Waamuzi
wanne wa Tanzania wameteuliwa na Shirikisho la Mpira wa Miguu
Africa(CAF) kuchezesha mchezo wa kombe la Shirikisho kati ya Fosa
Juniors ya Madagascar na As Port Louis ya Mauritius utakaochezwa Machi
18,2018 Madagascar.
Waamuzi
walioteuliwa ni mwamuzi wa kati kati Elly Ally Sassii atakayesaidiana
na Ferdinand Chacha mwamuzi msaidizi namba moja na Alli Kinduli mwamuzi
msaidizi namba mbili wakati mwamuzi wa akiba atakuwa Alphonce Mwandembwa
na kamishna wa mchezo huo anatoka Seychelles, Lewis Blaze Madeleine
Wakati
huo Mjumbe wa kamati ya Utendaji ya TFF Ahmed Msafiri Mgoyi ameteuliwa
kusimamia mchezo wa Kombe la Shirikisho kati ya Club Desportivo Costa Do
Sol ya Msumbuji na Cape Town City ya Africa Kusini utakaochezwa Machi
7, 2018 Estadio Nacional Dol Zimpeto,Maputo
Naye
Makamu wa Rais wa TFF Michael Wambura ameteuliwa kusimamia mchezo wa
Ligi ya mabingwa Africa kati ya Zesco ya Zambia na Asec Mimosas ya Ivory
Coast itakayochezwa Machi 7,2018 Uwanja wa Levy Mwanawasa uliopo Ndola.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni