
Shirikisho
la Mpira wa Miguu Africa(CAF) limewataja waamuzi kutoka Burundi kuwa
ndio watachezesha mchezo wa Ligi ya Mabingwa Barani Africa kati ya Yanga
ya Tanzania na Township Rollers FC ya Botswana utakaochezwa Machi
6,2018 kwenye Uwanja wa Taifa saa 10.30 jioni.
Mwamuzi
wa kati atakuwa Pacifique Ndabihawenimana akisaidiwa na mwamuzi
msaidizi namba moja Willy Habimana na mwamuzi msaidizi namba mbili
Pascal Ndimunzigo wakati Kamishna wa mchezo huo anatoka Swaziland
Mangaluso Jabulani Langwenya
Mechi ya marudiano itachezwa Machin 17,2018 nchini Botswana na itachezeshwa na waamuzi kutoka Morocco.
Mwamuzi
wa kati kati atakuwa Redouane Jiyed akisaidiwa na mwamuzi msaidizi
namba moja Youssef Mabrouk na mwamuzi msaidizi namba mbili Hicham Ait
Abou ,mwamuzi wa akiba Samir Guezzaz na kamishna wa mchezo huo anatoka
Africa Kusini Gay Makoena.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni