sauti yako! "Your voice registry" kotekote kwenye Sound check na performances.
 



MSIMAMO: Baada raundi ya 19 kukamilika, msimamo wa #VPL unaonesha Yanga ikizidi kuifukuzia Simba kileleni huku tofauti ikiwa ni pointi tano pekee, wakati Ndanda FC ikiendelea kubaki katika nafasi yake ya 13.

https://scontent.fdar1-1.fna.fbcdn.net/v/t1.0-9/28471571_1005802122919362_7051231216607248552_n.jpg?oh=4567d12019e5e7581ab12e677b084661&oe=5B081913

Mahakama yamsomea maelezo ya awali Tido Mhando


Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu imemsomea maelezo ya awali mkurugenzi mkuu wa zamani wa Shirika la Utangazaji Tanzania (TBC), Tido Mhando anayekabiliwa na mashtaka matano likiwamo la matumizi mabaya ya madaraka.

Kabla ya kusomewa maelezo leo Februari 28,2018 mbele ya Hakimu Mfawidhi, Victoria Nongwa, Wakili wa Serikali Dismas Mganyizi, alimkumbusha mashtaka yanayomkabili Tido anayetetewa na wakili Ramadhani Maleta.

Baada ya kusomewa, Tido ambaye yuko nje kwa dhamana amekubali maelezo binafsi na kwamba alikuwa mkurugenzi mkuu wa TBC mwaka 2006 hadi 2010,Amekubali kuwa alikuwa msimamizi wa shughuli za TBC lakini si zote.

Pia amekubali kutoa maelezo kwa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru) na kuwa alifikishwa mahakamani Januari 26,2018.

Tido amekana mashtaka yanayomkabili na upande wa mashtaka katika kesi hiyo utaanza kutoa ushahidi Machi 28,2018.

Anakabiliwa na mashtaka manne ya kutumia madaraka vibaya na moja la kuisababishia Serikali hasara ya Sh887.1 milioni.

Tido anadaiwa Juni 16,2008 akiwa Dubai, Umoja wa Falme za Kiarabu (UAE), akiwa mkurugenzi mkuu wa TBC kwa makusudi alitumia madaraka yake vibaya kwa kusaini mkataba wa kuendesha na kutangaza vipindi vya televisheni kati ya TBC na Channel 2 Group Corporation (BV1) bila kupitisha zabuni kinyume cha sheria ya ununuzi, hivyo kuinufaisha BVl.

Katika shtaka la pili anadaiwa kutumia vibaya madaraka yake ikielezwa Juni 20,2008 alisaini makubaliano ya utangazaji wa digitali duniani kati ya TBC na BVl.

Tido katika shtaka la tatu anadaiwa Agosti 11,2008 na Septemba 2008 akiwa Dubai alitumia vibaya madaraka yake kusaini mkataba wa makubaliano ya ununuzi, usambazaji, kufunga vifaa vya usambazaji na mnara wa utangazaji kati ya TBC na BVI na kuifaidisha BVI.

Shtaka la nne, anadaiwa Novemba 16,2008 akiwa Dubai alitumia vibaya madaraka yake kusaini mkataba wa makubaliano ya kuendesha miundombinu ya utangazaji kati ya TBC na BVI na kuinufaisha BVI.

Tido katika shtaka la tano anadaiwa kati ya Juni 16 na Novemba 16,2008 akiwa Dubai aliisababishia TBC hasara ya Sh887.1 milioni.

Hii ndio ripoti ya idadi ya Watu Tanzania


Ripoti ya makadirio ya watu nchini inaonyesha Tanzania kuna idadi ya watu 54.2 milioni hadi kufikia mwaka 2018 huku ikieleza kuwa kila mwaka kuna ongezeko la watu milioni 1.6.

Ripoti hiyo inaonyesha Tanzania Bara ina watu 52.6 na Zanzibar milioni 1.6  inaifanya Tanzania kuwa nchi ya sita barani Afrika kwa ongezeko kubwa la watu ikitanguliwa na Nigeria, Ethiopia, DRC na Misri.

Akizindua ripoti hiyo leo Jumatano Februari 28, 2018 Waziri wa Fedha na Mipango, Dk Phillip Mpango amesema idadi hiyo ya watu inakadiriwa kufikia 77.5 milioni ifikapo mwaka 2030 wakati nchi zote duniani zitakuwa zinatathmini mafanikio na changamoto za Malengo ya Mpango wa Dunia wa Maendeleo Endelevu (SDGs).

Amesema kwa kuzingatia matokeo ya sensa ya watu ya mwaka 2012, inakadiriwa kuwa kila mwaka kuna ongezeko la wastani wa watu wapatao 1.6 milioni hapa nchini.

"Ongezeko hili linatokana na idadi kubwa ya vizazi vipatavyo milioni 2 ikilinganishwa na idadi ndogo ya vifo ambavyo nintakribani 400,000 kwa mwaka," amesema.

Kutokana na takwimu hizo, Dk Mpango amesema hairuhusiwi shirika lolote kufanya makadirio ya idadi ya watu na kuchapisha makadirio hayo bila kuishirikisha Ofisi ya Taifa ya Takimu (NBS).

"Kwa kufanya hivyo ni kosa, makadirio hayo hayaendani na hali halisi ya watu na inahatarisha maendeleo ya nchi. Takwimu za nchi ambazo vigezo vyake haviendani na hali halisi vinapotosha hali ya ustawi wa nchi na wananchi waje," amesema.

Awali Mkurugenzi Mkuu wa NBS, Dk Albina Chuwa amesema kasi hiyo kubwa ya ongezeko la watu inasababishwa na kiwango cha juu cha uzazi  ambapo tafiti zinaonyesha wastani wa mwanamke kuzaa ni watoto watano kwa kipindi chake cha uzazi.

Amesema pia kasi hiyo inasababishwa na matumizi madogo ya njia za uzazi, umaskini na kiwango duni cha elimu miongoni mwa wanawake hasa katika maeneo ya vijijini.

Siku 100 toka Mwandishi wa Mwananchi achukuliwe na wasiojulikana




Leo February 28, 2018 Uongozi wa Kampuni ya Mwananchi Communications Limited (MCL) umefanya mkutano na waandishi wa habari na kuzungumza kuhusiana na mwandishi wa kampuni hiyo Azory Gwanda ambaye alipotea November 21, 2017.
Ikiwa zimepita siku 100 tangu mwandishi huyo amepotea, Mkurugenzi wa Kampuni hiyo Francis Nanai ameeleza kuwa kampuni hiyo imejitolea kuhudumia mahitaji ya familia ya mwandishi huyo.
Nanai ameeleza kuwa watalipia mahitaji ya watoto wa shule, bima ya afya, biashara ya kujikimu pamoja na gharama za chakula na kwamba kampuni itafanya hivi hadi pindi Bi Anna atakapoweza kusimama mwenyewe.
Taarifa zinaeleza kuwa wakati Azory anatekwa mkewe Anna Pinoni alikuwa mjamzito na alikuwa na mtoto wa miaka 6, Anna February 12, 2018 amejifungua mtoto wa kike waliyempa jina Gladness.

Yanga yafanya kweli mtwara




Baada ya kumaliza mchezo wa kombe la FA dhidi ya Majimaji ya Songea katika uwanja wa Majimaji, club ya Yanga ilikuwa na safari ya kwenda Mtwara katika uwanja wa Nangwanda kucheza mchezo wao wa Ligi Kuu Tanzania bara dhidi ya Ndanda FC.
Kabla ya game ya leo Yanga ilikuwa na rekodi mbaya dhidi ya Ndanda katika uwanja wa Nangwanda kwani ilikuwa haijawahi kupata ushindi wowote katika game zake, leo February 28 Yanga wanafanikiwa kupata ushindi wa magoli 2-1.
Magoli ya Yanga yaliyoweka rekodi na kuvunja mwiko wa kutopata matokeo katika uwanja wa Nangwanda yalifungwa na Pius Buswita dakika ya 6 na Hassan Kessy huku goli pekee la Ndanda la kufutia machozi lilifungwa na Nassoro Kapama dakika ya 46.

Watu 21 wanusurika kifo kwenye ajali ya treni Kigoma



Watu 21 wamenusurika kifo kwenye ajali mbaya ya Treni mchana wa leo katika Kijiji cha Mpeta wilayani Uvinza, mkoani Kigoma kati ya stesheni ya Malagarasi na Uvinza.

Akithibisha taarifa hizo, Kamanda wa polisi wa Mkoa wa Kigoma amesema hakuna mtu aliyepoteza maisha kwenye ajali hiyo, huku akiahidi kutoa taarifa zaidi juu ya tukio hilo.

Mashahidi wamesema kuwa kichwa cha Treni kiliacha reli na kudumbukia kwenye dimbwi la maji kuna mabehewa mawili yakifuata kichwa hicho.

Kombe la Dunia kutembelea nchi hizi

Wakenya wamejitokeza kwa wingi kulitazama na kupigwa picha na Kombe la Dunia la Shirikisho la Soka Duniani (Fifa) ambalo limekuwa nchini humo kwa siku mbili.

Kombe hilo ambalo liliwasili nchini Kenya na kupokelewa na Rais wa nchi hiyo, Uhuru Kenyatta lilipata watazamaji wengi ambao walifika kujionea na kupiga picha pamoja na kombe hilo.

Raia wa kawaida hawakuruhusiwa kuligusa kombe hilo, na badala yake walilitazama likiwa katika sanduku la Kioo.

Ni rais huyo pekee aliyeruhusiwa kuligusa kombehilo nchini Kenya. Kando na marais, ni wachezaji waliowahi kushinda kombe hilo pekee ambao huruhusiwa kuligusa.

Kombe hilo linatembezwa mataifa mbalimbali kabla ya michuano ya Kombe la Dunia kuanza Juni, nchini Urusi. Na ni mara ya tatu kwa kombe hilo kuwa nchini Kenya, awali ikiwa 2010 na 2013 katika ya fainali zilizofanyika Afrika Kusini na Brazil.

Kabla ya kutua Kenya, kombe hilo lilikuwa nchini Sudan kisha Ethiopia.

Hata hivyo ziara ya kombe hilo bado inaendelea ambapo limeondoka nchi Kenya na kuelekea Maputo, Msumbiji.

Nchi nyingine za Afrika zinazotarajia kufikiwa na ziara hiyo ya Kombe la Dunia ni Afrika Kusini, Uganda, Nigeria, Senegal, Cote D’Ivoire (Ivory Coast) kisha Misri.

Baada ya ziara ya kombe hilo barani Afrika kukamilika, litaelekea barani Ulaya kuendelea na ziara yake kabla ya kuanza mchuano ya Kombe la Dunia itakayofanyika nchini Urusi, Juni 14, mwaka huu.

Hapa chini ni ratiba nzima ya ziara ya Kombe la Dunia katika nchi mbalimbali duniani. Zipo nchi ambazo tayari zimeshatembelewa na nyingine zinaendelea kutembelewa.

Kituo                                  Tarehe

Colombo, Sri Lanka           23-24 January

Male, Maldives                   24-25 January

Phuket, Thailand                   26-27 January

Vientiane, Laos                   28 January

Macau, China P.R                   29 January

Nukualofa, Tonga                   31 January

Honiara, Solomon Islands   1 February

Port Moresby, Papua New Guinea 1 February

Lahore, Pakistan                    3 February

Almaty, Kazakhstan            4 February

Bishkek, Kyrgyz Republic    5 February

Dushanbe, Tajikistan            5 February

Tashkent, Uzbekistan            6 February

Ashgabat, Turkmenistan            7 February

Yerevan, Armenia                    7 February

Tblisi, Georgia                    8 February

Baku, Azerbaijan                    9 February

Valetta, Malta                           10 February

Vienna, Austria                   11 February

Minsk, Belarus                   13 February

Sofia, Bulgaria                   14 February

Tel Aviv, Israel                   15 February

Larnaca, Cyprus                   16 February

Ramallah, Palestine           17-19 February

Amman, Jordan                   20 February

Dubai, United Arab Emirates    21 February

Khartoum, Sudan                    22-23 February

Addis Ababa, Ethiopia           24-25 February

Nairobi, Kenya 26-27 February

Maputo, Msumbiji 28 February

Johannesburg, Afrika Kusini 1-2 March

Cape Town, Afrika Kusini 3 March

Kampala, Uganda 5-6 March

Abuja, Nigeria 7-8 March

Lagos, Nigeria 9-10 March

Dakar, Senegal 11-12 March

Abidjan, Cote d’Ivoire 13-14 March

Cairo, Misri 15-16 March

Naples, Italy 17-19 March

Paris, France 20-21 March

Cologne, Germany 22-23 March

Oslo, Norway 24 March

Torshavn, Faroe Islands 24-25 March

Reykjavik, Iceland 25 March

Tucuman, Argentina 27-28 March

Berazategui, Argentina 29 March

Buenos Aires, Argentina 30-31 March

Rosario, Argentina 1-2 April

Bogota, Colombia 3-5 April

Panama City, Panama 6 April

San Jose, Costa Rica 7-8 April

Guadalajara, Mexico 9-10 April

Monterrey, Mexico 11-12 April

Mexico City, Mexico 13-15 April

New York, USA 16 April

Miami, USA 17 April

Los Angeles, USA 18-20 April

Frankfurt, Germany 22 April

Ulaanbaatar, Mongolia 23 April

Beijing, China P.R 25 April

Shanghai, China P.R 26 April

Tokyo, Japan 27-28 April

Osaka, Japan 29-30 April

Vladivostok, Russia 1 May

Waziri Mavunde aagizi Wakurugenzi kupandishwa Kizimbani


NAIBU Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu, anayeshughulikia Kazi, Ajira na Vijana, Mhe. Antony Mavunde, ameagiza waajiri ambao hawajajisajili na Mfuko wa Fidia kwa Wafanyakazi kufanya hivyo, vinginevyo wafikishwe mahakamani mara moja.

 Mhe. Mavunde ametoa agizo hilo Jumatatu Februari 26, 2018 baada ya kufanya ziara ya kushtukiza jijini Mwanza, kubaini waajiri ambao bado hawajatekeelza takwa la kisheria kifungu cha 5 cha Sheria ya Fidia Kwa Wafanyakazi, Sura 263 marejeo ya mwaka 2015, ambayo inamtaka kila mwajiri kutoka sekta ya umma na binafsi Tanzania bara awe amejisajili na kuwasilisha michango kwenye Mfuko huo.

Kwa mujibu wa Mkurugenzi wa Uendeshaji wa Mfuko huo, Bw. Anslem Peter,  jiji la Mwanza pekee lina waajiri 1228, lakini kati ya hao ni waajiri 482 tu ndio waliojisajili na Mfuko huku waajiri wengine 746 wakiwa bado hawajajisajili. Hali hiyo ndiyo iliyomfanya Mhe. Naibu Waziri kufanya ziara hiyo ya ghafla.

Akitoa taarifa kwa waandishi wa habari mara baada ya ukaguzi huo wa kushtukiza, Mhe. Mavunde pia ameiagiza WCF kuwafikisha mahakamani mara moja, waajiri wa kampuni ya ujenzi ya JASCO, (Mkurugenzi Mtendaji Bw.Karan Bachu),

Mkurugenzi Mtendaji wa kampuni ya Airco Holdings  inayotoa huduma za kusogeza vifurushi na mizigo uwanja wa ndege wa Mwanza na hoteli ya Belmonte ya jijini humo ambapo Mkurugenzi Mtendaji wa Hoteli hiyo, Bw. Philemon Tei, amejikuta matatani.

"Naagiza  waajiri hao kulipa michango yote ya nyuma (tangu tarehe 1 Julai 2015 tangu Mfuko ulipoanza kutekeelza majukumu yake au siku mwajiri aliyoanza kazi zake iwapo ni baada ya tarehe 1 Julai 2015).

Mhe. Mavunde ameagiza waajiri hao kufanya mawasiliano na watendaji wa Mfuko haraka iwezekanavyo ili kuweza kubaini kiwango cha riba kila mwajiri anachopaswa kulipa kutokana na kuchelewesha michango katika Mfuko.

“Ni kosa la jinai kwa mwajiri kutotekelza takwa hilo la kisheria na kifungu cha 71(4) cha Sheria ya Fidia kwa Wafanyakazi kimeweka wazi kuwa mwajiri wa aina hii, anaweza kutozwa faini isiyozidi shilingi milioni 50,000, kifungo kisichozidi miaka 5 jela au adhabu zote kwa pamoja, kwa hivyo nitoe wito kwa waajiri hao, hakuna sababu ya kushurutishwa kutekeleza sheria.

"Tutatekelza agizo la Mhe. Waziri kama alivyolitoa, na nitoe rai tu kwa waajiri kote nchini (Tanzania Bara), kutekeleza takwa hilo la kisheria, kwani hakuna kichaka cha kujificha tutawafikia." Alisisitiza Mkurugenzi wa Uendeshaji wa Mfuko huo, Bw. Anslem Peter katika taarifa yake kwa waandishi wa habari.


#VPL Hassan Ramadhan Kessy anaipigia Yanga bao la pili. Ndanda FC 0-2 Yanga SC.

Image may contain: text



Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania [TCRA] imepokea Orodha ya nyimbo zisizokuwa na maadili kutoka Baraza la Sanaa la Taifa [BASATA].



Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania [TCRA] imepokea Orodha ya nyimbo zisizokuwa na maadili kutoka Baraza la Sanaa la Taifa [BASATA].



#VPL Pius Buswita anakuwa mchezaji wa kwanza wa Yanga kufunga bao katika dimba la Nangwanda Sijaona. Ndanda FC 0-1 Yanga SC,

Image may contain: text

Daktari wa Simba SC athibitisha Emmanuel Okwi yupo fiti

Daktari wa klabu ya Simba, Yassin Gembe amesema kuwa mshambuliaji wa timu hiyo raia wa Uganda, Emmanuel Okwi anaendelea vizuri kufuatia majeraha aliyopata kwenye mchezo uliyopita dhidi ya Mbao FC.

Gembe amesema kuwa Okwi anaendelea vizuri ukilinganisha na alivyokuwa hapo hawali na kunauwezekano mkubwa wa kuwepo katika mchezo ujao dhidi ya Stand United unaotarajiwa kupigwa siku ya Ijumaa.
Okwi anaendelea vizuri sana tofauti na jana, kwa hali aliyonayo pamoja na tiba ambazo tumeshampatia ni asilimia kubwa sana kwa yeye kuwepo kwenye mchezo unaofuata dhidi ya Stand United Ijumaa hii
Simba inaongoza katika msimamo wa ligi kuu soka Tanzania Bara kwa kuwa na jumla ya pointi 45 huku mshambuliaji wake huyo raia wa Uganda akiwa kinara wa mabao katika mbio za kuwania kiatu cha dhahabu kwa kujikusanyia jumla ya mabao 16 kibindo dhidi ya mchezaji wa Yanga SC Obrey Chirwa mwenye magoli 11 huku nafasi ya tatu ikishikiliwa na John Bocco wa Simba SC aliyo na goli zake 10.

Kauli ya Manara kuhusu hali ya Bocco

Mshambuliaji wa klabu ya soka ya Simba SC, John Bocco ameelezwa kupona majeraha aliyoyapata kwenye mchezo wa ligi kuu dhidi ya Mwadui FC na muda wowote ataanza kucheza kama kocha atampanga.

Afisa habari wa Simba Haji Manara amethibitisha hilo wakati akijibu maswali ya mashabiki wa klabu hiyo waliokuwa wanataka kujua hali ya nahodha huyo wa Simba kupitia ukurasa wake wa Instagram.

''Niwajuze tu kuwa hali ya Bocco anaendelea vizuri na yupo tayari kucheza kama kocha atampanga'', Manara alimjibu moja ya mashabiki waliouliza.

Aidha Manara ameongeza kuwa majeruhi pekee aliyebaki kwenye kikosi cha Simba ni Haruna Niyonzima ambaye hivi karibuni alipelekwa India kwaajili ya matibabu na Manara ameongeza kuwa naye yupo mbioni kurejea.

Majeruhi wengine wa muda mrefu ndani ya kikosi cha Simba ambao tayari wameanza mazoezi mepesi ni mlinda mlango Said Nduda na mlinzi Salim Mbonde ambao wote wamesajiliwa msimu huu wakitokea Mtibwa Sugar.

Jumanne, 27 Februari 2018

Agizo la Waziri Jafo kwa Maafisa elimu wote nchini

February 27, 2018 Waziri wa Ofisi ya Rais Tawala za mikoa na serikali za mitaa (TAMISEMI) Selemani Jafo alikutana na Walimu pamoja na maafisa elimu mkoani Dodoma lengo likiwa ni kuzijua changamoto zinazowakabili na kusababisha kushuka kwa viwango vya elimu ambapo amesema Serikali haitaendelea kuvumilia makosa binafsi.
Mkoa wa Dodoma bado kuna shida, haipendezi miaka nenda miaka rudi mkoa huu haufanyi vizuri kielimu. Mambo bado tiamaji tiamaji. Maafisa elimu fanyeni kazi na viongozi wenu tupo tayari kuwasaidia lakini hatupo tayari kuwavumilia kama mnafanya vibaya, badilisheni mienendo yenu” –Waziri Jafo

Waziri Mwijage abariki ujenzi wa kiwanda cha samani za ndani cha Danube na


Uzinduzi wa filamu ya ‘A Wrinkle in Time’ ulivyofanyika, Oprah na Kobe Bryant wahudhuria



Usiku wa jana umefanyika uzinduzi wa filamu ya ‘A Wrinkle in Time’ ambayo imeongozwa na Ava DuVernay. Filamu hiyo ambayo imetengenezwa na kampuni ya Walt Disney Pictures, inatarajiwa kuachiwa rasmi March 9, 2018.

Picha ya watu waliohusika kutengeneza filamu hiyo
Filamu hiyo mwanzoni ilipangwa kutoka Aprili 6, 2018. Baadhi ya watu waliohudhuria kwenye uzinduzi huo ni Oprah Winfrey, Kobe Bryant, Paco Delgado, Bellamy Young na wengine. Hapa chini ni baadhi ya picha za watu waliohudhuria kwenye uzinduzi huo.


Picha ya Ava DuVernay ambaye ni director wa filamu hiyo









 


 



 

Hali ya mtunzi wa wimbo wa ‘Tanzania yetu ndio nchi ya furaha’ yatia matumaini

Baraza la Sanaa Tanzania (BASATA) leo Jumanne Februari 27, 2018 limemtembelea mtunzi wa wimbo uliovuma zaidi miaka ya nyuma wa ‘Tanzania yetu ndio nchi ya furaha’, Mzee Stephen Hizza ambaye anasumbuliwa na ugonjwa wa saratani ya tezi dume.
Katibu Mtendaji Godfrey Mngereza (Kulia) akimjulia hali Mzee Stephen Hizza aliyelazwa katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili.
Mzee Hizza amelazwa wiki chache zilizopita katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili wodi ya Kibasila Chumba Na.16 ameonekana afya yake kuendelea vyema tofauti na kipindi cha nyuma kama ilivyoripotiwa awali na vyombo vya habari.
Wimbo wa ‘Tanzania yetu ndio nchi ya furaha’ uliimbwa na Bendi ya ‘ Atomic Jazz Band’ miaka ya 19 70’s ikiongozwa na John Kijiko. Jikumbushe wimbo huo hapa chini

Abdi Banda kafunguka leo kuhusu Thomas Ulimwengu

Moja kati ya stori zinazochukua headlines sana kwa sasa ni pamoja na kiwango cha beki wa kimataifa wa Tanzania anayecheza soka la kulipwa katika club ya Baroka FC ya Afrika Kusini Abdi Banda, inawezekana ukawa hauifahamu kuhusiana na mchango wa kimawazo wa Thomas Ulimwengu katika soka la Abdi Banda.
Thomas Ulimwengu ni mtanzania ambaye amewahi kuichezea TP Mazembe ya DRC Congo na baadae akajiunga na AFC Eskilstuna ya Sweden kabla ya kupata majeruhi yaliyomuweka nje ya uwanja kwa muda mrefu.

“Nakumbuka siku ya kwanza unaongea na mimi ilikuwa ETHIOPIA kwenye kambi ya timu taifa ulikuwa hunijui ila mimi nakujua kwa sababu ya mafanikio yako katikati ya mazoezi uliniambia nakuona mbali sana kwenye maisha yako ya soka”>>>Banda
“Jiamini kama unaweza utafanikiwa nadhani katika watu waliofikisha mpaka kuwa hapa leo basi wewe una nafasi yako na kikubwa unazid kunipa kiburi cha kuona hapa pia sehemu sahihi kwangu niendelee na safari asante sana bro @thomasulimwengu 👏👏👏Mungu azidi kukupa afya nzuri  @samagoal77👏👏 From ZERO to HERO Godfirst”hainakufeli”>>>Banda

MBINU ZA KUCHANGAMSHA MAENDELEO

Image may contain: outdoor and nature

 Wananchi wa Ghana wanaokabiliwa na ubovu wa miundombinu wamefikia uamuzi wa kupanda migomba kwenye mashimo yaliyokithiri katika barabara wanazopita kama ishara ya kupinga ubovu wa barabara hizo.
Baadhi ya wakazi hao wa Ghana wameamua kuanzisha kampeni ya kupanda migomba kwenye mashimo yaliyopo kwenye barabara huku mengine yakiwa katikati kwa lengo la kuzikumbusha mamlaka kutambua wajibu wao.
Mbali na Ghana, huko nchini Ukraine nao wanaharakati wake huamua kupanda maua katika barabara mbovu kwa lengo la kuwaamsha watendaji kuzikarabati barabara hizo punde zinapopata hitilafu na kuepusha usumbufu kwa watumiaji.

 Image may contain: outdoor

KUMBUKUMBU YA CHIFU SONGEA:


Serikali imeahidi kurejesha fuvu la kichwa cha Chifu Songea lililonyofolewa na wakoloni wa Kijerumani wakati wa vita vya majimaji mwaka 1906.

Hayo yamesema katika maadhimisho yanayowakutanisha wana Ruvuma na Watanzania wote kwa ajili ya kuwakumbuka mashujaa 66 walionyongwa katika vita ya Majimaji na kupoteza maisha yao wakati wa kupigania ukombozi wao.

Hata hivyo swali linaendelea kubaki ni kwa nini Wajerumani waliamua kuchukua kichwa cha Chifu Songea pekee badala ya vichwa 66.

Floyd Mayweather ajizawadia ndege ya kifahari siku yake yakuzaliwa bofya hapa kuiona

Image may contain: 2 people, people smiling, people standing





Bingwa wa masumbwi wa uzito wa kati
wa Marekani, Floyd Mayweather ameanika ndege binafsi aliyojinunulia kama zawadi ya siku ya kuzaliwa huku ikiambatana na zawadi nyingine kemkem. Mayweather ambaye ametimiza miaka 40 jana, aliangusha bonge la party lililohudhuriwa na watu maarufu mbalimbali kutoka Hollywood


FATUMA Karume, Bob Wangwe Kuishtaki Serikali






BAADHI ya wanasiasa, wanasheria na wanaharakati wametoa tamko juu ya namna ambavyo utekelezaji wa sheria kwenye maeneo mbalimbali ikiwemo uchaguzi na usimamizi wa kesi hususan za viongozi wanaokamatwa kwa hatia mbalimbali. Wakizungumza na waandishi wa habari mapema leo jijini Dar, viongozi wa masuala ya kisheria, siasa, harakati na haki za binadamu, ambao miongoni mwao ni mwanasiasa wa muda mrefu, Makongoro Milton Mahanga, wakili Fatma Karume, mwanaharakati Ensbert Ngurumo, mwananchi wa kawaida, Bob Chacha Wangwe na wengine, walisema katiba ya nchi ya Tanzania inasema kila mtu anayo haki ya kujiingiza kwenye mfumo wa kuiongoza nchi yake. Naye kwa upande wake, Makongoro amesema mahakamani ndiyo sehemu pekee ambapo haki inaweza kupatikana, lakini wao kama Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) wamekuwa wakishindwa kufungua kesi mbalimbali hususan za kiuchaguzi kutokana na sababu zilizo nje ya uwezo wao, ikiwemo kushindwa kuwalipa wanasheria wengi kwa wakati mmoja. Makongoro ambaye amewahi kuwa Naibu Waziri wa Kazi na Ajira katika serikali ya Awamu ya Nne, alisema zipo kesi nyingi za kikatiba zinazotokana na masuala ya uchaguzi ambazo wao kama chama walishindwa kuzifungua kutokana na uchache huo wa wanasheria hadi pale walipoomba msaada wa wanasheria bila malipo ili kuendesha kesi hizo, kwani Chadema haina uwezo wa kuwalipa.

MABADILIKO MENGINE YA RATIBA YAFANYIKA, MCHEZO WA SIMBA VS STAND WARUDISHWA NYUMA

Bodi ya Ligi imefanya mabadiliko ya michezo ya Ligi Kuu Soka Tanzania Bara kwa baadhi ya mechi.

Mchezo wa Simba SC dhidi ya Stand United uliopaswa kuchezwa Machi 4 2018, sasa utachezwa Machi 2 2018.

Vilevile mchezo wa Lipuli dhidi ya Ndanda umesogezwa mbele, badala ya kuchezwa Machi 2, sasa utapigwa Machi 4 2018.

Mechi nyingine ni Kagera Sugar dhidi ya Mwadui FC ambayo ilipangwa kufanyika March 11, sasa itafanyika Machi 13 2018.

Baada ya michezo hiyo kukamilika, Ligi itasimama kwa muda mpaka Machi 22 ili kupisha kalenda ya FIFA ambapo mechi za kimataifa kwa timu za taifa zitachezwa.


MECHI YA YANGA NA MTIBWA YAAHIRISHWA, SASA YAPANGIWA TAREHE HII







 Mchezo wa Ligi Kuu Tanzania Bara ambao ulipangwa kuzikutanisha Yanga na Mtibwa umeahirishwa ili kuipa nafasi Yanga kujiandaa na mchezo wa Ligi ya Mabingwa Afrika.

Mchezo huo ambao ulipaswa kupigwa mapema baada ya Yanga kucheza na Ndanda FC mkoani Mtwara, sasa utapangiwa tarehe nyingine hapo baadaye.

Yanga itacheza mechi yake na Ndanda February 28 2018, na kisha baada ya hapo itapata muda wa kujiandaa na mchezo wa Ligi ya Mabingwa Africa dhidi ya Township Rollers ya Botswana.

Mchezo huo dhidi ya Rollers, utachezwa March 6 2018 katika Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.

TWIGA STARS KUCHEZA NA ZAMBIA AFCON YA WANAWAKE




Timu ya Taifa ya Wanawake(Twiga Stars) itacheza na Zambia katika mchezo wa kufuzu fainali za Africa kwa Wanawake zitakazochezwa Ghana baadaye mwaka huu.
Twiga Stars inatakiwa kucheza mechi zote mbili kati ya April 2 na April 10,2018.
Mchezo huo ni wa raundi ya kwanza.

WATANZANI SITA KUCHEZESHA NA KUSIMAMIA MECHI LIGI YA MABINGWA NA KOMBE LA SHIRIKISHO






Waamuzi wanne wa Tanzania wameteuliwa na Shirikisho la Mpira wa Miguu Africa(CAF) kuchezesha mchezo wa kombe la Shirikisho kati ya Fosa Juniors ya Madagascar na As Port Louis ya Mauritius utakaochezwa Machi 18,2018 Madagascar.
Waamuzi walioteuliwa ni mwamuzi wa kati kati Elly Ally Sassii atakayesaidiana na Ferdinand Chacha mwamuzi msaidizi namba moja na Alli Kinduli mwamuzi msaidizi namba mbili wakati mwamuzi wa akiba atakuwa Alphonce Mwandembwa na kamishna wa mchezo huo anatoka Seychelles, Lewis Blaze Madeleine
Wakati huo Mjumbe wa kamati ya Utendaji ya TFF Ahmed Msafiri Mgoyi ameteuliwa kusimamia mchezo wa Kombe la Shirikisho kati ya Club Desportivo Costa Do Sol ya Msumbuji na Cape Town City ya Africa Kusini utakaochezwa Machi 7, 2018 Estadio Nacional Dol Zimpeto,Maputo
Naye Makamu wa Rais wa TFF Michael Wambura ameteuliwa kusimamia mchezo wa Ligi ya mabingwa Africa kati ya Zesco ya Zambia na Asec Mimosas ya Ivory Coast itakayochezwa Machi 7,2018 Uwanja wa Levy Mwanawasa uliopo Ndola.

SIMBA YAPANGIWA WAAMUZI WA AFRICA KUSINI WATAKAPOKIPIGA NA MAFARAO MACHI 7 TAIFA




Shirikisho la Mpira wa Miguu Africa (CAF) imewapanga waamuzi kutoka nchini Africa Kusini kuchezesha mchezo wa Kombe la Shirikisho Barani Africa Simba ya Tanzania itakapocheza na El Masry ya Misri Machi 7,2018 Uwanja wa Taifa saa 10 kamili jioni.
Mwamuzi wa kati atakuwa Thando Helpus Ndzandzeka akisaidiwa na Zakhele Thusi Siwena mwamuzi msaidizi namba moja na Athenkosi Ndongeni mwamuzi msaidizi namba mbili wakati mwamuzi wa akiba atakuwa Christopher Harrison na kamishna wa mchezo huo Tuccu Guish Chrbremedhin kutoka Eritrea.
Mchezo wa marudiano utachezwa huko Port Said Machi 17, 2018 utachezeshwa na waamuzi kutoka Eritrea .
Mwamuzi wa kati kati atakuwa Yonas Zekarias Ghetre akisaidiwa na Angesom Ogbamarian mwamuzi msaidizi namba moja na Yohannes Tewelde Ghebreslase mwamuzi msaidizi namba mbili wakati mwamuzi wa akiba atakuwa Yemane Asfaha Gebremedhin na kamishna wa mechi hiyo anatoka Libya Gamal Salem Embaia.