
Timu
ya Taifa ya Vijana chini ya miaka 20(Ngorongoro Heroes) imepangwa
kucheza na DR Congo kwenye mchezo wa kutafuta tiketi ya kucheza fainali
za Vijana za Africa zitakazochezwa Niger mwezi Novemba.
Mchezo
wa kwanza utachezwa Tanzania kati ya Machi 30,31 na April 1,2018 na ule
wa marudiano utachezwa Congo kati ya Machi 20,21 na 22.
Mshindi katika mchezo huo atacheza na Mali katika raundi ya pili itakayochezwa kati ya Mei 11,12 na 13,2018.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni