Shirikisho
la Mpira wa Miguu Africa (CAF) imewapanga waamuzi kutoka nchini Africa
Kusini kuchezesha mchezo wa Kombe la Shirikisho Barani Africa Simba ya
Tanzania itakapocheza na El Masry ya Misri Machi 7,2018 Uwanja wa Taifa
saa 10 kamili jioni.
Mwamuzi
wa kati atakuwa Thando Helpus Ndzandzeka akisaidiwa na Zakhele Thusi
Siwena mwamuzi msaidizi namba moja na Athenkosi Ndongeni mwamuzi
msaidizi namba mbili wakati mwamuzi wa akiba atakuwa Christopher
Harrison na kamishna wa mchezo huo Tuccu Guish Chrbremedhin kutoka
Eritrea.
Mchezo wa marudiano utachezwa huko Port Said Machi 17, 2018 utachezeshwa na waamuzi kutoka Eritrea .
Mwamuzi
wa kati kati atakuwa Yonas Zekarias Ghetre akisaidiwa na Angesom
Ogbamarian mwamuzi msaidizi namba moja na Yohannes Tewelde Ghebreslase
mwamuzi msaidizi namba mbili wakati mwamuzi wa akiba atakuwa Yemane
Asfaha Gebremedhin na kamishna wa mechi hiyo anatoka Libya Gamal Salem
Embaia.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni