Wakenya wamejitokeza kwa wingi kulitazama na kupigwa picha na Kombe la
Dunia la Shirikisho la Soka Duniani (Fifa) ambalo limekuwa nchini humo
kwa siku mbili.
Kombe hilo ambalo liliwasili nchini Kenya na kupokelewa na Rais wa nchi
hiyo, Uhuru Kenyatta lilipata watazamaji wengi ambao walifika kujionea
na kupiga picha pamoja na kombe hilo.
Raia wa kawaida hawakuruhusiwa kuligusa kombe hilo, na badala yake walilitazama likiwa katika sanduku la Kioo.
Ni rais huyo pekee aliyeruhusiwa kuligusa kombehilo nchini Kenya. Kando
na marais, ni wachezaji waliowahi kushinda kombe hilo pekee ambao
huruhusiwa kuligusa.
Kombe hilo linatembezwa mataifa mbalimbali kabla ya michuano ya Kombe la
Dunia kuanza Juni, nchini Urusi. Na ni mara ya tatu kwa kombe hilo kuwa
nchini Kenya, awali ikiwa 2010 na 2013 katika ya fainali zilizofanyika
Afrika Kusini na Brazil.
Kabla ya kutua Kenya, kombe hilo lilikuwa nchini Sudan kisha Ethiopia.
Hata hivyo ziara ya kombe hilo bado inaendelea ambapo limeondoka nchi Kenya na kuelekea Maputo, Msumbiji.
Nchi nyingine za Afrika zinazotarajia kufikiwa na ziara hiyo ya Kombe la
Dunia ni Afrika Kusini, Uganda, Nigeria, Senegal, Cote D’Ivoire (Ivory
Coast) kisha Misri.
Baada ya ziara ya kombe hilo barani Afrika kukamilika, litaelekea barani
Ulaya kuendelea na ziara yake kabla ya kuanza mchuano ya Kombe la Dunia
itakayofanyika nchini Urusi, Juni 14, mwaka huu.
Hapa chini ni ratiba nzima ya ziara ya Kombe la Dunia katika nchi
mbalimbali duniani. Zipo nchi ambazo tayari zimeshatembelewa na nyingine
zinaendelea kutembelewa.
Kituo Tarehe
Colombo, Sri Lanka 23-24 January
Male, Maldives 24-25 January
Phuket, Thailand 26-27 January
Vientiane, Laos 28 January
Macau, China P.R 29 January
Nukualofa, Tonga 31 January
Honiara, Solomon Islands 1 February
Port Moresby, Papua New Guinea 1 February
Lahore, Pakistan 3 February
Almaty, Kazakhstan 4 February
Bishkek, Kyrgyz Republic 5 February
Dushanbe, Tajikistan 5 February
Tashkent, Uzbekistan 6 February
Ashgabat, Turkmenistan 7 February
Yerevan, Armenia 7 February
Tblisi, Georgia 8 February
Baku, Azerbaijan 9 February
Valetta, Malta 10 February
Vienna, Austria 11 February
Minsk, Belarus 13 February
Sofia, Bulgaria 14 February
Tel Aviv, Israel 15 February
Larnaca, Cyprus 16 February
Ramallah, Palestine 17-19 February
Amman, Jordan 20 February
Dubai, United Arab Emirates 21 February
Khartoum, Sudan 22-23 February
Addis Ababa, Ethiopia 24-25 February
Nairobi, Kenya 26-27 February
Maputo, Msumbiji 28 February
Johannesburg, Afrika Kusini 1-2 March
Cape Town, Afrika Kusini 3 March
Kampala, Uganda 5-6 March
Abuja, Nigeria 7-8 March
Lagos, Nigeria 9-10 March
Dakar, Senegal 11-12 March
Abidjan, Cote d’Ivoire 13-14 March
Cairo, Misri 15-16 March
Naples, Italy 17-19 March
Paris, France 20-21 March
Cologne, Germany 22-23 March
Oslo, Norway 24 March
Torshavn, Faroe Islands 24-25 March
Reykjavik, Iceland 25 March
Tucuman, Argentina 27-28 March
Berazategui, Argentina 29 March
Buenos Aires, Argentina 30-31 March
Rosario, Argentina 1-2 April
Bogota, Colombia 3-5 April
Panama City, Panama 6 April
San Jose, Costa Rica 7-8 April
Guadalajara, Mexico 9-10 April
Monterrey, Mexico 11-12 April
Mexico City, Mexico 13-15 April
New York, USA 16 April
Miami, USA 17 April
Los Angeles, USA 18-20 April
Frankfurt, Germany 22 April
Ulaanbaatar, Mongolia 23 April
Beijing, China P.R 25 April
Shanghai, China P.R 26 April
Tokyo, Japan 27-28 April
Osaka, Japan 29-30 April
Vladivostok, Russia 1 May
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni