mwana wa liganga blog ni blog ya kutoa taarifa, matukio, yaliyotokea katika ulimwengu hususani katika nchi yaTanzania blog hii inasimamiwa na mwandishi wa habari kitaaluma bwana Deus Thomas liganga.lengo ni kutoa taarifa kwa umma,kwa maendeleo ya taifa na Dunia kwa ujumla kwa mawasiliano kuhusu mtangazo, habari, wasiliana nasi 0659944423,deusliganga@yahoo.com,mzeeliganga@gmail.com
Jumanne, 27 Februari 2018
FATUMA Karume, Bob Wangwe Kuishtaki Serikali
BAADHI ya wanasiasa, wanasheria na wanaharakati wametoa tamko juu ya namna ambavyo utekelezaji wa sheria kwenye maeneo mbalimbali ikiwemo uchaguzi na usimamizi wa kesi hususan za viongozi wanaokamatwa kwa hatia mbalimbali. Wakizungumza na waandishi wa habari mapema leo jijini Dar, viongozi wa masuala ya kisheria, siasa, harakati na haki za binadamu, ambao miongoni mwao ni mwanasiasa wa muda mrefu, Makongoro Milton Mahanga, wakili Fatma Karume, mwanaharakati Ensbert Ngurumo, mwananchi wa kawaida, Bob Chacha Wangwe na wengine, walisema katiba ya nchi ya Tanzania inasema kila mtu anayo haki ya kujiingiza kwenye mfumo wa kuiongoza nchi yake. Naye kwa upande wake, Makongoro amesema mahakamani ndiyo sehemu pekee ambapo haki inaweza kupatikana, lakini wao kama Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) wamekuwa wakishindwa kufungua kesi mbalimbali hususan za kiuchaguzi kutokana na sababu zilizo nje ya uwezo wao, ikiwemo kushindwa kuwalipa wanasheria wengi kwa wakati mmoja. Makongoro ambaye amewahi kuwa Naibu Waziri wa Kazi na Ajira katika serikali ya Awamu ya Nne, alisema zipo kesi nyingi za kikatiba zinazotokana na masuala ya uchaguzi ambazo wao kama chama walishindwa kuzifungua kutokana na uchache huo wa wanasheria hadi pale walipoomba msaada wa wanasheria bila malipo ili kuendesha kesi hizo, kwani Chadema haina uwezo wa kuwalipa.
Jisajili kwenye:
Chapisha Maoni (Atom)
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni